CAG afanye ukaguzi kwa asilimia 100 katika baadhi ya wilaya kwa kila mkoa

OPORO

Member
Apr 22, 2012
59
14
Wapendwa wana JF,Ukaguzi unaofanywa na CAG ni sampuli (Auditing by Sample) matokeo yake hatupati ukweli wote na kwa maana ya ukaguzi ni kutoa maoni ya kiutalamu tu na siyo uhakika kamili.Ukaguzi ambao umekuwa ukifanyika katika wizara,mashirika,mikoa na wilaya zote umekuwa ni wa sampuli na hauwezi kufuchua uozo wote uliopo katika taasisi zetu.

Ili kuweza kusaidia nchi hii,CAG afanye ukaguzi wa asilimia mia 100% kwa baadhi ya wilaya kwa kila mkoa,kwa mfano mkoa wa mwanza ina wilaya sita,CAG afanye ukaguzi wa asilimia mia kwa wilaya 3 au 2 ili kuweza kutoa picha halisi kwa kila mkoa,ukaguzi huu utaweza kusaidia kwa kufichua hali iliyopo katika wilaya zetu,wizara na mashirika.

Lakini wakaguzi kutoka ofisi ya CAG nao walipwe malipo yatakayowawezesha kufanya ukaguzi tofauti na hali ilivyo sasa,ukaguzi tunaopata matokeo yake ni nusu au robo ya hali halisi katika taasisi zetu.

Naomba maoni yenu
 
Ni kweli kabisa C.A.G anafanya ukaguzi kwa kutumia sampling method ila pale panapokua na mashaka hufanya full auditing .
Haitakua rahisi kwa resource zilizopo kwa sasa kufanya aina hiyo ya ukaguzi hadi zitakapoongezwa rasilimali watu na fedha.
Tatizo kubwa hapa ni serikali legelege na yenye kulinda mafisadi na watenda maovu
 
hakuna kitu kinaitwa 100% audit.. auditor anatoa reasonable assurance na sio absolute assurance..haiewezekani kufanya 100% Audit kwa CAG au hata cjui KPMG au PWC..In Audit profeshen ambayo ina deal na past information only ukaguzi utafanywa kwa sampling unless other means ni rahisi zaidi...Plz usicomment km hujui utaratibu wa profesheno husika..okbye
 
Back
Top Bottom