bemg
JF-Expert Member
- Apr 25, 2010
- 2,799
- 642
weka muda
Heshima kwenu wapenzi wa soka wote,,
Wadau leo ndo leo kwenye african football as 2nd league ya semi finals inapigwa leo usiku mjini Tunis kwenye uwanja wa nyumban wa esperance baada ya kuwalazimisha sare Tp mazembe mjini lubumbash kwenye uwanja wao mpya na wa kisasa The new mazembe stadium,, wadau wa soka mnahis leo nani anaondoka?
Mbwana samatta na imani atakuwa katika mechi kubwa sana kwake as makocha wa team zote kubwa ulaya huwa wanaangalia mechi kama hizi as ndo word class match in clubs level kutoka africa...
On my views nahisi kama Mazembe anaondoka as game 1 waarabu walitisha sana.. Wadau mnaonaje?
Super sport 9 wanarusha game live leo usiku, mashabiki wa simba na yanga naomba tuangalie hii mechi ili tujue vilabu vyetu vipo nyuma kiasi gani... Maana spidi inayopigwa humu na pass za haraka haraka ni kama ulaya...
Tusisahau kutazama na kesho Semi finals nyingine between SUNSHINE STARS VS AL HALY as sunshine from Nigeria mjini igejebuje akiwa away kujaribu kufosi ushindi baada ya kulazimishwa sale nyumbani igejebuje nigeria...
Kwa match za kwanza nilivyoona nikagundua Simba na Yanga ni bado sanaaaa kufika level hizi za kucheza champions league semi finals.. Hawa watoto wa nigeria wana dogo anaitwa Azuka a University of lagos student first year ndo amesimama mbele pale ni balaa tupu ambaye scouts wa ulaya wanamzingira daily na anamalizia msimu aelekee zake ufaransa wakati wa dirisha dogo,,,, Wapenda soka wote naomba mumcheki kisha muone wakina Okwi sijui Twite walivyo magumashi....
Goli la offside
mazembe out
Mkuu, umezungumza points za nguvu saana na umetoa elimu kubwa kwa wachezaji wetu na mashabiki wa soka. wachezaji wetu hawana makosa ila serikali za awamu mbili za mwanzo zinafaa kubeba lawama zote hizi. Hakuna hata nchi moja iliyoshabikia ukomunisti hapa dunniani ikatamba kisoka. Soka letu lilibomoka mwaka 1976 wakati serikali chini ya waziri wa michezo wakati huo mirisho sarakikya alipowafukuza Tambwe Leya na Nabi Kamara. Jiulize kwanza kwa nini serikali iliwafukuza wataalamu waliokuwa wanleta soka la kisasa kwa vijana wetu? halafu kutokuwa na television kwa miaka 30 ya ujamaa na kujitegemea kulichangia sana vijana wetu kutokwenda na wakati na soka.Nakubali soka letu linaharibiiwa na kilabu hizi kubwa na wachezaji wetu hawana mtazamo wa kujiendeleza. kisoka
[1].mazoezi ya nguvu hawataki kufanya,
[2].wanaweka imani za kishirikina zaidi.
[3].hawana mipango wala hawataki kujifunza kwa wengine.[eti wakiona mkanda wa sebene wanaweza kuiga vizuri ,lakini sio soka la wengine.
[4].Mchezaji wetu akipata TZS.20m anakimbilia kununua gari badala ya kufanya yafuatayo;{kutenga pesa kidogo ajifunze kifaransa,atenge pesa atengeneze master CD ampe wakala,atenge pesa kidogo ajifunze kutumia kompyuta na kufungua Email,atenge pesa kidogo atafute mwanasheria wake kwa ajili ya mikataba,atenge pesa kidogo amtafute msemaji wake.!!!YOTE HAYA HAYAZIDI TZS.3,000,000/=}
[5].Mchezaji akifika simba au yanga basi anjiona amefika.!!
[6].timu zinacheza kwenye media zaidi ya uwanjani.
[7].Viongozi wanataka ulaji na umaarufu tu.