cable tv za mikoani...

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,884
ukienda mikoani unakuta kuna watu tofauti wana toa huduma ya cable tv

cha ajabu kwenye cable hizo unakuta channel zote za local na
zingine mfano supersport na kdhalika kwa bei nafuu mno
while watu wa dar wanalia na gharama za dstv au ubovu wa star times....

sasa swali ni hili

ni teknolojia ipi wanatumia hawa wenye cable za mikoani kurusha
channel nyiingi na kuchanganya zoote za dstv na zingine?
je ni halali?

na mtu ukitaka uweke tu kwa matumizi ya nyumbani inakuwaje?
 
Mkuu hizo cable za mikoani chaneli nyingi ni za mazabe, anapokwenda kuomba kibali cha kusambaza cable anatakiwa mwenye cable atafute uhalali wa kupewa haki ya kurusha vipindi kutoka kwa wahusika wenye chaneli kitu ambacho hawafanyi, vinginevyo wanatakiwa kurusha free chaneli tu kama hawana vibali vya kufanya hivyo

Kwa hapa DSM walikuwepo zamani lakini DSTV wakawakomalia kupitia mamlaka husika kuhakikisha hawaonyeshi mpira wala chaneli zote wanazorusha wao maana ni wao tu wana mamlaka ya kurusha chaneli hizo hivyo cable zikafa kibudu, na hii ni kwasababu DSTV soko lao kubwa wamebase zaidi hapa DSM

Wanachofanya wale jamaa ni kuwa na dish na receiver let say ya DSTV na zingine kisha wana ziunga kwenye cable, wanasambazia wateja na kukusanya mapato wakati DSTV wanalipa kama single user(personal use), na most of time chaneli ni hizo hizo za DSTV kama supersports, MM, mnet nk
 
nilifikiri kuna aina ya dish unaweza pata channel zoote hizo
nitafute na mimi
 
Nipo mkoani tabora ninapata chanel zote za mipira,movies,news nk bureeeee!NIMECHAKACHUA!ila kwa mwezi unalipia 10000 na kampuni nyingine 7000.zipo chanel zaid ya 55.MECHI YOYOTE YA ULAYA KUANGALIA UKIWA TABORA NI SH.100 wakati dar ni 500 mpaka 1000!sina mpango wa kununua startimes wala ting
 
Mkuu umenikumbusha mbali sana kuna jamaa anaitwa shashi na califonia cable yani dah kila kitu laivu, nikajua bongo wanainjoy zaidi kumbe dah huku full mizinguo
 
Nipo mkoani tabora ninapata chanel zote za mipira,movies,news nk bureeeee!NIMECHAKACHUA!ila kwa mwezi unalipia 10000 na kampuni nyingine 7000.zipo chanel zaid ya 55.MECHI YOYOTE YA ULAYA KUANGALIA UKIWA TABORA NI SH.100 wakati dar ni 500 mpaka 1000!sina mpango wa kununua startimes wala ting

Mkuu tumwagie mautundu nasisi basi
 
Nipo Moshi; cable zipo mbali kidogo. natumiam dishi la futi 6
 
Halafu hizo cable ziko pouwa sana, kwam fano pale mtwara kuna huyu jamaa Abdul Shaban wa pale mtwara guest ana kitu inaitwa mtwara cable yaani channels zote a mipira ya ulaya especially EPL utaziona labda sionyweshe muda mmoja. Na huduma zake kuvutia ni 30000 na 10000 monthly, this is better than Star Times, na mara nyingi mipira inaonyeshwa through channels za kiarabu
 
Huyo anaesema chanel ni za mazabe naona hajui hii kitu,mi niko Mwanza nimeunganishiwa hiyo cable kwa mwezi 15,000 naona mechi zote za ulaya na hawa jamaa wana nguzo za kupitisha cable zao mji mzima hadi mbele ya ofisi ya DSTV wameweka nguzo yao.na pia katika hizo channel wanazo channel zao wanarusha vipindi vyao wao wenyewe na ndizo hizo wanatumia kutuonesha mechi za CAN.
 
Cable ya Bukoba ni funika mbaya, zinapatikana channels kama HBO,Star Movies,Dubai Sport,Super Sport,Channel zote za bongo,Kenya,Uganda,Zambia,SABC zote,MBC zote, channel ya DSTV inayoonyesha movie za kiswahili,Filmax,Macau,MTV,Trace,Discovery,CNN,Aljazeera n.k. kwa sh 12,000 kwa mwezi
 
Huyo anaesema chanel ni za mazabe naona hajui hii kitu,mi niko Mwanza nimeunganishiwa hiyo cable kwa mwezi 15,000 naona mechi zote za ulaya na hawa jamaa wana nguzo za kupitisha cable zao mji mzima hadi mbele ya ofisi ya DSTV wameweka nguzo yao.na pia katika hizo channel wanazo channel zao wanarusha vipindi vyao wao wenyewe na ndizo hizo wanatumia kutuonesha mechi za CAN.

mkuu fanya utafiti tu ndio utajua kwanini tunasema za mazabe.
Yaani DSTV walipe milions of dola halafu wewe ununue dish na recever kama mteja wa kawaida kisha uanze kuwasambazia watu kwa malipon hiyo unaona ni sawa? Ukiona hivyo wameamua kupotezea kibongo bongo
Jiulize kwanini bongo hazijasambaa zipo chache kwa wahindi na bei ni juu
Ni DSTV pekee ndio wenye haki ya kuonyesha vipindi vyao kama spersports zoten mm, mnet nk wengine wezi tu labda waonyeshe chaneli za bure
 
Tafuta dish la ft 8 lenye rotater na receiver inayoitwa WIZTECH HD,hizo channels za kulipia unazikamata zote for free!

Mkuu unaleta hadithi wewe. Hakuna kitu kama hicho vinginevyo watu wange fanya hivyo kuliko kulipishwa midola ya DSTV kila mwezi
 
Nyie wa mjini ndo mnaoangaishwa nahivyo ving'amuzi sisi huku mikoani tunakula vitu vya Multichoice bureeeeeee kwa bei nafuu kwenye cable.
 
Mkuu kweli mnafaidi, nilikuwa Singida juzi kati kuna cable mbili ya Mohamedi na Faisali malipo sh 5000 kwa mwezi
Yaani ni full APL
 
Back
Top Bottom