Cabinet reshufle coming tomorrow?!

Jamani acheni aende popote huyu mtoto anafaa sn, sijaona MP mwenye mipango yakaribu km huyu mtt, kweli heshima ya manyuzi naamini ataiweka mbele, mm si mpenzi wa CCM ila mtu afanyavyo vizuri lazima tumpe hongera.

Sijaona MP hata mmoja wa CCM ambaye yuko tayari kukataa Lunch box ya 1m na kuwaambia wenzake, kama mwenyekiti hakuwa tayari kupokea 1m km lunch kwani ni hongo, kunachakula gani cha sh. mil. 1, anastahili hata akiwa FM namfagilia sana, naamini nchi itabadilika, wacheni vijana wachukue usukani kwenye jahazi linaloyumba watawasaidia wazee kufika mahali palipokutegemewa.

Je alivyokuwa anaipigia debe DOWANS ulijiuliza kama ile ilikuwa hali ya kawaida au alikuwa na msukumo fulan?

Chunguza njomba utabaini...!
 
Ni kawaida ya CCM kupoozana< haiwezekani Mzee Mzima Makamba atoswe hivi hivi tuu,; wajinga ndio waliwao; wataoamini kuwa wamejivua gamba kiweli kiweli!!!!
 
Ok now January's dreams of becoming president are a step closer... Membe is weak ndio ukweli wenyewe huo... JK huwezi jua anania gani. Anaweza mpa shavu mtu yeyote ata 2025 kama vipi ile dogo Magogoni mbona sana tuu.. EL atachakachuliwa...his power and influence peaked a lil too early...mahesabu mabovu... U need to be powerful but at the right time, maadui wasipate nafasi yakujibu mashambulizi... Nasubiri kuskia kina Chenge itakuwaje... CHenge wampoteze tuu.
 
Siwezi kushangaa hilo kwani mwanzoni baada ya uchaguzi miye nilitegemea JM aende Foreign kwa sababu zangu binafsi; kwa hiyo hata kupelekwa huko kwa CCM nadhani ni part ya kitu kile kile. Lakini itakuwa ni aibu kufanya mabadiliko ya baraza la mawaziri hata mwaka haujapita..

Mawaziri waliokuwa na kofia ya Chama, yaani cheo kwenye Sekretariat, wamenyang'anywa hicho cheo. Hii ndio sababu hasa ya kumtoa Membe (lakini vile vile kwasababu ana kundi lake la kuwania Urais). Kulikuwa na tatizo hapo kabla ambapo Membe, Chiligati, Mkuchika wote walikuwa kwenye Sekretariat na pia ni Mawaziri. Kwahiyo basi sitegemei anytime soon kwamba JM atapewa uwaziri MOFA halafu abaki kwenye Sekretariat ya Chama.

But at the end of the day, you serve in the cabinet at the pleasure of the President!
 
Kuhusu J Makamba sikubaliani na wanaomsifia,bado nammweka kwenye kundi la watu ambao misimamo yao haieleweki

Kwa nyongeza bado anagamba la baba yake ambaye hakuwa na hekima ya kuongoza chama na aliyejaa ulopokaji. Pia conflict of interest, kama baba yake aliweza kukigawa chama, na watu haohao anaotakiwa JM awaongoze, je hata kuwa na kisasi? na je hao anaowaongoza wenye visasi na baba yake hawatamzushia mambo ili aonekane hafai? Kwa hiyo kijana JM ana kazi ya kuunganisha wale wote waliokuwa wameikatia matumaini CCM, la sivyo ataishia kuwa mropokaji kama baba yake
 
Last edited by a moderator:
Kama bwana atawatamalaki watu hao na iwe kwao baraka, ila wasijesahau uongozi ni dhamana.
 
Acheni kupaparuka ina Maana Zakia Meghji atakuwa Waziri wa Fedha?

Hizo kamati za chama wote ni Wabara? Hakuna Wazanzibari ? Au ndio Maana Z'Bar walimkataa Naibu Katibu Mkuu aliyechaguliwa na Kikwete?
 
Kuteuliwa kwa January Makamba kuongoza Idara ya Mambo ya Nje ya CCM kunaashiria mabadiliko ya haraka ya Baraza la Mawaziri, ambapo Januari atachukua nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje. Hii ni kwa sababu mbili:

-Waziri wa Mambo ya kawaida ndiye Mkuu wa Idara hii ya CCM
-Membe ameondolewa katika idara hii na pia hayumo hata katika Kamati Kuu.
vipi januari lile bifu lake na bibi mmoja wa marekani limeishia wapi?
 
images
 
ccm hizi ndizo siku za kufa nyani miti yenu yote mnayokwea inateleza tu hiyo safu mliyoitangaza wala si ya ushindi km ni ufisadi ccm kuanzia mwenyekiti wao mpaka sijui nani huko wote ni mafisadi tuu. mmejivika gamba la chatu sasa mtatumeza wooote lkn 2015 mtatutapika tuu halafu we will attend your funneral CCM!! at kisutu cemetery.
 
Acha ushabiki usio na maana alikataa milioni moja kwa uzalendo au kwa kuw Dowans walishamkatia?? Hivi Tanzania ni nchi ya Kifalme??? lazima awepo Kinana, Kigoda, Mwinyi, Makamba Families kila mahala??? maanake hakuna watanzania wengine wenye upeo UPUUZI MTUPU...........
 
Kweli M k w e r e anatapatapa. Alipowachagua miezi 5/6 iliyopita alitumia vigezo vipi na inakuwaje chini ya nusu mwaka anajaribu tena kuwahadaa walipa kodi? Kuna haja kubwa ya kutokuwa na imani na hii serikali ya kishkaji shkaji. Fedha za walipa kodi zinapotea kwa sababu ya uzembe wa m k w e r e. Bado M k w e r e hajafanya lolote la maana tangu aibe kura za uchaguzi mkuu na matatizo ya mfumuko wa bei ndio usiseme wakati hajaziba ile mianya ya mafisadi kuchuma kwenye shamba la bibi bila kulipa kodi.


Nchi masikini lakini tunaambiwa kodi ya 3 brmd apartment ni USD 4000.00 kwa mwezi tena inalipwa kwa mkupuo moja, Je, ni kazi gani hiyo inayoweza kumfanya mtu Oooops Fisadi alipe hivyo bila wasi wasi kama kweli inalipa kodi kwa mujibu wa sheria? Mazingaombwe ya JK ni lazima yasitishwe, hawezi kuyasitisha yeye mwenyewe ni sisi walipa kodi pekee ndio tuna uwezo wa kumwambia amefikia tamati.
 
Kuteuliwa kwa January Makamba kuongoza Idara ya Mambo ya Nje ya CCM kunaashiria mabadiliko ya haraka ya Baraza la Mawaziri, ambapo Januari atachukua nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje. Hii ni kwa sababu mbili:

-Waziri wa Mambo ya kawaida ndiye Mkuu wa Idara hii ya CCM
-Membe ameondolewa katika idara hii na pia hayumo hata katika Kamati Kuu.

Kama baraza litavunjwa, I bet Six for PM. Pinda is a total failure, na kama Sitta atakuwa PM anaweza leta imani kwa baadhi ya watu kuwa huenda JK kaamua kuwa sasa ni kazi tu miaka mitano ya kulipa fadhila imetosha.
 
Je alivyokuwa anaipigia debe DOWANS ulijiuliza kama ile ilikuwa hali ya kawaida au alikuwa na msukumo fulan?

Chunguza njomba utabaini...!

Ndio nyie akina "bora mgao kuliko kuwasha Dowans". Mnatanguliza siasa mbele kuliko common sense.
 
Back
Top Bottom