Cabinet Baada Ya Lowassa: Waziri Mkuu Mpya Atakuwa Nani?

Wana JF, Jakaya kama kweli anataka kutupeleka sehemu njema basi uchaguzi wa PM usiwe wa kirafiki kama ilivyokuwa kwa Lowasa.

Kwa sasa katika CCM ni wachache sana ambao wako safi, na hao ni kama Shein, Msekwa, Makinda na Mwandosya. Na ni kati ya hawa wanne ndiyo wenye uwezo wa kuwadhibiti mawaziri wengine - natoa hoja.
 
hivi kwanini hamuelewi kuwa PM akijiuzulu lazma baraza nalo hua linavunjwa by convention. 80% ya mawaziri watarudishwa... KEEP THT IN MIND>>>
 
Kwa mara ya kwanza kabisa, Tanzania yetu itakuwa miongoni mwa nchi zenye demokrasia ya juu na yenye kujali usawa na haki za wanawake.....itapata Waziri Mkuu wa kike, naye ni Mama Makinda!!
 
Its Un Believable Kuwa Baadhi Ya Wanachama Wa Jambo Forum Bado Wana Akili Za Kutaka Tuendelee Kurecycle Wanasiasa Wale Wale

Nimemuuliza Fikiraduni Whats So Special About Malecela Hajanijibu

Nimemuuliza Kipi Kipya Wasira Ataleta Hajajibu

Halafu Huyu Huyu Analalamika Kuwa Itabidi Tubadili Watawala

Ama Kweli Ukistaajabu Ya Musa Utashangaa Ya Firauni
 
Habari zinazoifikia intelligence unit yangu na wenzangu zinasema kuwa Kikwete atampendekeza Mama Ana Makinda kuwa waziri mkuu mpya wa jamhuri ya Tanzania.

Source karibu kabisa na Kikwete zinasema kuwa wanamtandao wanataka kuwa na mtu ambaye hana ambition za uraisi na wala hana nafasi ya kumfunika Kikwete katika utendaji kazi wake.

Kumbuka hii habari inaweza kubadilika kutokana na upinzani fulani unaoonyesha na waziri mmoja ambaye ni rafiki mkubwa wa Kikwete na ambaye anasubiria hii nafasi kwa hamu kubwa pia.

Wana JF watch this thread wakati hii habari ikiendelea kufunguka na uhakika wote ukiendelea kuwekwa kuwa Kikwete hatabadilisha mawazo yake katika hatua za mwisho mwisho kama alivyofanya b4

.....

My Take......

Kwa vile inaonekana PM atakuwa chaguo la kikwete, binafsi ninaunga mkono Mama Makinda for PM! at least for now....

tik tak tik tak tik......
 
the guy is not serous

hivi huyu mama amekuwa madarakani for how many years?

WTF is wrong na huyu JK?
 
mie mbona habari zilizo nifikia ni kati ya mdhihiri na bendera!!!! ziangalie tena duru zako......lol.
 
Kwa rekodi hii...I will put my money on Membe.

Membe Bio...

Ministry of Foreign Affairs Ambassador advisor 1992 2000

President's Office - Defence and National Security National Security Analyst 1977 1990

Ministry of Energy and Minerals Deputy Minister 10/17/2006 1/11/2007

Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation Minister 1/12/2007

Ministry of Home Affairs Deputy Minister 1/1/2006 10/16/2006
 
By the way MWK,
sikuona sababu ya kuanzisha hii thread mpya wakati kuna ingine inayoendelea

Mods please merge this threads
 
Kwa rekodi hii...I will put my money on Membe.

Membe Bio...

Ministry of Foreign Affairs Ambassador advisor 1992 2000

President's Office - Defence and National Security National Security Analyst 1977 1990

Ministry of Energy and Minerals Deputy Minister 10/17/2006 1/11/2007

Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation Minister 1/12/2007

Ministry of Home Affairs Deputy Minister 1/1/2006 10/16/2006


Membe anafaa kuwa waziri wa mambo ya Ndani kwa profile hiyo au waziri wa Ulinzi

lakini vile vile hiyo siyo carte blache apewe tuu kwa sababu:

hakuna aliyefanya tathmini ya mafanikio yake katika hizo posti ulizozitaja hapo juu


Kuwa Defence na analyst haitoshi kwani kwa cheo hicho basi AGOSTINO MAHIGA ndio mwenye kazi yake
 
By the way MWK,
sikuona sababu ya kuanzisha hii thread mpya wakati kuna ingine inayoendelea

Mods please merge this threads

Kila mtu yuko stressed na JK na serikali yake na hilo baraza lake la mawaziri

kama hupendi kusoma threads mpya you have a choice ya kwenda kwenye michezo na burudani

hebu tupe nafasi humu
 
By the way MWK,
sikuona sababu ya kuanzisha hii thread mpya wakati kuna ingine inayoendelea

Mods please merge this threads

Hii ni tofauti na zile ila kama unataka kupewa u-MoD na kuziunganisha basi ni vyema ukafanya hivyo ila kesho utawishi hii thread ilikuwa independent!.... tik tak tik tak tik tak..
 
Back
Top Bottom