C.C.M tukiri udhaifu!!

Goooooooooood!!!!!!!! Lakini huwezi kujiita msafi wakati umekaa jalalani, nenda sehemu safi ili udumishe usafi wako. Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeees ...............................................................!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Umesema ukweli kabisa!...Hata Obama baada ya kuingia madarakani na kuona upinzani wa Republicans unazidi alilazimika kutembea majimboni kutafuta kuendelea kuungwa mkono kwenye sera zake mpya za afya na ajira.Hakulalamika kama Kikwete kusema kama kuna hati miliki ya ikulu na kwamba ukishaingia madarakani basi "live us alone" tutawale hadi uchaguzi mwingine uje ili tuibe kura na kurudi tena.Hakuna sababu za kuendelea kutawala kama huna wananchi wa kutosha kukuunga mkono.Halafu kulalamika kwa kutegemea kuhurumiwa na kuungwa mkono hakuwezi kuwashawishi wananchi ambao maisha yao yanaendelea kuwa magumu kila kukicha!.
 
Sidhani kama tuna huo utaratibu, kukosoana imeshakuwa desturi yetu vinginevyo Mwakymbe tusingekuwa naye mpaka leo

ripoti ya mwakyembe na wenzake ilijaa mambo ya juu juu sana, hata yeye alikiri hivyo. wangeanika kila kitu, wangeshasomewa hitma siku nyingi!!
 
mimi ni mwanachama wa c.c.m, na kiongozi ndani ya chama katika ngazi ya wilaya lakini kwa mara ya kwanza nalazimika kusema ukweli, malalamiko ya viongozi wetu ngazi ya taifa kuhusiana na maandamano ya chdema yalenge katika ukweli, tujiulize hawa watu wanalaumu nini? Na wanawaambia nini wananchi? Kuna ukweli ndani yake? Kama hakuna ukweli kwa yale wanayoyasema tuwashitaki haraka iwezekanavyo, nahisi kama hatuwatendei haki kusema wana dhamira ya kumwaga damu, so far sijaona kosa walilofanya na ndo maana hawajapelekwa mahakamani na wakapatikana na hatia hizo, unajua kwa haya malalamiko yetu inaonyesha hatutaki changamoto za kweli na hatupendi vyama vya upinzani viwe strong. Nadhani sisi kama chama tuwe wa kweli wananchi wamechoka na maisha duni yanayozidi kuwa makali kila kukicha nadhani umefika wakati sasa viongozi wetu kutekeleza ilani zetu kwa vitendo na tusifanye siasa katika hili, tukiri katika utawala huu mambo yamekuwa tofauti sana ukilinganisha na vipindi vilivyopita kwa mfano itakuwa ni busara sana tukitumia muda mwingi kujibu maswali yanayoulizwa kwa mifano hai ya utekelezaji wa tuliyo waahidi kuliko kulaumu tu na umefika wakati sasa tuwe na ahadi chache na zinazotekelezeka ni hatari kuahidi maisha bora kwa kila mtu ilihari hata nchi tajiri zinapata changamoto kubwa sana kufikia hiyo hatua, tunatakiwa tujipange vinginevyo watatushinda kwa hoja mbele ya wananchi.

msema kweli ni mpenzi wa mungu.

wewe una akili sana. Kama watu wote wangekuwa rational namna hii, nadhani hata chadema wasingezuka huku na kule kusema ukweli. Cha ajabu mnakataa kuwa hamna shida, hii ndo inaudhi. Lakini mgekubali na mkasema ni kweli nchi ina shida basi tushirikiane tutatue matatizo, wala kusingekuwa na shida. Honera mkuu una akili sana bado nasema
 
Najua unachokitaka nikwambie wilaya gani, japo haita saidia sana. Sita ondoka katika chama nitabaki humu humu ila sitakuwa mnafiki from now onward inasikitisha sana kama kiongozi kuunga mkono hata pale tunapokosea. Kwa mfano hivi ni kipi naweza kujivunia katika ahadi zetu za awamu iliyopita kama utakuwa makini nenda kazisome vizuri na utekelezaji wake una-ripotiwa kisiasa zaidi. Mimi binafsi maisha yangu siyo mabaya sana lakini nina ushahidi wa watu wanaonizunguka.

Ukisikia kitu kinaitwa UNAFIKI ndicho unacho kifanya your good for nothing.
 
Mimi ni mwanachama wa C.C.M, na kiongozi ndani ya Chama katika ngazi ya Wilaya lakini kwa mara ya kwanza nalazimika kusema ukweli, Malalamiko ya viongozi wetu ngazi ya Taifa kuhusiana na maandamano ya CHDEMA yalenge katika ukweli, tujiulize hawa watu wanalaumu nini? na wanawaambia nini wananchi? kuna ukweli ndani yake? kama hakuna ukweli kwa yale wanayoyasema tuwashitaki haraka iwezekanavyo, nahisi kama hatuwatendei haki kusema wana dhamira ya kumwaga damu, so far sijaona kosa walilofanya na ndo maana hawajapelekwa mahakamani na wakapatikana na hatia hizo, unajua kwa haya malalamiko yetu inaonyesha hatutaki changamoto za kweli na hatupendi vyama vya upinzani viwe strong. Nadhani sisi kama chama tuwe wa kweli wananchi wamechoka na maisha duni yanayozidi kuwa makali kila kukicha nadhani umefika wakati sasa viongozi wetu kutekeleza ilani zetu kwa vitendo na tusifanye siasa katika hili, tukiri katika utawala huu mambo yamekuwa tofauti sana ukilinganisha na vipindi vilivyopita kwa mfano itakuwa ni busara sana tukitumia muda mwingi kujibu maswali yanayoulizwa kwa mifano hai ya utekelezaji wa tuliyo waahidi kuliko kulaumu tu na umefika wakati sasa tuwe na ahadi chache na zinazotekelezeka ni hatari kuahidi maisha bora kwa kila mtu ilihari hata nchi tajiri zinapata changamoto kubwa sana kufikia hiyo hatua, tunatakiwa tujipange vinginevyo watatushinda kwa hoja mbele ya wananchi.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

Tuchukue ule usemi usemao CCM wanaogopa kivuli chao wenyewe. Na wanakiongopea kivuli chao sio watanzania, watanzania walishaamka sio wale wa jana. Kama CCM ilikuwa ni ya kubadilika au inayokubali kukosolewa isingeshambuliana na CHADEMA, wao wangekuwa mstari wa mbele kufanya kazi na kutekeleza ahadi zao kwa wananchi. Lakini wao wanahangaika kutafuta mbinu ya kukiua chama cha CHADEMA ambacho kinaendelea kupata nafasi zaidi ya kujiimarisha. Mimi baba yangu mdogo alikuwa amepanga nyumba ya mjumbe mmoja wa CCM lakini alimfukuza eti kwa ajili ni mwanachadema. Eti hataki kuiona bendera ya CHADEMA nyumbani kwake na hao marafiki zake, wakati alikuwa ameweka bandera ya chadema juu ya kabati chumbani kwake sebuleni wala sio nje ya nyumba. Walikuwa wanaongea kama utani utani kumbe mzee wa watu anaumia rohoni kutokana na mwenendo wa CHADEMA. Baba yangu mdogo aliondoka akamwachia miezi miwili juu kwa karaa na vituko alivyokuwa anavipata. Hawa CCM wanaroho mbaya sana wanajiona ni wafalme wa kupigiwa magoti. Hawa sio watu wa kubadilika kutokana na kasumba yao mbaya ya umimi. Kama kikwete angekuwa mpenda mapinduzi angefurahi kwa changamoto ya CHADEMA ya kuwaelimisha wananchi, na yeye angetumia fursa hiyo kutumia rungu lake kuwawajibisha hao vilaza wanaowadanganya wananchi kura zao na kwenda kujificha huko upanga wakati wananchi wanateseka.
 
Mimi ni mwanachama wa C.C.M, na kiongozi ndani ya Chama katika ngazi ya Wilaya lakini kwa mara ya kwanza nalazimika kusema ukweli, Malalamiko ya viongozi wetu ngazi ya Taifa kuhusiana na maandamano ya CHDEMA yalenge katika ukweli, tujiulize hawa watu wanalaumu nini? na wanawaambia nini wananchi? kuna ukweli ndani yake? kama hakuna ukweli kwa yale wanayoyasema tuwashitaki haraka iwezekanavyo, nahisi kama hatuwatendei haki kusema wana dhamira ya kumwaga damu, so far sijaona kosa walilofanya na ndo maana hawajapelekwa mahakamani na wakapatikana na hatia hizo, unajua kwa haya malalamiko yetu inaonyesha hatutaki changamoto za kweli na hatupendi vyama vya upinzani viwe strong. Nadhani sisi kama chama tuwe wa kweli wananchi wamechoka na maisha duni yanayozidi kuwa makali kila kukicha nadhani umefika wakati sasa viongozi wetu kutekeleza ilani zetu kwa vitendo na tusifanye siasa katika hili, tukiri katika utawala huu mambo yamekuwa tofauti sana ukilinganisha na vipindi vilivyopita kwa mfano itakuwa ni busara sana tukitumia muda mwingi kujibu maswali yanayoulizwa kwa mifano hai ya utekelezaji wa tuliyo waahidi kuliko kulaumu tu na umefika wakati sasa tuwe na ahadi chache na zinazotekelezeka ni hatari kuahidi maisha bora kwa kila mtu ilihari hata nchi tajiri zinapata changamoto kubwa sana kufikia hiyo hatua, tunatakiwa tujipange vinginevyo watatushinda kwa hoja mbele ya wananchi.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

Peleka huko uhuni wako Chadema!
 
Mkuu jjapo uliyo sema yote yana ukweli ndani yake maneno yako yange kuwa na nguvu zaidi kama unge jitokeza wazi na kusema wewe ni fulani na pia kama maneno unayo ongea hapa unge yapeleka kwenye vikao rasmi vya CCM. Otherwise big up kwa kutambua kwamba Chadema na wananchi wana madai halali.
 
Nadhani mitazamo ya watu kama Sita, Magufuli, Mwakyembe , Mwandosya na Butiku ndio ikaribishwe TBC 1 sio wachovu kina Wasira.
 
Kuwa nabii wa kuishuhudia kauli yako kwa wanaccm wasiotumia mtandao hasa mnapokuwa kwenye vikao vya chama. wasaidie kuamka ambao bado wamelala ndani ya chama chenu.
 
Ole wako Makamba akusikie..hehehe! They never admit the truth hata kama kila kitu kiko wazi.
 
Jamani haya maandamano ya CDM na maneno yanayotolewa kwenye mikutano ni uchochezi ili wananchi waichukie Serikali. Uchaguzi umefanyika miezi mitatu tu iliyopita. Si msubiri basi kidogo muone kasi zaidi na ari zaidi itatoa matunda gani? Viongozi ndio kwanza wamechaguliwa (Mawaziri, wabunge n.k.). Si muwape muda basi muone watafanya nini? Kama kuna makosa ndani ya Chama na Serikali ni dhahiri yameshaonekana, kwani wao wajinga kuendelea na makosa hayo? Naamini wako katika harakati za kuyarekebisha makosa na kutafuta ufumbuzi wa kuleta mabadiliko na maendeleo kwa wananchi na kuondoa kero. Hii mikutano sioni kama inalenga kuleta maendeleo, ni kuleta uvunjaji wa amani tu. Mimi sio mwanasiasa na siko upande wowote, lakini naipenda nchi yangu na napenda Amani. Tusimuandame Rais wetu na Serikali yetu kwa mambo ambayo yako katika mchakato wa kutekelezwa. Mabomu, umeme, ukali wa maisha n.k. vinatakiwa kutafutiwa ufumbuzi, sio kuandamana na kutoa lawama tu.
Ni wale wale tu toka 2005, tangu mabomu ya Gongo la mboto, kisha Mbagala tena Gongo la Mboto...ndiyo wale wale tuwape muda mpaka 2055 labda,
 
Jamani haya maandamano ya CDM na maneno yanayotolewa kwenye mikutano ni uchochezi ili wananchi waichukie Serikali. Uchaguzi umefanyika miezi mitatu tu iliyopita. Si msubiri basi kidogo muone kasi zaidi na ari zaidi itatoa matunda gani? Viongozi ndio kwanza wamechaguliwa (Mawaziri, wabunge n.k.). Si muwape muda basi muone watafanya nini? Kama kuna makosa ndani ya Chama na Serikali ni dhahiri yameshaonekana, kwani wao wajinga kuendelea na makosa hayo? Naamini wako katika harakati za kuyarekebisha makosa na kutafuta ufumbuzi wa kuleta mabadiliko na maendeleo kwa wananchi na kuondoa kero. Hii mikutano sioni kama inalenga kuleta maendeleo, ni kuleta uvunjaji wa amani tu. Mimi sio mwanasiasa na siko upande wowote, lakini naipenda nchi yangu na napenda Amani. Tusimuandame Rais wetu na Serikali yetu kwa mambo ambayo yako katika mchakato wa kutekelezwa. Mabomu, umeme, ukali wa maisha n.k. vinatakiwa kutafutiwa ufumbuzi, sio kuandamana na kutoa lawama tu.
Akili mgando!
 
Mimi ni mwanachama wa C.C.M, na kiongozi ndani ya Chama katika ngazi ya Wilaya lakini kwa mara ya kwanza nalazimika kusema ukweli, Malalamiko ya viongozi wetu ngazi ya Taifa kuhusiana na maandamano ya CHDEMA yalenge katika ukweli, tujiulize hawa watu wanalaumu nini? na wanawaambia nini wananchi? kuna ukweli ndani yake? kama hakuna ukweli kwa yale wanayoyasema tuwashitaki haraka iwezekanavyo, nahisi kama hatuwatendei haki kusema wana dhamira ya kumwaga damu, so far sijaona kosa walilofanya na ndo maana hawajapelekwa mahakamani na wakapatikana na hatia hizo, unajua kwa haya malalamiko yetu inaonyesha hatutaki changamoto za kweli na hatupendi vyama vya upinzani viwe strong. Nadhani sisi kama chama tuwe wa kweli wananchi wamechoka na maisha duni yanayozidi kuwa makali kila kukicha nadhani umefika wakati sasa viongozi wetu kutekeleza ilani zetu kwa vitendo na tusifanye siasa katika hili, tukiri katika utawala huu mambo yamekuwa tofauti sana ukilinganisha na vipindi vilivyopita kwa mfano itakuwa ni busara sana tukitumia muda mwingi kujibu maswali yanayoulizwa kwa mifano hai ya utekelezaji wa tuliyo waahidi kuliko kulaumu tu na umefika wakati sasa tuwe na ahadi chache na zinazotekelezeka ni hatari kuahidi maisha bora kwa kila mtu ilihari hata nchi tajiri zinapata changamoto kubwa sana kufikia hiyo hatua, tunatakiwa tujipange vinginevyo watatushinda kwa hoja mbele ya wananchi.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

This is too good to be true!!!

Jamani haya maandamano ya CDM na maneno yanayotolewa kwenye mikutano ni uchochezi ili wananchi waichukie Serikali. Uchaguzi umefanyika miezi mitatu tu iliyopita. Si msubiri basi kidogo muone kasi zaidi na ari zaidi itatoa matunda gani? Viongozi ndio kwanza wamechaguliwa (Mawaziri, wabunge n.k.). Si muwape muda basi muone watafanya nini? Kama kuna makosa ndani ya Chama na Serikali ni dhahiri yameshaonekana, kwani wao wajinga kuendelea na makosa hayo? Naamini wako katika harakati za kuyarekebisha makosa na kutafuta ufumbuzi wa kuleta mabadiliko na maendeleo kwa wananchi na kuondoa kero. Hii mikutano sioni kama inalenga kuleta maendeleo, ni kuleta uvunjaji wa amani tu. Mimi sio mwanasiasa na siko upande wowote, lakini naipenda nchi yangu na napenda Amani. Tusimuandame Rais wetu na Serikali yetu kwa mambo ambayo yako katika mchakato wa kutekelezwa. Mabomu, umeme, ukali wa maisha n.k. vinatakiwa kutafutiwa ufumbuzi, sio kuandamana na kutoa lawama tu.

Mkubwa Mawaziri karibu wote waliochaguliwa safari hii walikuwepo katika Serikali iliyopita!!! Hawakufanya chochote substantial na nalazimika kuamini hawatafanya chochote substantial hata sasa!!! Hata wakipewa miaka 100!!! Hawatafanya lolote jipya hao MAFISADI!!! Wamelewa madaraka na dawa yao ni kuwang'oa tu!!!
 
Inawezekana ukajinadi kuwa huwezi kuwa mnafiki. Hata kusema bila kutaja jina nao ni unafiki. Kwa nini unaogopa kujulikana kama unafikiri unachosema ni ukweli. Pili, kama kweli ndani ya moyo wako unaamini sisiemu imeshindwa kutekeleza mahitaji ya wananchi, kwani unasema huwezi kutoka? Inawezekana kwa kuwa wewe unapata maisha. Huu nao ni unafiki. kwani unawasaliti watu walio wengi ambao maisha yao ni magumu. Ukweli ni kwamba, tulio wengi tunaoweza chart hata kwa internet kama hivi ni wale maisha yetu yanaahueni. Lakini tunapiga kelele kwa sababu wa wengine walio wengi wanakosa hata mlo. Hivyo, no vizuri tuwe wakweli.
 
Jamani haya maandamano ya CDM na maneno yanayotolewa kwenye mikutano ni uchochezi ili wananchi waichukie Serikali. Uchaguzi umefanyika miezi mitatu tu iliyopita. Si msubiri basi kidogo muone kasi zaidi na ari zaidi itatoa matunda gani? Viongozi ndio kwanza wamechaguliwa (Mawaziri, wabunge n.k.). Si muwape muda basi muone watafanya nini? Kama kuna makosa ndani ya Chama na Serikali ni dhahiri yameshaonekana, kwani wao wajinga kuendelea na makosa hayo? Naamini wako katika harakati za kuyarekebisha makosa na kutafuta ufumbuzi wa kuleta mabadiliko na maendeleo kwa wananchi na kuondoa kero. Hii mikutano sioni kama inalenga kuleta maendeleo, ni kuleta uvunjaji wa amani tu. Mimi sio mwanasiasa na siko upande wowote, lakini naipenda nchi yangu na napenda Amani. Tusimuandame Rais wetu na Serikali yetu kwa mambo ambayo yako katika mchakato wa kutekelezwa. Mabomu, umeme, ukali wa maisha n.k. vinatakiwa kutafutiwa ufumbuzi, sio kuandamana na kutoa lawama tu.

Ni kweli umeongea ila ilimradi umeongea mana naona dhahiri uwezo wako wa kufikiri ni mdogo naomba kajipange upya uje na hoja yenye MASHIKO
 
Jamani haya maandamano ya CDM na maneno yanayotolewa kwenye mikutano ni uchochezi ili wananchi waichukie Serikali. Uchaguzi umefanyika miezi mitatu tu iliyopita. Si msubiri basi kidogo muone kasi zaidi na ari zaidi itatoa matunda gani? Viongozi ndio kwanza wamechaguliwa (Mawaziri, wabunge n.k.). Si muwape muda basi muone watafanya nini? Kama kuna makosa ndani ya Chama na Serikali ni dhahiri yameshaonekana, kwani wao wajinga kuendelea na makosa hayo? Naamini wako katika harakati za kuyarekebisha makosa na kutafuta ufumbuzi wa kuleta mabadiliko na maendeleo kwa wananchi na kuondoa kero. Hii mikutano sioni kama inalenga kuleta maendeleo, ni kuleta uvunjaji wa amani tu. Mimi sio mwanasiasa na siko upande wowote, lakini naipenda nchi yangu na napenda Amani. Tusimuandame Rais wetu na Serikali yetu kwa mambo ambayo yako katika mchakato wa kutekelezwa. Mabomu, umeme, ukali wa maisha n.k. vinatakiwa kutafutiwa ufumbuzi, sio kuandamana na kutoa lawama tu.

Kweli kabisa ndugu yangu mauaji ya Arusha na Mbeya, milipuko ya mabomu na makombora Gongo la Mboto na mauaji yake, mgawo wa umeme usiokwisha, kupanda kwa bei ya bidhaa ndio kasi zaidi, ari zaidi, na nguvu zaidi! Sina la kusema ila nadhani wataalamu wa elimuakili wanaweza kukusaidia kuona mwisho wa mtiririko wa mawazo yako.
 
Back
Top Bottom