Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,756
Alisimamia na kuamini kuwa Chadema haingeshinda Arumeru na kwamba Sioi ndiye angeapishwa kama mbunge, sasa hapa alisukumwa na nini kama si itikadi? Je na hapo tulishindwa kumwelewa?Mimi nadhani huwa mnashindwa tu kumwelewa Pasco,huwa anasimamia anachokiamini bila kujali itikadi za chama.
Tukirudi kwenye mada naomba mkumbuke kuwa kesi iliwahi kufunguliwa dhidi ya CCM na mali inazozimiliki isivyo halali na wakili wa kujitegemea Marehemu Mujuna Balozi lakini kama kawaida majaji wetu katika kuisetiri CCM waliitupilia mbali. Kwa sasa hapa Tanzania hatuna jaji mwenye ujasiri wa kutoa hukumu ya haki dhidi ya CCM. Lakini mwaka 2015, CCM isubiri tu kufilisiwa na viongozi wake kuishia Keko kwa wizi, udanganyifu, ufisadi na mauaji ya Watanzania wasio na hatia.