"Bye Daddy"...... Dah!!!

Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
68,012
95,358
Wajameni salaam kwa mpigo.

Ukubwa dawa wajameni......

Hii biashara ya mabinti na baba zao kuwa "washkaji" sijui imetokea wapi. Jana nlikapeleka kabinti kangu kapendwa shule kuanza maisha rasmi ya boarding. Shule imekomaa mabinti lazima wahamie hostel kwa ajili ya maandalizi ya "kufa mtu" ya mitihani ya kitaifa mwaka huu. Ikawa haina jinsi.....Sikuwahi kuwaza kabinti kangu kataenda boarding katika elimu ya msingi asee.....

Tumekapeleka haka kabinti nikiwa na mama yake.... wakati ndo tunamkabidhi kwa "wazazi wake wapya" kabinti kakatoka mbio na kunirukia na kuniambia "Bye daddy"... kisha hakooo kakatokomea..... Cha kustaajabisha, mamake alipewa bye ya mbaaaali lol

Hii "bye daddy" bado haijatoka masikioni asee.... kwamba ntarudi home leo bila kulakiwa na kamatesha kangu... damn!.... Na haya maisha ya mimi na mama Matesha wangu kubaki peke yetu nyumba nzima, si honeymoon nyingine hii wajameni? Atanikomaje?

Baada ya kusema hayo naomba msaada...... Eti kuna kitu gani kinawafanya mabinti "wazimike" namna hii kwa baba zao? Ni kwanini mababa wengi nao pia wanakuwa kama "wamelogwa" na mabinti zao? (Hapa ODM nakiri, vibinti vyangu navizimikia kinoma asee... tena haka kamatesha ndo usiseme.....)

Bye Daddy... dah!
 
ODM, mimi na baba yangu tu marafiki sana. na mara nyingi mama akiniletea rabsha baba anani-deffend mbaya, lazima siku hiyo kitanuka. Bye Daddy, nakumbuka nilisema hayo wakati kwa mara ya kwanza natengana na wazazi wangu kwenda boarding school. Loh
 
Aisee! Am learning!

Anakupenda kwasababu unampenda.

Watoto wa kiume hua walaini kwa mama zao, na wa kike kwa baba zao. Ni ile attention ya 'different sex'. . .
Word!

Hapo kwa red..... different sex ina-impact mpaka kwa watoto kumbe lol
 
Kwa ufupi tafuta wimbo wa Lucky Dube unaitwa "Good Girl" utaona machungu ya baba bintie au mwanae,au tafuta unaoitwa "the one" wa huyohuyo Lucky dube unaweza kulia!
 
I see some bragging hapa ikichukua mkondo.....lol.... Message itafika kwa mama Matesha.

Katika Ulezi mara nyingi akina mama tupo strict saana kwa watoto hasa wa kike. Baba nae anaweza kua strict lakini sio kwa level za mama. Mimi kama mama - na hasa tokana na makuzi kua mtoto wa kike lazima a master kila kitu nyumbani.... Inakufanya utake the same for your kid. Utahakikisha wakapangia responsibilities tokana na level ya Ukubwa wake, toka kupika chai hadi kupika ugali, toka kusuza kikombe hadi kuosha vyombo, toka kufuta maji yalo mwagika to the level ya kupiga deki. Mara nyingi (for hata mimi ilikua hvio) unaona kama mama ni mnoko fulani, hakupendi, anapenda tu kukutumikisha na the like....

Baba yeye akiwa na mtoto wa kike anchowaza cha kwanza ni jinsi gani amtimizie binti yake asifanyiwe na ma bazazi yale yeye baba afanyavyo kwa watoto wa wenzie, ama dada wa wenzie na wanawake woote. Wanaume wengi wanaamini kua toka utoto akidhibiti penzi la mtoto wake wa kike na kumtimizia kila kitu mwanae walau ataepuka kikombe cha kurubuniwa huko mtaaani (Yes it helps to some extent) but ukweli unabaki pale pale no matter how she Loves you... She will eventually fall in love.... Kwa muktadha huo yeye binti huona kua baba is the best parent, lolote atakalo apewa, anadekezwa na baba anamjali na kumuulizia kila saa.... Tena sa ingine hata hua amwambia mama kua ampunguzie kazi.....

Na nature tu, wa kiume kwa mama wa kike kwa baba.... Mtoto wangu wa kiume.... ni mdogo, ana wivu huyo hataki kabisa mtu mwingine apate attention yangu hasa kama ni opposite sex.... anakua mkali kabisa na tu amri twa hapa na pale....
 
Aisee....:A S embarassed:
 
Una bond kali na bintiyo...hata hivyo kama Lizzy alivyosema watoto wa kike na baba zao halafu boys na mamiiz..

Bye daddy..!
 
Aisee! Am learning!

Word!

Hapo kwa red..... different sex ina-impact mpaka kwa watoto kumbe lol
Mama hua anaonekana mkali/mnoko kwa mtoto wa kike na baba kwa mtoto wa kiume. Ndio maana ni rahisi sana wa kiume kumkimbilia mama ikiwa atahisi baba anamuonea kuliko kumkimbilia baba hata kama mama atafanya kitu kile kile alichofanya baba. . hivyo hivyo kwa watoto wa kike. Yani wanaangalia past "malengo/matendo" na kuangukia kwenye utofauti wa jinsia kati yao na mzazi.
 
I see some bragging hapa ikichukua mkondo.....lol.... Message itafika kwa mama Matesha.

Katika Ulezi mara nyingi akina mama tupo strict saana kwa watoto hasa wa kike. Baba nae anaweza kua strict lakini sio kwa level za mama. Mimi kama mama - na hasa tokana na makuzi kua mtoto wa kike lazima a master kila kitu nyumbani.... Inakufanya utake the same for your kid. Utahakikisha wakapangia responsibilities tokana na level ya Ukubwa wake, toka kupika chai hadi kupika ugali, toka kusuza kikombe hadi kuosha vyombo, toka kufuta maji yalo mwagika to the level ya kupiga deki. Mara nyingi (for hata mimi ilikua hvio) unaona kama mama ni mnoko fulani, hakupendi, anapenda tu kukutumikisha na the like....

Baba yeye akiwa na mtoto wa kike anchowaza cha kwanza ni jinsi gani amtimizie binti yake asifanyiwe na ma bazazi yale yeye baba afanyavyo kwa watoto wa wenzie, ama dada wa wenzie na wanawake woote. Wanaume wengi wanaamini kua toka utoto akidhibiti penzi la mtoto wake wa kike na kumtimizia kila kitu mwanae walau ataepuka kikombe cha kurubuniwa huko mtaaani (Yes it helps to some extent) but ukweli unabaki pale pale no matter how she Loves you... She will eventually fall in love.... Kwa muktadha huo yeye binti huona kua baba is the best parent, lolote atakalo apewa, anadekezwa na baba anamjali na kumuulizia kila saa.... Tena sa ingine hata hua amwambia mama kua ampunguzie kazi.....

Na nature tu, wa kiume kwa mama wa kike kwa baba.... Mtoto wangu wa kiume.... ni mdogo, ana wivu huyo hataki kabisa mtu mwingine apate attention yangu hasa kama ni opposite sex.... anakua mkali kabisa na tu amri twa hapa na pale....
Shem umenisisimuaje? manake dah!

Nakumbuka kipindi mama yao aliposafiri, nlikuwa nikitoka job nawahi kumchuka tunaenda sehemu tunapata menyu.... chipsi kuku/mayai zilimkomaje? Basi ikawa kila siku anauliza mama atarudi lini, nikifikiri amemmisi ile mbaya...... ilipofika wakati sasa kuwa mama anarudi kesho nikasikia :"Ayaaa, si akaekae tena kidogo?" lol
 
kiukweli nampenda sana mdingi wangu aisee.uspime i thinki nae ananilove sana yaani daily lazima anicall.yaani anamshinda hata mpenzi
umenikumbusha naenda holiday wk ijayo tar 14 feb lazima nile na mdingi wangu
he is my happyness
 
Shem umenisisimuaje? manake dah!

Nakumbuka kipindi mama yao aliposafiri, nlikuwa nikitoka job nawahi kumchuka tunaenda sehemu tunapata menyu.... chipsi kuku/mayai zilimkomaje? Basi ikawa kila siku anauliza mama atarudi lini, nikifikiri amemmisi ile mbaya...... ilipofika wakati sasa kuwa mama anarudi kesho nikasikia :"Ayaaa, si akaekae tena kidogo?" lol
lolz..... ..!
bye dady!
no comment naona zote zimezugumzwa hapo juu babu.
 
Shem umenisisimuaje? manake dah!

Nakumbuka kipindi mama yao aliposafiri, nlikuwa nikitoka job nawahi kumchuka tunaenda sehemu tunapata menyu.... chipsi kuku/mayai zilimkomaje? Basi ikawa kila siku anauliza mama atarudi lini, nikifikiri amemmisi ile mbaya...... ilipofika wakati sasa kuwa mama anarudi kesho nikasikia :"Ayaaa, si akaekae tena kidogo?" lol

Unaona tofauti sasa? Akina mama sometimes tuna tabia mbaya... Mzee akiwepo home chakula kizuri kila siku for hutaki mumeo ale chakula cha ovyo ovyo.... Ukiondoka ukasafiri inaanza budget ya hali ya juu... watoto wanaambiwa chemshen viazi tumchemshe na chai...lol.... Yaani maporomoko ya chakula ile mbaya! Wakati baba atampeleka sehemu ya kula na hataki aagize chakula cha ovyo ovyo... anatakwa what is best for the kid....
 
Hapa sasa mzee...........yani kwamba yani, mama matesha yani kwamba dah!!!

sasa inamaana yani unataka kukomoa ili ukichelewa kwenye Feawei asikupigie.....yani kwamba......

asee.......bye daddy!!!
 
Bye Daddy
Huu udhungu bwana! Mimi nimewafundisha kuaga kwa kikwetu na siyo hayo maneno ya kidhungu!
 
Hapa sasa mzee...........yani kwamba yani, mama matesha yani kwamba dah!!!

sasa inamaana yani unataka kukomoa ili ukichelewa kwenye Feawei asikupigie.....yani kwamba......

asee.......bye daddy!!!

Biggie hapa tatizo ndugu yako huyu anapenda saana majigambo.... Ukute Mama Matesha nae ana furaha zoote (kama kweli ODM huwajibisha ipasavo) na hivi hapa yupo kufanya maandalizi kua nyumbani mazingira yawe ya ki hani mun-hani mun.....lol
 
Back
Top Bottom