Bwawa la ajabu tunduru

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Wakati nikiwa Tunduru nilipata simulizi mbalimbali kuhusiana na wilaya hiyo jinsi ilivyo tajiri wa ardhi yenye rutuba ya kutosha pamoja na maji mengi ya kutosha kulinganisha na wilaya nyingine zilizopo mikoa ya Kusini.

Lakini kilichonisisimua zaidi ni simulizi juu ya hili bwawa ambalo hata kuletwa na kufika hapa na mwenyeji wetu ilikuwa shughuli kidogo na ilitulazimu tuwaombe wenyewe ili tufike na kurudi salama. Unaweza kulidharau kwa macho ukilitazama lakini amini usiamini ninachokueleza ndicho nilichoshuhdiwa na wenyeji. Bwawa hili lina nguvu za ajabu ambapo kama utakuwa umekwenda kwa shughuli zako na kuhatarisha matumizi yake ikiwa ni kukojoa, kutukana matusi na mambo mengine ambayo ni chukizo, hakika unapoteza maisha. Na inasemekana kila baada ya kipindi fulani mtu hupoteza maisha kwa kufia humo bwawani.

Bwawa hili lililopo Kiuma wilaya ya Tunduru linasemekana linatoa maji safi ya kunywa pamoja na matumizi mengine ikiwamo ufyatuaji wa tofali za udongo kwa wenyeji. Mwaka jana wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kiuma iliyopo karibu na bwawa hilo walikwenda kuoga pamoja na kufua nguo lakini mmoja wao hakurudi salama.

Ilikuwaje? Inaelezwa kwamba mara baada ya kijana huyo kumaliza shughuli zake alikaa pembeni ya bwawa akiwasubiri wenzake. Lakini kadiri jua lilivyozidi kuongezeka alihisi joto na kuonelea ni busara akaingia bwawani ili apooze joto la mwili wake. Wakati akiwa bwawani, kijana huyo alitamka lugha ya matusi na maneno mabaya kuhusu maji ya bwawa hilo ghafla akahisi nguvu kali ikimvuta kuelekea chini. Akaomba msaada kwa wenzake ambao walijaribu kutaka kumwokoa wakaona nawao wanazidiwa nguvu kwa kuvutwa ikashidnikana na mwenzao akatokomea majini.

Baada ya mwenzao kutokomea majini, vijana wale walikwenda kutoa taarifa shuleni kwao kwamba mwenzao amepotea katika maji bwawani na wamejaribu kumwokoa wakashindwa. Wakuu na wahusika wengine wakaanza taratibu za uokoaji ili kusalimisha maisha ya kijana huyo ikiwa na Mkuu wa kituo cha Kiuma kuagiza ndege binafsi yenye wataalam wa uokoaji kutoka Dar es salaam kuja mara moja kumwopoa kijana huyo jitihada ambazo zilishindikana pamoja na waokoaji wengine. Ndipo ikalazimu kwenda kwa wazee wa jadi ambao walifanya tambiko na kuomba kwa muda wa siku 3 na mara baada ya hapo kazi ya kumwopoa ikaanza. Inaelezwa kwamba kijana huyo alipatikana lakini nguvu ya ziada ilitumika kwani mbali na kupatikana kwake lakini bado walinyang'anyana wakiwa majini. Alipoopolewa kijana huyo alikuwa tayari amekwishafariki cha ajabu kilichoonekana ni kutokwa na damu puani kwa kijana huyo hali alikuwa majini kwa siku 3. Tukio hilo lilileta simanzi kubwa katika jamii nzima ya Kiuma na uongozi wa Kiuma ulichukua hatua ya kuwapiga marufuku wanafunzi wake kufika katika eneo hilo.

Walioingia kumwokoa kijana huyo walieleza kwamba walikutana na vitu ambavyo ni adimu kuonekana katika hali ya kawaida katika maisha ya binadamu. Ikiwa na sehemu ambazo hakuna maji kabisa na kuwa kukavu kama nchi kavu huku upande mwingine maji yakiwa yamezunguka pamoja na matukio mengine ya ajabu ambayo ni ngumu kumuelezea mtu akaamini.

Inaelezwa kwamba kuna bwana mmoja mvuvi alikwenda kutafuta kitoweo bwawani hapo alipotwika ndoano na kuvuta akavuta lundo la samaki wakavu waliochomekwa katika umambo mmoja jamaa akatimua mbio na ikawa mwanzo na mwisho wa kukanyaga hapo. Matukio mengine ni kama kukuta nguo zimeanikwa na wahusika hawaonekani ama kusikia sauti za watu zikiongea na usiwaone.

Hayo ndiyo maajabu ya Tunduru Tembea Uone usingoje kuambiwa. Asiyeamini afuatilie na kujua kuhusiana na matukio niliyoyaeleza hapo kuhusu bwawa hilo la KIUMA.
65232_163524193660791_100000096333724_516473_7947681_n.jpg
 
kumbe halina maslahi kwa taifa, mimi nilijua lina sifa nzuri tuanze kulitangaza kiutalii, kumbe linaua watua , i mean llimejaa wachawi
 
Wakati nikiwa Tunduru nilipata simulizi mbalimbali kuhusiana na wilaya hiyo jinsi ilivyo tajiri wa ardhi yenye rutuba ya kutosha pamoja na maji mengi ya kutosha kulinganisha na wilaya nyingine zilizopo mikoa ya Kusini.

....

Inaelezwa kwamba kuna bwana mmoja mvuvi alikwenda kutafuta kitoweo bwawani hapo alipotwika ndoano na kuvuta akavuta lundo la samaki wakavu waliochomekwa katika umambo mmoja jamaa akatimua mbio na ikawa mwanzo na mwisho wa kukanyaga hapo. Matukio mengine ni kama kukuta nguo zimeanikwa na wahusika hawaonekani ama kusikia sauti za watu zikiongea na usiwaone.

Hayo ndiyo maajabu ya Tunduru Tembea Uone usingoje kuambiwa. Asiyeamini afuatilie na kujua kuhusiana na matukio niliyoyaeleza hapo kuhusu bwawa hilo la KIUMA.
Hayo uliyo yaandika umesimuliwa, ukushuhudia, kwa hiyo hakuna ukweli au uthibitisho wa hizo simulizi...! Just a myth!
 
Back
Top Bottom