Bwana Mukama. "mtu mzima akichoka akili, hubwatuka"

Royals

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
1,466
378
Maneno gani yale uliokiwa unayatoa katika ufunguzi wa kampeni pale Usa river? Ulitutia aibu wanachama wenzako.

Wala hukuwa unashangaa umati woote ule ulikuwa unakushangaa wewe ulikuwa unamwiga masanja wa orijino komedi.

Pale ulitakiwa kuueleza umma uzuri wa mgombea wetu bwana Siyoi na siyo kuonesha ufundi wa kutupa madongo majirani zetu wa Chadema. Wao wakitupiga madongo ni sawasawa yao maana wao hutafuta hasira yetu ilipo ili kwa kutumia nguvu ya hasira tuwe kama wao kisha tuonekane kwa jamii kuwa sisi ni sawa na wao. Ulikosea. Muangalie alivo na busara kubwa mwenyekiti wetu wa chama. Yeye hatupiwi dongo kisha naye akalibeba kwa mikona yake na kulirudisha lilikotoka. Muige huyu.

Kwa mfano uliposema " mtu kama upadri umekushinda ubunge utauweza wapi?". Hapa ni mwehu pekee ndiye ambaye hajui kuwa ulikuwa unamsema mzee wa Chadema.

Au umesahau kuwa alikuwa anaumiza sana vichwa vyetu alipokuwa mbunge wa Karatu?
mtu mzima akichoka akili hubwatuka.
 
Kuna clip ya ccm nikuwa naiangalia. Nilipoona Mukama anaanza kuongea niliipeleka mbele haraka. Jamaa namchukia kutoka ndani
 
Maneno gani yale uliokiwa unayatoa katika ufunguzi wa kampeni pale Usa river? Ulitutia aibu wanachama wenzako.
Wala hukuwa unashangaa umati woote ule ulikuwa unakushangaa wewe ulikuwa unamwiga masanja wa orijino komedi.
Pale ulitakiwa kuueleza umma uzuri wa mgombea wetu bwana Siyoi na siyo kuonesha ufundi wa kutupa madongo majirani zetu wa Chadema. Wao wakitupiga madongo ni sawasawa yao maana wao hutafuta hasira yetu ilipo ili kwa kutumia nguvu ya hasira tuwe kama wao kisha tuonekane kwa jamii kuwa sisi ni sawa na wao. Ulikosea. Muangalie alivo na busara kubwa mwenyekiti wetu wa chama. Yeye hatupiwi dongo kisha naye akalibeba kwa mikona yake na kulirudisha lilikotoka. Muige huyu.
Kwa mfano uliposema " mtu kama upadri umekushinda ubunge utauweza wapi?". Hapa ni mwehu pekee ndiye ambaye hajui kuwa ulikuwa unamsema mwenyekiti wa Chadema. Au umesahau kuwa alikuwa anaumiza sana vichwa vyetu alipokuwa mbunge wa Karatu?
mtu mzima akichoka akili hubwatuka.

kumbe mwenyekiti wa chadema ni slaa!kweli ukiwa mzee wapitwa na mengi.
Yaonekana na wewe umechoka kiakili na umeamua kubwabwaja

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
kwa mtu yeyote akitaka kujiunga na ccm lazima ukate baadhi ya fyuzi za faham ndio uende sambamba nao!!

dah una akili sana wewe chalii yangu!!,ndo maana nakupendaga sana!!.Ngoja nibofye kitufe cha like!.Thanks exellent!
 
Unajua wa tz tunabakwa na CCM mpaka tumezoea! Maana tunalalamika sanaaaaa lakini bado tunawachagua!!!
 
Mukama anarudia kosa lile lile la Mkapa. Dr. Slaa hagombei nafasi Arumeru, hayuko kwenye team ya campaign huko Arumeru, sasa kwa nini awe topic? Mukama ameenda Arumeru kumuongelea Dr Slaa? Ili iweje?

CCM wanajua fika hakuna hata mmoja kati yao aliye msafi, sijui kwa nini wameamua kurusha mawe wangali wakiwa bado kwenye nyumba zao za glass?
 
mashabiki wote wa ccm hawana akili timamu kama wametolewa kafara vile,kuanzia wewe uliepost hii clip,akina masanja,na wale wanaovaa kanga na tshirt za kijani na kucheza mbele ya mwigulu wote mnafanana tofauti yenu ni jinsia na maumbo tu ila kiakili mpo sawa wote hamjitambui mmewekwa kwenye chupa
 
Ina maana na mimi niko hivyo? Kamuulize mwalimu wa mwalimu wako kama mimi niko hivo.
 
kila wakati kuweweseka na Dr (wa kweli) W. Slaa. Yeye hakuwa kwenye mkutano ule lakini mara upadri...... Mwulizeni Jk ndiye anayejua makali ya Dr. Mukama siasa za uzeeni hizo: umekumbuka shuka kukiwa kumepambazuka. Nenda kapumzike kijijini.
 
Mimi nataka kujua Mkapa aliposema kuwa "CHADEMA walirusha matangazo live kwenye TV na kuweka kwenye matandao wao wa internet" alimaanisha huo mtandao wa internet ni JF au kuna mtandao mwengine wa CHADEMA?
Maana nakumbuka kwenye ufunguzi wa campaign za CHADEMA, walitangaza kuwa star TV na JF walikua wanarusha live.
 
Mkapa yaani na kuchoka akili vile ndo ccm walimuona anafaa kuzindua kampeni!!! je wengine ingekuwaje,Mkapa laana za watanzagiza zimeanza kumu-affect,.Kama ningekuwa na uwezo ccm wote ningewapeleka Gwantanamo gerazani
 
CCM wanakata tawi la mti wakiwa wamelikalia.Mukama! "Mtoto wa mwenzio mbebe kalala akiwa macho atakuuliza mama yuko wapi"Watanzania wameshaamka.
 
Tatizo kubwa linalowapata na kuwapa shida ccm na kuwafanya kuisema vibaya chadema ni kuwa utatoa sera gani Arumeru mashariki ambazo ni mpya wakuelewe, tatizo ni maji, ardhi, elimu na kazi kwa vijana kukosa ajira, sasa ubunge ulikuwa wao kwa miaka mingi, leo unapata wapi ujasiri wa kuwaambia kuwa utaleta hivyo vitu na nini kilikufanya usilete kabla? Dawa ni kuwasema vibaya chadema ili muda uishe wa kampeni halafu wafanye wanavyofanyaga kisha maisha yanasonga. Kiukweli hawana hoja ccm.
 
Sina hamu na ccm magamba. Infact ni kama vichaa fulani hivi mabo yao ya kampeni za vijembe. Staili za mwaka 77 bado wanaendeleza hata baada ya analogue kuexpire . Sasa ivi tunaingia the digital age . Muangalie mabo mnayofanya yatawasumbua sana
 
Back
Top Bottom