Bwana harusi aingizwa ukumbini kwa bakora........ ...

Shomari

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,112
241


Bwana harusi mmoja mkazi wa Makete mkoani Iringa jina na picha za harusi yake zimehifadhiwa ametoa mpya ya mwaka baada ya kugoma kata kata kuingia ukumbini kwa madai kuwa bibiharusi si chaguo lake na kuwa hajazoea kutazamwa na watu wengi kiasi hicho.


Bwana harusi huyo ambaye ni mmoja kati ya wafanyabiashara katika mikoa ya kusini mwa Tanzania alitoa kali hiyo baada ya MC wa sherehe hiyo kuwaingiza ndani ya ukumbi wasimamizi wa harusi na wacheza show na kuingia zamu ya maharusi kuingia ambapo bwana harusi aligoma kata kata kuingia ukumbini na kupelekea baadhi ya mabaunsa ambao walikuwa katika kamati ya harusi hiyo kuingilia kati na kuta kumpa kichapo bwana harusi hiyo kwa kutaka kuivuruga sherehe hiyo.

Hata hivyo muda wote bibi harusi na ndugu wa maharusi hao ambao walikuwa wameingia ukumbini muda wote machozi yalikuwa yakiwatoka kutokana na hatua ya bwana harusi kugoma kuingia ukumbini .

Kutokana na vuta nikuvute kati ya MC ,mabaunsa na bwana harusi huyo ambaye alikuwa amelewa pombe kupita kiasi kumalizika kwa sharti la bwana harusi kutaka taa zote zizimwe ndipo aingie ukumbini ,harusi hiyo iliendelea kama kawa japo bwana harusi hakuacha kutoa vituko pindi alipotakiwa kufanya jambo.

source: Francis Godwin blog
 
hiii habari ya kulewa siku ya harusi si nzuri. ndugu yangu mmoja alitaka kumkataaa bibi harusi madhabahuni ilibidi best man afanye kazi ya ziada. hasa kwa hawa wanaoshinikizwa na wazazi muoe furani kwa sababu umezaa naye kumbe jamaa hajapenda toka moyoni. alivyopata maji ya uzima (pombe) akili ikafunguka kuwa kalazimishwa na akataka kukataa " chonde chonde ulevi ni noumer"
 
Nimekumbuka kuna bwana harusi mtarajiwa alienda kwenye sendoff ya bibi harusi wake mtarajiwa bahati mbaya mabaunsa hawakuwa wakimtambua na kadi hakuwa nayo. Alipoulizwa kadi akajitambulisha, kwakuwa mabaunsa na yeye wote walikuwa walevi, hawakuelewana! Jamaa akaamua kususia shughuli! Ilikuwa kazi kubwa kumaliza ule ugomvi.
 
Duuu! Imenikuna hii bwana harusi alichaguliwa mke,af kaona bora alewe,hahahahahaaaa,sasa kanisani si alishasema ndioooooooooooooooo kama mjengoni sa ukumbini ilikuwaje tena akagoma.teheteheteheee aligonga chag'aa huyo,
 
Back
Top Bottom