Busu la kurumagia!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Busu hili busu gani,
Busu la kurumagia,
Uzuri wake ni nini,
Kavukavu kubusia?

Tonge kulishikilia
Mchuzi ninyimwani
Nabaki kutamania
Kama samaki pichani?

Unaponipa chakula
Nipe na mchuzi pia
Na njaa mwisho ntalala,
Na tonge naachilia!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
Busu hili busu gani,
Busu la kurumagia,
Uzuri wake ni nini,
Kavukavu kubusia?

Tonge kulishikilia
Mchuzi ninyimwani
Nabaki kutamania
Kama samaki pichani?

Unaponipa chakula
Nipe na mchuzi pia
Na njaa mwisho ntalala,
Na tonge naachilia!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
Naona mkuuu leo ni siku ya mistari kwa kwenda mbele!!
 
Busu hili busu gani,
Busu la kurumagia,
Uzuri wake ni nini,
Kavukavu kubusia?

Tonge kulishikilia
Mchuzi ninyimwani
Nabaki kutamania
Kama samaki pichani?

Unaponipa chakula
Nipe na mchuzi pia
Na njaa mwisho ntalala,
Na tonge naachilia!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
Kubusiwa ni hiari
Kama huipendi shari
Waweza hata subiri
Ubusiwe kisha lumangie

Shavu litatetemeka
Busu likiisha anguka
Shavuni kutomeguka
Uzuri wake ni raha

Raha ni wake uzuri
Usingoje kwa kiburi
Lisogelee kwa hiari
Pembeni usijeenda
 
Afadhali utupe burudani tu leo.............
 
Busu hili busu gani,
Busu la kurumagia,
Uzuri wake ni nini,
Kavukavu kubusia?

Tonge kulishikilia
Mchuzi ninyimwani
Nabaki kutamania
Kama samaki pichani?

Unaponipa chakula
Nipe na mchuzi pia
Na njaa mwisho ntalala,
Na tonge naachilia!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
mkuu i hope haikuwa maana ya ''KUDUMISHA MILA'' mtaani huko ukafosi na mabusu!

huko sisi mabusu SIO INTEREST YETU!...mabusu kwa mkeo nyumbaniiii....!huko ni mila tu....:D
 
Yeah hasa baada ya stori complex za jery we needed the break!

Asenti

ahaaaaaa shingo zimezunguka kama feni jana na leo; hujakaa sawa jerry hivi, ukigeuka jerry vile , ukitaka kuchangia aaah sio hivi jerry ni vile yak!!!!!!!!!!!!!

bora mautenzi ya MM na Ndahani tuburudike sie kuelekea valentine!!!!!!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom