Bush mdogo akaamuru kahaba anyongwe……………..!

Ahsante sana ndugu,

Story yako ni nzito sana. Ina mambo mengi ambayo yanatisha, kuhuzunisha na kushangaza pia. Ina kuwa ngumu kuamini ni kwa jinsi gani mtu ambaye awali alikuwa kama mnyama anaweza kubadilika na kuwa mtu wa kuvuta hisia za wenzake. Na pia jinsi ambavyo watu wanashindwa kutoa nafasi ya kuprove kile kinachochanganya akili za wengi.

Hivi Bush angebadili huyo hukumu kitekokea nini??

Babu DC!!

Hii ndiyo tunaita miujiza !
Japo wengi walibisha wakiamini kuwa anaweza rudia tabia zake akibadilishiwa hukumu.
Na mume ya yule mama hakuwa tayari kumsamehe japo kwa ukorofi wake aliweza kumwingiza mkewe matatizoni
 
Hii ndiyo tunaita miujiza !
Japo wengi walibisha wakiamini kuwa anaweza rudia tabia zake akibadilishiwa hukumu.
Na mume ya yule mama hakuwa tayari kumsamehe japo kwa ukorofi wake aliweza kumwingiza mkewe matatizoni


Kweli Nata,

Watu wengi lazima wengabaki na wasi wasi wa namna hiyo. Ila matukio aliayoyafanya katika siku zake za mwishi yalikuwa yanagusa hisia kibinadamu na ndiyo maana inakuwa ngumu kuelewa ni jinsi gani Bush aliweza kuwa na roho ngumu kiasi kile.

Hata mie ninengemsamehe!!

Babu DC!!
 
Naona umeadimika sana
ujue tunahitaji busara zako hapa
uwe unatukumbuka.

Pole kwa msiba.


Ahsante sana Kongosho,

Unajua nini, ni vigumu kuendelea na hadithi zetu hizi za kibabu wakati wajukuu wanalia na kujigalagaza kwa uchungu...Na especially kama kinachowaliza hukielewa kwa akili yako ya 1947!!

Dawa ni kuwaacha wamalize maombolezo kwanza!!

Babu DC!!
 
Kweli Nata,

Watu wengi lazima wengabaki na wasi wasi wa namna hiyo. Ila matukio aliayoyafanya katika siku zake za mwishi yalikuwa yanagusa hisia kibinadamu na ndiyo maana inakuwa ngumu kuelewa ni jinsi gani Bush aliweza kuwa na roho ngumu kiasi kile.

Hata mie ninengemsamehe!!

Babu DC!!

Labda kwa sababu ilikuwa na public interest,
Maana pamoja na kuchukuwa muda mrefu vile siku ya kunyongwa kwake watu walizunguka gereza na mabango wakipiga kelele anyongwe!
 
Asante sana Mtambuzi yaani inasikitisha sana!

Niliona watu walivyokuwa wakimtetea jamani .

Huyu Bush angemuulumia bado wale wamabango na ndugu wa marehemu wangeweza kutomkubali kwenye jamii
na wangeweza mfanyizia chochote.

huyu Bush mdogo alikuwa na msimamo...
 
Kusimamia sheria!

Kwa hiyo hata kuivamia Iraq na Afghanistan ilikuwa ni kusimamia SHERIA...........................!?
Kiutambuzi tunaambiwa kwamba mtoto anapozaliwa anakuwa kama plain paper...........sisi kama wazazi, walezi au jamii ndio tunaoingiza elimu, tabia, hulka, na utambuzi akilini mwa watoto wetu.............mtoto anapofikisha umri fulani unaomuwezesha kuangalia mambo na kuyapima kwa mantiki ndipo anapokuwa na uwezo wa kupembua pumba na mchele, lakini hili litategemea zaidi jamii iliyomzunguka.................

Karla katika barua aliyoiandika kwa Gavana Bush alisema..............Naomba nimnukuu:

"Nikiwa na umri wa miaka 14, (mama)alinichukua na kunipeleka kwenye maeneo ambayo yalikuwa na wanaume na alinifundisha na mimi niwe binti wa kujiuza kwa wanaume hao. Nilitaka kumridhisha mama yangu, nilitaka ajivunie kuwa na mtoto mtiifu kwake kama mimi, hivyo badala ya kukataa, nilijaribu kila alichoniambia. Kitu ndani kabisa ya moyo wangu kiliniambia kwamba ninachofanya si sahihi.:

Mwisho wa kunukuu

Kisha akamalizia...............Naomba nimnukuu tena:

"Haikuwa ni kanuni ya kundi nililokuwemo, ilikuwa ni kanuni ya familia nilimozaliwa."

Mwisho wa kunukuu.

Hapo kwenye Bold Nyekundu amekiri wazi kwamba, kitu ndani ya moyo wake kilimwambia anachofanya si sahihi, na anakiri tena kwamba kuendelea na tabia hizo chafu haikuwa ni kanuni ya makundi aliyojiunga nayo, bali ilikuwa ni kanuni ya familia...........

Yaani shinikizo la yeye kujiingiza na kuendelea na vitendo vichafu, si kwamba ushawishi mkubwa ulitoka kwa makundi aliyojiingiza bali shinikizo lilikuwa linatoka ndani ya familia alimozaliwa.

Kumbukeni alizaliwa nje ya ndoa ya wazazi wake. Hamjui baba yake. Wazazi wake wakatengana kwa ajili yake. Akalelewa malezi ya upande mmoja ambapo huyo huyo mzazi akamfundisha ulevi. ukahaba na matumizi ya madawa ya kulevya.............

Huyu alikuwa hamjui Mungu, alikuwa hajui mema na mabaya, kwake kila kitu kilikuwa sawa.........

Hivi ni nani wa kulaumiwa hapa?

Kafanya mauaji. Lakini akiwa jela anapata fursa ya kumjua Mungu, fursa ambayo hakuwahi kuipata uraiani...........Anakiri makosa yake na anayajutia, kisha anatubu, lakini pia anatumia muda wake mwingi kuiasa jamii juu ya vitendo viovu, vilivyomfikisha hapo alipo.....Je ni vijana wangapi wameongoka kutokana na uzoefu wake.............Je amebadili mioyo ya waovu wangapi?

Naamini kulikuwa na haja ya kuliangalia hilo kabla ya mwanamke huyu kunyongwa..........
Mbona mfungwa mwenzie Pam Perillo, alibadilishiwa adhabu na kuhukumiwa kifungo cha maisha.........Kuuwa ni kuuwa tu iwe umeuwa kwa Sururu au kwa kutumia kamba.........lakini wote waliuwa.

Nimeangalia mkasa wa mwanamke huyu kwa jicho la tatu.
 
Big up mkuu, endelea kutulea haya matukio ya kusisimua.Bahati mbaya sijamaliza kuangalia video bundle limebakia kidogo lakini inaelekea ni nzuri sana.
 
Amen Ahsante sana kwa kuweka hii simulizi na movie yenyewe i seee ina mafundisho mazuri sana Jesus is good all the time,ubarikiwe sana the man of God
 

Similar Discussions

15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom