satellite
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 616
- 164
Bus la JM ni jipya limeanza safari zake za Mbeya dar muda si mrefu sana ila wameanza vibaya kwa kutaka uroho wa pesa,ilikua hivi nilikata tiketi siku ya j4 nikitaka kujaribu likoje(ndo mara yangu ya kwanza kulipanda)ilipofika siku ya J5 jioni wakanipigia simu kuwa bus linamatatizo haliwezi kusafiri na wametutafutia bus lingine luxury lenye gharama sawa na JM(nauli ya bus la JM ni 35,000 hadi mbeya) ambapo walisema ni SUMRY na MBEYA EXPRESS kiukweli sikupenda ila baada ya kuona ni luxury coach nikaona niepushe shari kama bus lao limearibika,kufika asubuhi stend ya ubungo nikakuta mzozo wa baadhi ya abiria wenzangu wa JM wanamwakia wakala wa bus kumbe lilikua limekodiwa na timu ya yanga na sio kuwa lilikua bovu nikagundua abiria wametugawa magari 3 mimi kwa vile nilikua naongea sana na wenzangu kama 7 hivi tukapewa SUMRY luxury,wengine sumry zile za kawaida na Pricess muro,Abiria tulikereka sana kutoheshimiwa na kupewa mabus mengine.sitakuja kulipanda tena na mjihadhari wadau mtakaofikiria kulipanda hilo gari wanathamini pesa kuliko utu.