Bus la Green Star toka Dar kwenda Mwanza Jana kidogo linilaze Porini aise.

Nzoka yihenge

Member
Jan 14, 2011
46
29
Wana JF, Jana nimepanda bus la Green Star nililoamini ndo bus lenye ubora na kiwango, sikuamini macho na masikio yangu tokea ubungo lilivyokuwa likiendelea kutoa kelele ktk diff yake na hatimaye tulipofika maeneo ya Gairo bus hilo likashindwa kuendelea na safari . nililazimika kutafuta usafiri mbadala.Natoa angalizo kwa wamiliki wa Buses kuwa wanafanyia service magari yao na sio kukusanya pesa tu.
 
Yutong zile basi za kichina, hata hivo kawaida tu inawezekana c ukosefu wa service bali technical fault inayoweza tokea popote kwa gari yoyote! Rejea gari ya mh Sugu Landcruiser iliyotaka kuwaka moto kipindi kile,,
 
hilo litakuwa bus no 2, sitasahau siku lilotulaza singida kwa matatizo hayo hayo ya diff .This guys r nt serious kabisa.
 
Hapa silalamiki mkuu, na naamini haukuzaliwa jana mpaka ushindwe kuona kuwa nataoa tahadhali kwa abiria na wamiliki kuwa makini kila mmoja kwa upande wake. Ni hayo.
 
huu ndio huwa usafiri wangu, kama nayo yameanza basi tena nitakuwa najipinda na ndege huku nikisubiri train ya umeme
 
Ndo leo tumeshangaa kuliona hapa SHY linapita mida ya saa 2 asubuhi likienda MZA.
 
hizi Yutong zina matatizo sana na diff, siku hizi wamiliki wengi wanabadilisha kwa kuweka za scania 124, tusubiri maafa, vipuri vyote yutong,diff scania

Yutong zile basi za kichina, hata hivo kawaida tu inawezekana c ukosefu wa service bali technical fault inayoweza tokea popote kwa gari yoyote! Rejea gari ya mh Sugu Landcruiser iliyotaka kuwaka moto kipindi kile,,
 
made in Chhina.Bora zile product za '' Kwa msaada wa watu wa Marekani'' zinadumu kidogo. za Kichina ni waleo wa kesho
 
Pole mkuu, mimi lilikuwa ndio basi langu wakatulaza singida kwa matatizo hayo ya diff, nimebadili napanda ALLYS sijaona kifafa chochote hapo. Hizo yutong za Green ni town bus nawashauri wanunue yutong za cross country double diff kama za shabiby.
 
Panda Ally's basi ya kiume saa 1 umeshafika Mwanza

mkuu hakuna basi linaloweza kuingia mwanza saa 1 jioni likiwahi sana ni saa tatu na nusu usiku hii inatokana na ratiba ..
 
mh jamani halilishindi basi la sumri lilivyo kimeo, nilisha wahi kutoka mbeya nikafika saa kumi na moja asubuhi dah tena likafia njiani baada ya kufika saa kumi na moja jioni au kumi na mbili. haya mabasi servise ni sifuri kabisa uroho wa pesa.
 
Back
Top Bottom