Burundi: Nchi masikini duniani

Mkuu umesisitiza kuhusu muungano na ndicho EAC inakifanya. Au unataka wajiunge vipi tena?
 
Somalia sio masikini kabisa, utahsangaa data zao zimekaa bora kuliko za Tanzania. Ila the last timr I checked Congo (DRC) ilikua ndio imeshika mkia. Sasa sijui hizi za Burundi kua ya mwisho kazitoa wapi. Labda atuwekee source.
Hata ikiwa ni kweli, sioni kwanini nchi iunganishwe na nchi zingine maskini. They will just drag the better off country down to their level maana na hizo zinazoonekana less poor are relying on aid.

Nilitoa hapa
Poorest Countries in the World

Naamini nchi zikiungana hasa za Afrika mashariki zitakuwa zimemaliza tatizo la ukabila, uwajibikaji kati ka mashirika ya umma na serekalini. Kabila lililokuwa linajiona kubwa ghafla litajiona kuwa tone kwenye bahari ya makabila. Kuungana kutaongeza brain power, sports power na research power. Itaunganisha mashirika yaliopo sasa hivi kati ka kila nchi na yatakua mashirika ya nguvu zaidi. Soko litapanuka, badala ya biashara yako kulenga wateja 45m uta target wateja zaidi ya 100m. Kwa hiyo idadi ya matajiri itaongezeka na hela zao zitakuwa nyingi zaidi. Bottomline muungano unaofaa utamaliza umasikini kwa mda mfupi tu.Viongozi wa afrika mashariki watuoneeni huruma wafanya vijimambo (Afrika mashariki tuwe super power na tuntengeneza nuclear bomb kama iran)Alafu hao viongozi watakumbukwa forever na kuingia kwenye vitabu vya historia.
 
Ni ajabu burundi hivi sasa wamekuwa maskini baada ya miaka hamsini of self-rule. Maskini kivipi. Kawaida ma NGO hawalali, wako juu ya kazi yao shughuli pevu kudhalalisha.watu wako katika hangover.
 
hivi umasikini wa nchi unapimwa katika nini? Nahisi wazungu walituwahi kutukariisha hii dhana ya Tanzania ni nchi masikini ili uwe mlango wao kuja kutupola kwa njia mbadala
 
Kwani wewe bwana mkubwa ukiwa masikini wa fedha utajiua?

una mawazo mgando!!!
 
burundi wamekuwa kwenye vita vya kupinduana miaka yote, mpaka sasa uhasama bado upo. Alafu hawana rasilimali yoyote ya kueleweka kwamba itawaongezea mapato zaidi ya kufuga wale ngombe wenye pembe zenye uzito mkubwa kuliko the rest of the body. Sasa tz miaka yote ya kutulia, ardhi yote,madini,mbuga za wanyama, maziwa,bahari, natural forests zote tunakuwa nafasi ya 22 kutoka mwisho unaona fahari?


Mkuu sioni fahali hata kidogo lakini si kweli kwamba kiuchumi wametuzidi ingawa nakubaliana na wewe vita na resources kuwa haba vimewaathiri sana!Nilichokipinga ni muheshimiwa kule alivyosema kwamba wao wapo vizuri kiuchumi kuliko sisi.
 
Mkuu umesisitiza kuhusu muungano na ndicho EAC inakifanya. Au unataka wajiunge vipi tena?

Hamna muungano unaofanyika. Dilly dally game for the next ten years, Utajua kuna muungano wakati utaanza kusikia kuusu referendum ili wananchi waamue hiki au kile. Nchi zinacheza kamare - poker against each other. Wana test waters na wanapo enda kwenye mikutano ya EAC kila nchi inaenda kwa nia ya kuvutia kitu fulani kwake na kuto kuwaiwa kwenye hiki au kile. Wakati wataanza kuungana the countries will not be playing against each other. They will be playing as a team against other federations and nations. Mkuu, Utazeeka ukiwa unasubiria muungano. Labda hapa kati wawe serious. Ukitaka kujua ukweli hoji clearing agents na watu wanao vuka vuka mipaka kama kuna unafuu kiasi gani sasa hivi na miaka kumi iliopita.
 
Kwani wewe bwana mkubwa ukiwa masikini wa fedha utajiua?

una mawazo mgando!!!

Mkuu, ukizungumza kuusu umasikini wa mtu binafsi ni tofauti na wa nchi. Ukizungumzia nchi masikini unamaanisha watu walio choka, waliokata tamaa na hawana njia ya kutoka. Desperation. Bora umasikini wa mtu binafsi unaweza kwenda kwa jirani. Kama mpo wengi hakuna wa kusaidia mwingine mnaanza kulilia Mungu amtume Musa tena.
 
Vita vya muda mrefu kati ya watu na watusi vimewaathiri sana kiuchumi. Waige alivyofanya kagame rwanda huweziamini kama kulikuwa na genocide 1994.
 
Back
Top Bottom