Jana niliangalia kwa hamu kubwa ili nione jinsi wana Shinyanga walivyomuaga shujaa wao, lakini kwa bahati mbaya TV zote hazikulimulika tukio hili, sidhani kuwa hawakuwa na taarifa nalo bali inawezekana ni juhudi za CCM kuwanyima sauti wananchi waamini kuwa vyama vya upinzani (hasa Chadema) havina wafuasi na wanalipoti pale tu kunapokuwepo na habari yenye mtizamo hasi.
Hawataweza.... RIP Shelembi!
Shelembi kwa jadi alikuwa kama Derefa kwani lafudhi yake ya kisukuma kamwe haikuachi mbavu zikiwa salama.RIP ''lutunya mwana nyenze Shilembi".Upande wa Pili wa ujumbe wa Zitto unatuonyesha jinsi Shilembi alivyosurvive kigumugumu ndani ya Chadema maake kumtetea Wange Rasta ilikuwa ni kugeuka adui wa moja kwa moja kwa Mbowe.Hii inanipa imani kuwa msimamo wake upande wa Zitto ni "changamoto" lakini kwa Mbowe ni "uadui".
Jiwe la pili limedondoka huku likiwa bado kazini sasa sijui ni nani tena atawarithi hawa maake kumkabili mbowe si kazi ya kitoto .Sijui Zitto ama Shibuda wanaweza kumuenzi Mzee huyu?