Buriani Fr Isidory Nyonzo wa Morogoro!

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,598
Leo asubuhi nimepata habari za kusikitisha sana kuwa Fr Isidory Nyonzo wa kanisa kuu la Morogoro amefariki dunia na kuzikwa jana. Nimesikitika sana kwani ameondoka kabla sijatimiza ahadi yangu ya kwenda kumtembelea.

Ni mtu wa pekee sana katika historia ya maisha yangu na kifo chake kimenigusa sana. Naamini Mungu ataipokea nia yangu na salamu zangu atazipokea huko alikopumzika katika raha ya milele.

Bwana ametoa, bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe amina. Fr Nyonzo apate rehema kwa Mungu apumzike kwa amani....Amina.
 
R.IP

Lakini umesema tu kanisa kuu la Morogoro hujasema kanisa gani?? RC, Anglikana, Lutheran (Jokes)
 
Poleni saana Mzee DC... Na nawaombea kwa Mwenyezi Mungu
awatie nguvu na kuwaongezea imani...

May he rest in peace...
 
RIP Fr Nyozo.

DC, ni Fr Nyonzo aliyewahi kuhudumu kanisa la Mvomero miaka ya 80-90?

Sina hakika mkuu ila inawezekana. Mimi nilikutana naye kanisa kuu la RC pale Moro mwanzoni mwa 2000. Tulielewaana sana kwa kipindi kifupi nilichokaa naye. Pamoja na kwamba alikuwa na umri wa karibu miaka 80 wakati huo, bado alikuwa na nguvu za kufanya mambo mengi. Na zaidi ya yote alikuwa na hekima na busara.
 
Kwa umri huo ulioutaja, most likely atakuwa yeye. Alikaa muda mrefu tu kanisa la Mvomero. Nilipata komuniyo ya kwanza kupitia kwake.
 
Kwa umri huo ulioutaja, most likely atakuwa yeye. Alikaa muda mrefu tu kanisa la Mvomero. Nilipata komuniyo ya kwanza kupitia kwake.

Kweli umri wake ulikuwa mkubwa sana. Jnne ya wk iliyopita nilikuwa Moro kwa muda mfupi sana na niliambiwa kahamishiwa nyumbani kwa Askofu kwa uangalizi zaidi na kwamba afya yake ilikuwa imedorora sana. Nilitamani sana kwenda kumwona lakini nikajishawishi kwamba nitarudi rasmi... I wish I made a wise decision to visit him...Now it is too late.

Mungu atanisamehe!
 
Back
Top Bottom