Buriani Amina Chifupa!

Status
Not open for further replies.
kwa kweli Watanzania wote kwa ujumla nadhani tutakuwa tumeipokea habari hii kwa majonzi na masikitiko, Amina alikuwa bado mdogo sana na alikuwa ndio kwanza anaanza kutafuta mafanikio... pia marehemu ameacha mtoto mdogo ambaye nadhani ana umri wa miaka 4 tu bila ya mama ni ngumu kwa kweli.

Watanzania wenzangu wote ambao tulimsema Amina kwa mabaya inabidi tuombe hata kimoyo moyo atusamehe cos hakuna mtu aliye msafi hapa duniani kila kiumbe ambacho kipo hai na kinatembea kina madhambi/mapungufu yake.

Huu sasa ni wakati wa kumuombea marehemu m/mungu ailaze roho yake mahari pema peponi na si kuanza kuendelea kumsema au kumtafuta mchawi.... hakuna mchawi m/mungu amekitaka kiumbe chake na hatuna budi kuukubali ukweli.

mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu dada yetu Amina chifupa Mpakanyia mahali pema peponi. Amin.
 
inna lillahi wa innna ilayhi rajiiun nnaandika machozi yanilenga lenga machoni.

ni jaala yake mola alietuumba na alietupangia wakati lakini inaumiza sana.

mola amuweke pahala pema peponi na hili pia liwe funzo kwetu tusikubali kuchezea maisha ya watu namna hii.

mola awape moyo wasubira wafiwa wote na wale wote tuliokuwa tukimuombea na kumtakia mazuri
 
Mkandara,
Nilikuwa nakuja kupost hii news, nikakuta tayari umeshaiweka.
Nilikuwa naongea na wanafamilia huko home, ndio wakaniambia kuwa walikuwa wanaangalia breaking news kuhusu kifo cha Amina.
Sina cha kuandika kwa sasa zaidi ya kusema roho inaniuma sana.

Ninaungana na familia za Chifupa na Mpakanjia, pamoja na waTZ wote wenye mapenzi mema katika kuomboleza msiba huu mzito, na wenye kutia simanzi kubwa.
Mungu ailaze roho ya marehemu Mhe. Amina Chifupa mahali poema peponi, Amen.
 
kwa wale wataonafasika wajitahidi kumsindikiza mwenzetu, na sisi tuliobakia tujitahidi kumuombea dua mola amuweke pahala pema peponi na ampe makuzi mema mwanawe na subira ya kutosha wafiwa wote
 
Bwana ametoa Bwana ametwaa.Kama ni kazi ya Mungu basi tunakubali matokeo kwani God's case no appeal,lakini kama ni hizo polonium ndani ya CCM basi wahusika watambue kuwa siku yao inakuja.
 
Bwana ametoa Bwana ametwaa.Kama ni kazi ya Mungu basi tunakubali matokeo kwani God's case no appeal,lakini kama ni hizo polonium ndani ya CCM basi wahusika watambue kuwa siku yao inakuja.
 
Nikiendelea kutafakari huu msiba, naanza kukumbuka post za mwanakijiji kuhusu hili jambo nikianzia na ile ya free Amina. Mwanakijiji alitutahadharisha juu ya hatari iliyokuwa inamkabili huyu binti kwa kuzuiwa kuongea. Nitakuwa wa mwisho kuamini kwamba kifo hiki ni mapenzi ya bwana!
 
A national is only as strong as the character of its citizens
 

Attachments

  • ndiyo maisha.doc
    29.5 KB · Views: 138
Jamani ndo maisha haya... lakini ametutoka wakati familia na jamii nzima ikimtegea sana.

Bwaa alitoa na Bwana ametwaa jina lake litukuzwe

Amlaze pema peponi
 
RIP AC, it is very sad indeed, my heartfelt condolences to the family
 
Nikitafakari huu msiba, naanza kukumbuka post za mwanakijiji kuhusu hili jambo nikianzia na ile ya free Amina. Mwanakijiji alitutahadharisha juu ya hatari iliyokuwa inamkabili huyu binti kwa kuzuiwa kuongea. Nitakuwa wa mwisho kuamini kwamba kifo hiki ni mapenzi ya bwana!


Nimejaribu kutafuta ile thread ya free Amina siioni je imeshawekwa kapuni?. Nilikuwa nataka kuipitia tena kwa makini baada ya msiba huu kwani ni kama Amina was never freed since then.
 
Hakika mazingira ya kifo cha dada huyu yanahitaji imani ya kumwezesha mtu kutembea juu ya maji, kuamini kwamba ni kifo kwa mapenzi ya Mola. Is more than a coincidence!

RIP Amina.
 
Wakuu.
Nilitoka kidogo wenye ushauri kwangu nimesikia. niliaombwa na Dua mwanzoni niache nikakubali, wakaja vidudu mtu wakasema sina data ndio nikaamua kuendelea si nia yangu kuwakwaza watu. all in all file bado ninalo la mheshimiwa.

siku chache nilieleza kuwa hali ya Amina sio nzuri hamjui nani anaingia na nani anatoka nikaomba waheshimiwa wakamsalimie mgonjwa lakini naona wako busy na kutizama protocal jinsi ilivyokosewa wakati timu ya Taifa inaenda bungeni. wenye nia ya kumpa pole mgonjwa waniPM niwape mobile yake mumtumie salamu za kuimfariji. sisi tuwe rafiki wa shida kwenye uhondo tuwaachie wenzetu.

Mswahili ulikuwa na huruma sana kwa AMINA na familia yake. AMINA lala salama.
 
Let it be known, kwamba kama ni mkono wa Nchimbi, ingawa wengi wetu tunakuwa wanafiki kujaribu kukataa kwamba hahusiki; then huo uraisi ambao anataka kuupata kwa nguvu za giza hataupata hata akiamua kuwaua wapinzani wake wote. Kwanza Ipyana then Amina Chipufa. Huyu jamaa inabidi ashughulikiwe.
 
Mzee Mswahili,

Ahsante kwa kutuletea hizi habari mkuu wangu, ni habari nzito hizi, tena sana, ninamuombea Marehemu kwa mwenyezi Mungu amlaze pema peponi, ni ustaarabu kuwapa muda ndugu na jamaa wa marehemu waweze kuzika na kuomboleza,

But, nina promise one thing!, kuwa hapa forum tuta-get to the bottom of this thing, enough, hiki kifo kinafanana sana na Marehemu Ipyana, ambaye in his case ilikuwa sambusa, nasikia safari hii ilikuwa ni samaki!

Sasa fasten Your Belt, kuna mzee mmoja ambaye amekuwa akiwatumia text message watu mabli mbali toka kifo kilipotokea, tunauliza baba kulikoni ya Ngoswe yakakuhusu mpaka kutumia hela zako zote hizo kutuma hizo message?

Mungu amlaze pema marehemu, Amina!
 
But, nina promise one thing!, kuwa hapa forum tuta-get to the bottom of this thing, enough, hiki kifo kinafanana sana na Marehemu Ipyana, ambaye in his case ilikuwa sambusa, nasikia safari hii ilikuwa ni samaki!

Sasa fasten Your Belt, kuna mzee mmoja ambaye amekuwa akiwatumia text message watu mabli mbali toka kifo kilipotokea, tunauliza baba kulikoni ya Ngoswe yakakuhusu mpaka kutumia hela zako zote hizo kutuma hizo message?

Mungu amlaze pema marehemu, Amina!


Mzee ES,

Please,

Tupe mwanga kuhusu huyu mtu anayefurahia msiba huu kwa kusambza txt messages; just expose him. Watu wa aina hiyo watatumalizia wanasiasa wazuri kusudi wabaki peke yao.

MUNGU ILAZE PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU AMINA
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom