Bungeni zijadiliwe hoja, kanuni, pongezi, miongozo, mipasho, utani, vijembe iwe home work

The Analyst

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
464
246
Habari zenu wakuu. Najaribu kutafakari Bunge letu na kukiri kwamba limechangamka sana lakini linaanza kukera kwa kelele ambazo mimi naona hazina maana sana. Angalieni usomaji wa kanuni kila dakika mbunge anapotaka kusema jambo na kanuni hiyohiyo kusomwa mara kadhaa kwa kitendo kilekile ndani ya kikao kimoja. Angalieni muda unaotumika kupongeza unaotumiwa na mawaziri na wabunge...baadhi wanawapongeza na kuwashukuru hadi familia zao, wapigakura wao na mbunge au waziri mwenza. Jamani...jamani ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia ya mawasiliano waheshimiwa hawa hawawezi kutumia simu, mtandao kumshukuru wake au waume zao hadi wapewe nafasi ya kuzungumza Bungeni? Haya ni matumizi mabaya ya muda wa kujadili mambo ya msingi. Eti waziri anamshukuru rais kwa kumteua wakati wa kikao cha bunge wakati wanakutana hata kabla ya kuapa kutumikia nafasi hiyo, kwa nini asimshukuru na kutoa ahadi zake huko? ....This is crazy!

Angalieni mipasho, utani, kejeli, vijembe na jinsi mambo hayo yanavyopoteza muda wa Bunge na mwishoni wanaishia kupitisha bajeti haraka haraka pasipo kupitia baadhi ya vifungu kwa kisingizio cha muda kumalizika. Hauhitaji calculator kujua kwamba muda wanaotumia kina Lema, Chatanda, na wapenda vijembe wengine, unatosha kabisa kumalizia zile dakika zinazopungua kila bajeti zinapokuwa zinapitiwa kifungu nadi kifungu especially around saa mbili usiku.
Napendekeza wabunge/mawaziri/spika/wenyeviti wasome kanuni wanapokuwa nje ya ukumbi na kuwa huru kuzitumia pasipo kupoteza muda mwingi kuzisoma wakati wa mjadala. Waheshimiwa hawa pia wakawashukuru wapiga kura wao wanapowatembelea majimboni kwao na si wakati wa kujadili mambo ya maana. Baadhi ya viti maalum wakianza kuzungumza utatamani uzime TV. Baadhi yao wanachojua ni mipasho, masimango, maudhi utadhani........... Jamani mambo mengine yafanyeni wakati wa mapumziko na si wakati wa vikao!
 
Habari zanu wakuu. Najaribu kutafakari Bunge letu na kukiri kwamba limechangamka sana lakini linaanza kukera kwa kelele ambazo mimi naona hazina maana sana. Angalieni usomaji wa kanuni kila dakika mbunge anapotaka kusema jambo na kanuni hiyohiyo kusomwa mara kadhaa kwa kitendo kilekile ndani ya kikao kimoja. Angalieni muda unaotumika kupongeza unaotumiwa na mawaziri na wabunge...baadhi wanawapongeza na kuwashukuru hadi familia zao, wapigakura wao na mbunge au waziri mwenza. Jamani...jamani ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia ya mawasiliano waheshimiwa hawa hawawezi kutumia simu, mtandao kumshukuru mkewe au mumewe hadi apewe nafasi ya kuzungumza Bungeni?
Angalieni mipasho, utani, kejeli, vijembe na jinsi mambo hayo yanavyopoteza muda wa Bunge na mwishoni wanaishia kupitisha bajeti haraka haraka pasipo kupitia baadhi ya vifungu kwa kisingizio cha muda kumalizika. Hauhitaji calculator kujua kwamba muda wanaotumia kina Lema, Chatanda, na wapenda vijembe wengine, unatosha kabisa kumalizia zile dakika zinazopungua kila bajeti zinapokuwa zinapitiwa kifungu nadi kifungu around saa mbili usiku.
Wewe sio analyst as far as the literal meaning of the subject concerns!
Ni vema ukawa fair kwa kutaja source ya ulichopaste hapo juu!
Hayo ni maongezi Live ya kipndi cha HOJA YANGU kilichorushwa Live na ITV usiku huu!
Umemnukuu Mama Ananilea Nkya neno kwa neno na ku,paste hapa, halafu huweki source!
Tujifunze kuthamini mawazo ya wenye Hekima kwa kunukuu maneno yao na si kufanya PIRACY!
 
Nashukuru kwa mawazo yako! Bahati mbaya hapa ninapoishi sipati ITV. Ni kweli, mimi siyo Analyst kwa maana unayoitaka wewe. I'm just a simple guy. Hata wewe naamini si Paka. Are you? God! ....These are just ID's! Didn't you learn about that when you joined the forum? Next time ukihisi mawazo ya mwanaJF mwenzako yanafanana kwa aina yeyote na source unayoijua wewe ukadhani amekopi bila admission ni vizuri ukasoma kazi/post zake nyingine kwa sababu napata hisia kwamba unajaribu kunihukumu kama nisiye na uwezo wa kupresent ninachokiwaza isipokuwa hadi nikopi ITV.
Nasikitika kukujulisha kwamba sijatazama ITV na wala siyo mbovu kiakili kama wewe unavyodhani. I might not be the best but I believe and know that I'm good enough. Thanx anyway!....Paka!
Wewe sio analyst as far as the literal meaning of the subject concerns!
Ni vema ukawa fair kwa kutaja source ya ulichopaste hapo juu!
Hayo ni maongezi Live ya kipndi cha HOJA YANGU kilichorushwa Live na ITV usiku huu!
Umemnukuu Mama Ananilea Nkya neno kwa neno na ku,paste hapa, halafu huweki source!
Tujifunze kuthamini mawazo ya wenye Hekima kwa kunukuu maneno yao na si kufanya PIRACY!
 
Wabunge viti maalum kuwa mabingwa wa mipasho, utani, kejeli na vijembe ni kwa sababu wako humo mjengoni kwa kazi hiyo. Ni cheerleaders. Wengi, hasa wa CCM, hawana uwezo hata wa kuwa wajumbe wa nyumba kumi.
 
Nakubaliana na wewe kwa baadhi ya mambo uliyoyawakilisha hapa jamvin kuhusu hayo madudu wanayofanya badhi ya wawakilishi wetu.Kunajambo moja ambalo nimeligundua kutokana na kufuatilia hiyo mikutano ya bunge inayoendelea,inapotokea wabunge wa upinzani wanapokuwa wanatoa hoja nzito zinazoikaba koo serikali hapo ndio utaona wabunge wengi wa ccm wanapoomba mwongozo ili kujaribu kuinasua serekali,na sidhani kama ninahitaji kuwa na elimu kama ya malehem shekhe Yahaya kutabiri ya-kwamba bunge hili litavunja rekodi kwa wabunge kuomba mwongozo.Mwisho sidhani kama kuomba mwooga ni kitu kibaya ila wajaribu kuomba mwoongozo ulio na tija kwa wanao waongoza isiwe kwaajili ya maslai ya vyama vyao.
 
Halafu wajanja kweli, pindi Mbunge wa upinzani anaposimama na kuanza kuchangia utasikia spika anaanza kulalamika kuhusu muda. baadaye ndio utagundua kwamba muda mwingi umetumika kutuma salamu na kutaja majina ya wachangiaji, halafu imeshakuwa kama mchezo kila mtu siku hizi anaalika familia yake kutembelea bungeni ama kuwatumia hizo salamu na wakati utakuta walikuwa pamoja masaa machache yaliyopita, ni kama wapo kwenye mashindano vile.
 
Back
Top Bottom