Wamunzengo
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 810
- 321
Binafsi siku nilipoigundua tu JF, nikatafuta na modem kabisaaa ili nifuatilie mambo ya nchi yangu kwa upana zaidi. Mwakyembe na Membe ni mfano tu, ila NADHANI hakuna mwanasiasa hapa Tanzania asiyetupia jicho hili jamvi. Maana hapa unaambiwa ukweli ulivyo japo wengi hawapendi. Msisahau viongozi wetu wengi ni waborongaji kwa kiwango fulani, halafu hawapendi kukosolewa. Ila naamini wameshaanza kuzoea kukosolewa bila kuonewa aibu, na hii itawajenga sana kisiasa maana walizoea kukosoana kishikaji kwenye vikao vyao vya kichama. JF bhana ni full doze, kasoro sawa zipo, lakini huwezi ukapuuza mchango wa JF kwa siasa za Tanzania mijini hasa kwa hivi karibuni. Nadhani ndo maana ccm inapata taabu mijini maana watu uelewa wa mambo ni mkubwa.