Bungeni: Waziri Membe aiponda taarifa ya Wenje aihusisha na JamiiForums

Bora WENJE amelisema,mi inanisitisha sana kuhusu Rais wetu
 
Mkuu,

Si kama inahusiana na Wenje, bali Wenje alisoma maoni ya Waingereza dhidi ya Rais wetu; lakini kauli ya Membe kama ya Radhia Sweety, hawajaangalia SOURCE LINK na kufikiria.

Membe kakiri kuwa Guardian walifanya coverage ya JK vema akiwa Davos, jambo jema! Lakini kusema uki-google habari yenyewe unaishia JamiiForums ni kutoelewa search engines zinafanyaje kazi.

Maoni hayo yapo tovuti ya Guardian mpaka dakika hii na unaweza kuyaona kwenye link hii: Davos 2012: Day two, as it happened | Business | guardian.co.uk

Membe anajua ku-google au kutumia search engine? msiwe mnamlalamikia kumbe mwenzenu uwezo wake wa ku-google unaishia JF.
 
Tatizo Watawala wa Tanzania hawajui hata kutumia Internet wanachojua wao ni kutype MS Word basi, msiwaone wakibeba Ipad na Laptop's mkajua wanajua kuzitumia wengine ni wanabeba ili kuwatisha wananchi ili wasionekane wapumbavu
 
ZITO ameendelea kuthibitisha asivyojua vitu. Spika amepiga swali lake chini. Ni aibu kwa mmbunge kama Zito kutokuelewa kuwa wanachopitisha hapo bungeni ni makisio na sio kitu halali. Ni aibu kumuomba Waziri wa fedha ajikomit kuwa atawapa wizara ya mambo ya nje fedha yote waliomba. Kama mtu aliyemo ndani ya mjengo anakuwa na uelewa wa aina hii mlala hoi wa Mwanarumango atasema nini?
 
Sasa Nimeelewa, Na Membe ameongea Kwa uchungu ...TUSIWE WANAFIKI- Wizara inahitaji Pesa na niwajibu ipewe 100% ya Bajeti yake...Wizara Haiwez ikaenda kwa 46% ya bajeti.Wizara ya fedha itoe Pesa..Tuache Siasa tuangalie Goals za Wizara Baada ya kupewa pesa

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Kwa ujumla Membe ameonesha udhaifu mkubwa leo, kadri anavyotaka/alivyotaka kuonesha kuwa anafaa kuwa presidential material ndo kadri anavyoharibu zaidi. Mbali ya hilo la kushindwa kuelewa mantiki ya hoja, pia ameonesha udhaifu katika collective responsibility. Maana kaenda pale kwenye podium kuzungumza maneno ambayo alipaswa kuyazungumza kwenye Baraza la Mawaziri.

Alichokuwa anafanya ni one man show! Kujipambanua kuwa yeye hahusiki, bali ni wizara zingine, tatizo ni bajeti, ooh, mara hakuna ministerial linkage...and so so so so!

Muda wote alikuwa analalamika. Naona hata spika hapa anampiga below the belt here kuhusu suala hilo!
 
Mawazir wakishindma kujibu maswali wanakimbilia kusema hizo ni habar za jf. Siku hiz wamefanya jamii forum kuwa jibu lao. Shame on you membe shame on you samuel sitta. Wote hampati u rais ng'o
 
Mawazir wakishindma kujibu maswali wanakimbilia kusema hizo ni habar za jf. Siku hiz wamefanya jamii forum kuwa jibu lao. Shame on you membe shame on you mwakyembe.
 
Nilichokipenda ni kuwa membe naye ana browse Jf. Nadhani hata brazake anabrowse pia

Mkuu mi naamini hata lile baraza la usalama la taifa kabla halijakutana jtatu, lazima wapewe taarifa ya habari mpya zilizojiri JF
 
Hivi tatizo la Membe hapo ni ukanjanja, kutosoma, kutofuatilia mambo ya msingi hasa yanayohusu wizara yake au ni siasa za CCM za kukoroga na kufunika kombe mwanaharamu apite wakijua kuna makanjanja wachache kama akina Radhia watawapigia chapuo na kuwashabikia??

Najiuliza sana nashindwa kupata jibu hapa.
 
Nilichokipenda ni wakati spika wetu anahitimisha leo ktk wizara ya mambo ya nje, ambaye huwa hatabiriki kwa mwambia Membe kuwa ati na wewe ni sehemu ya serikali na aache kulalamika yakuwa bajeti ya wizara hii haitoshi,tumebinywa sana. Tafsiri yake nini?

Kuna hali ya kutoelewana ktk baraza la mawaziri na hasa wizara ya fedha
 
ZITO ameendelea kuthibitisha asivyojua vitu. Spika amepiga swali lake chini. Ni aibu kwa mmbunge kama Zito kutokuelewa kuwa wanachopitisha hapo bungeni ni makisio na sio kitu halali. Ni aibu kumuomba Waziri wa fedha ajikomit kuwa atawapa wizara ya mambo ya nje fedha yote waliomba. Kama mtu aliyemo ndani ya mjengo anakuwa na uelewa wa aina hii mlala hoi wa Mwanarumango atasema nini?

Makisio na makadirio.... Then wizara inapewa 46% ya makadirio yake?? Si ujuha huo?? Sasa makadirio gani hayo ya kuwaponza wananchi kwa libajeti likubwaaa kumbe uwezo wa kukusanya kodi na kuomba omba ni sifuri.

Huu ni ubakaji wa wazi wa mategemeo ya wananchi.
Mnapitisha budget hewa? Wizara ngapi zimepata 100% ya bidget zake mwaka uliopita? Labda wizara zenye ulaji!
I bet..... Kapekue utaona. Wizara ya viwanda ilipata 26 bilion kati ya 57b walizoomba.
 
Naona sasa mawaziri wanashindwa kuelewa kitu kimoja, unapopata taarifa si vizuri kukimbilia kuwa hiyo ni taarifa ya kupiga, fanyia kazi kwanza ndo ujiridhishe, vinginenvo utang'aka baadae ndo utaona kuwa duhh, kumbe ni kweli, unabaki, ningejua!
 
Sio Kila mzungu Padre ...Mkabeba Maneno yake na Mkachukua kama Yalivyo...hata humu JF kuna story nyingi sana.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Hili lilianza na Mwakyembe na sasa linakuja kwa serikali yote kusingizia taarifa kutengenezwa na JF sasa ndo nchi inapotea kabisa kama viongozi wameanza kukanusha habari sahihi kwa kuseam ni za JF!
 
Nilichokipenda ni wakati spika wetu anahitimisha leo ktk wizara ya mambo ya nje, ambaye huwa hatabiriki kwa mwambia Membe kuwa ati na wewe ni sehemu ya serikali na aache kulalamika yakuwa bajeti ya wizara hii haitoshi,tumebinywa sana. Tafsiri yake nini?Kuna hali ya kutoelewana ktk baraza la mawaziri na hasa wizara ya fedha
 
Tunazidi kuboresha verified user's list kutoka kwa viongozi wakubwa wa nchi hapa JF.

Alianza Mwakyembe, baadae akafuatia Afisa Afya mkoa wa Kagera na leo ameongezeka Membe.

Ni vizuri kujua kwamba nao ni members hapa JF, ingawa kwa bahati mbaya sana kuwepo kwao hapa hakuwasaidii kuujua ukweli wa mambo na kuusema kama ulivyo.

Tuendelee nao hivyo hivyo iko siku watakiri hadharani kwa kiasi gani wamekuwa wakinufaika na JF.
 
Back
Top Bottom