Elections 2010 BUNGENI: Upinzani upo ndani ya kambi ya upinzani?

Kwa haya yanayoendelea huko Bungeni inadhihirisha kwamba hawa wenzetu wa CUF ni vibaraka wa CCM na sio wapinzani. Katika kinyang'anyiro cha uspika walisema kura zao zote zitakuwa kwa Marando lakini kwa hesabu za haraka tu inaonekana waliwapigia CCM na si vinginevyo. Ukija katika suala la kiongozi wa upinzani Bungeni wao wanampinga Mbowe wakati kwa mujibu wa sheria Chadema ndiyo wanatakiwa kuunda na kutoa Kiongozi wa upinzani lakini hawa wenzetu wa CUF wanapingana na sheria, hivi kweli hawa ni wenzetu?
 
Ulipaswa kujua CHADEMA ndicho chama pekee cha upinzani tangu wakati wa uchaguzi mdogo wa Tarime. Waliandamwa na kila chama. Kuanzia chama chakachua Matokeo (CCM) mpaka bendera ufuata upepo (CUF). Naamini siku moja tutakamata dola. Kama unabisha hiyo imekula kwako
 
Kwani chadema wao si wamesema wapo 12% na wanatosha? nadhani bunge sio sehemu ya majaribio wapinzani wengine wanaona mbali ndio maana wamempa mtu mwenye uwezo tatizo la chadema wameshalewa ukubwa mapema!!!!

Kamwene bee, kambwa
avatar10026_2.gif
kenyewe kalikuwa kadogo. Ukichinja niite.
 
Halima mdee=viti maalum wote wa CCM na CUF + kumi wa kuchaguliwa wa CCM+Ana makinda
Tundu Lisu=jk+sitta+pinda+EL+RA+ wengine sitini
Mnyika=wa kuchaguliwa wote wa CUF+NCCR+UDP+TLP +majimbo waliyoiba kura ya segerea, temeke,kinondoni,ilala na kigamboni

Zitto=jaza mwenyewe
Vicent Nyerere=endelea
Mbowe=acha kabisa

utakuwa ujinga kwa ccm kuwapa watu wanaotoka a small area as pemba kuunda serikali ya upinzani il hali wapo wanaotoka almost all corners of the country. mwaka 2015 hiyo move itatumika kuwaadhibu sana.
Naisikitikia JF, zamani ilijizolea sifa kemkem katika ujenzi wa hoja na kumkoma nyani gidali kweupe.
Siku hizi ni kijiwe cha matusi na dharau!
 
Tutafakari kwa kina kinachojiri katika kambi ya upinzani hivi sasa. Nahisi kuna msukumo fulani usioonekana ki-urahisi – lakini mtu anaweza kufanya deductions zake.

Hivi mtu kama Rostam, Manji, Subhash Patel, El na wengineo mafisadi mapapa wanaipenda Chadema kweli? Kwa mtazamo wao, wanakiona kweli hiki ni chama kinachoweza kulinda masilahi yao? Tuambizeni ukweli hapa jamani!

Halafu tunasikia kwamba Rostam na CUF kinaeleweka sana hadi kufikia kukisaidia chama hicho kifedha -- kwa siri. Hili sina uhakika nalo lakini linasemwa sana. Ninacho uhakika nacho ni uswahiba mkubwa kati ya Jussa na RA. Hakuna mwenye kubisha hapo.

Profersa Lipumba naye alinitia wasiwasi sana mwaka juzi alipoitisha waandishi wa habari na kumbwatukia Mzee Mengi alipowataja hadsharani mafisadi papa akiwamo Rostam.

Ilikuwa ni lazima kwa Lipumba kufanya vile? Si bora angekaa kimya tu, kuliko kuwapa mafisadi support yoyote ndogo wanayohitaji? Mimi nadhani ile support waliinunua!

Lipumba alirudia tena katika sakata la mitambo chakavu ya Dowans – alitoa kauli za kusupport kununuliwa mitambo hiyo ya kifisadi inayohusishwa na Rostam na EL. Alitumwa tena?

Kwa hiyo unaweza kukuta kwamba hivi sasa kambi ya CUF inasukumwa kutoshirikiana na Chadema na wanaotoa msukumo huo wanacheza karata yao kwamba inaweza ikapatikana technical loophole ya wao, wakiungana na vyama vingine vinaweza pia kuunda kambi ya upinzani.

Hawa mafisadi wanataka ku-control serikali na upinzani pia – hasa upinzani ule usiokuwa na principles.

Kwa mfano wanaweza kuweka utaratibu kwa kubadilisha kanuni kwamba kama kuna kambi mbili za upinbzani zinapingana, basi Bunge likae na kupiga kura kuchagua kambi ipi ndiyo iwe rasmi.

Nakiri kwamba hii scenario niliyoitaja ni ngumu kuikubali ingawa ni ni possible, hasa kwa siasa zetu hizi zilizojaa uchafu wa kila aina. (Namhurumia Anne Makinda!!)

Kwa upande mwingine mwanasiasa kama Hamad Rashid Mohamed ni muadilifu sana kwqa muonekano wake – naamini kabisa hawezi kukubali kuingiliwa na mafisadi wa type ya akina Rostam.

Naomba kuwasilisha.
 
Ni hisia zako, kwani minority wakiamua kuungana kuna shida gani? Maelewano yapo ndio maana kambi rasmi ina uongozi wake na wameapishwa wao kwanza kama sehemu ya uongozi wa Bunge la 10
 
Ulipaswa kujua CHADEMA ndicho chama pekee cha upinzani tangu wakati wa uchaguzi mdogo wa Tarime. Waliandamwa na kila chama. Kuanzia chama chakachua Matokeo (CCM) mpaka bendera ufuata upepo (CUF). Naamini siku moja tutakamata dola. Kama unabisha hiyo imekula kwako

Kinachowasaidia Chadema ni chama cha wananchi, wako karibu na wananchi.
 
ndio maana mara kadhaa mimi nimekua nikiwaambia watu, hakuna haja ya CHADEMA kuungana na CUF, NASEMA HAKUNA HAJA, CUF wanaagenda zao za siri zinazowasukuma katika siasa, na niagenda za Ubinafsi na mambo yasiyofaa kwa TZ, CUF leo inapambana na CHADEMA kwa nguvu kuliko wanavyopambana na CCM, nimekuwapo Mwanza, Musoma Mjini, Tarime, Mbeya, Iringa, Tanga, Kilimanjaro na Arusha, Sehemu zoote hizo, CUF wamekua wakirusha madongo mazito yakuwashambulia CHADEMA, ila sishangai, wana Agenda yao, na upo ushahidi wa namna chama hicho kinavyofungamanishwa na pesa chafu za mafisadi na magaidi.
si kipindi kirefu tutaujua Ukweli, kuna Mpasuko unawanyemelea,
Uswahiba wao na ccm UMEANZA MIAKA mingi , sasa mapenzi yameshamiri kila jambo hadharani, VIVA CHADEMA, hakuna kurudi Nyuma.
 
Hayo ni mawazo yako mkuu mimi napenda mabadiliko lakini kwa yaliyotokea jana na leo dodoma chadema hamna haja kumtafuta mchawi mchawi ni nyie wenyewe kwa vyovyote itakavyokuwa nina imani upinzani wa kweli bado haujazaliwa na kama upo basi sio huu wa chadema pengine haujapata nafasi na tungoje 2015.
 
Hawana agenda ya siri ila sehemu kubwa ya viongozi wao waliokuwa wanalipwa na chama sasa watalipwa na serikali ya Zanzibar hivyo kukifanya chama kiwe na ziada ya pesa za kujitangaza
 
Hayo ni mawazo yako mkuu mimi napenda mabadiliko lakini kwa yaliyotokea jana na leo dodoma chadema hamna haja kumtafuta mchawi mchawi ni nyie wenyewe kwa vyovyote itakavyokuwa nina imani upinzani wa kweli bado haujazaliwa na kama upo basi sio huu wa chadema pengine haujapata nafasi na tungoje 2015.

hatuwahitaji CUF katika hatua zoote za mafanikio ya chama chetu, hatuhitaji watu wakati, watu vuguvugu, tunataka watu wenye msimamo thabiti, nia na malengo yao yasiwe yakutiliwa shaka.
cuf NI SEHEMU YA SERIKALI KULE znz, Ambapo Rais wa nchi hiyo ni member wa Cabinet, kwa lugha nyingine Seif kama makamu wa Rais anaruhusiwa kuingia CABINET ya Jamuhuri kama Rais wa Znz hayupo.
hivyo CUF ni sehemu ya maamuzi ya serikali ya Jamuhuri ya muungano, CUF ni branch ya CCm katika Uendeshaji Taifa.
hawaaminiki, ni watu ambao wamekata tamaa.
 
chadema ni after maslahi

hilo Utajua mwenyewe, lakini CUF ni ccm B, kimaadili, kisheria, na kimuonekano.
WATANZANIA WAMEAMKA, WAMEGUNDUA, imebaki kwa ndugu zangu Wapemba wachache, na wale wamamkonde kule kusini.
 
Haya Bwana!! kwa hiyo chadema ndio pekee wapinzani!

back to the history, see reality, know what is real happening in these parties!

Note that, we have no opposition parties and chadema they are not among them!! neither ccm!!!!!!!!!

labda mtu aniambie kuwa idadi ya wabunge wa chadema inaweza kuleta mabadiliko yanayoweza kuonekana, zaidi ya kuongea,

bado hawana nguvu na kubaguana huku na kutengana kwao huku ndio kunakopelekea kusema chadema hipi unayosema ya wapinzani? waliopata urais asilimia 24 ndogo zaidi ya aliyopata Mrema mwaka 1995!! acheni ushabiki we have long way with these sorts of mind!

hoja yako ya kuwa serikali ya mseto ya cuf na ccm kinaiondoa cuf kuwa chama cha siasa ni ya hatari na ya kupingwa mno, unaishi karne ya 11 au 12 hivi! tunahitaji serikali kama hiyo Tanzania bara pia!

katika serikali ya mseto, viongozi wanataka uongozi ili walete kitu fulani unique na kuweka historia kuwa walitatua matatizo fulani, hawapati uongozi kwa sababu ya dhiki zao na wajaze matumbo yao kama viongozi wengi wanavyowaza!

with such mind of yours, never expect kuwa kura yako vote(latin-votum) which means 'choice' au 'wishes' kuwa itafanya kitu chochote.

ni ujinga na upumbavu uliotukuka kuamka asubuhi kumpigia kura Slaa ili awe rais, yet anakosa urais , lakini kura yako haina nafasi yoyote ya kihistoria, that led 10million people not to vote just recently!!

serikali ya mseto ingemfanya Slaa kuwa mmoja wa watu watakaounda serikali, I mean chadema ingepewa kama wizara 4 hivi, ndio kenya wanavyoishi hivyo, so as South Africa etc......

Tuwaze mabadiliko ya katiba yatakayo accomodate vyama vyote, kama kuna vyama vitakavyochemsha automatically vinakimbiwa na wananchi!!!!

nchi ni ya wote regardless of our respective vyama!!! haiwezekani aliyeshinda asilimia 61, atuongoze miaka mitano ijayo, na haikuwezekana zanzibar waliopitana kwa asilimia 1% basi ccm waongeze serikali-ingekuwa haimake sense

kwa mawazo yako haya sitaki kukubaliana na wakenya kuwa kenya wako mbele miaka 15 kidemokrasia kuliko tanzania!!!! japo kwa mawazo yako unadhihirisha

ushabiki wa chadema humu fanya, ila kumbuka hatujuani, hoja na ukweli daima viwe kinga ya kulinda utu na akili zetu za kawaida, kusema kila kitu kwa lengo ya kuisifia chadema sio kukijenga!

chadema iangalie ni wapi ilipokosea, mpaka ikakosa kushirikiana na vyama vingine!!

ilikuwa nccr, ikaja cuf na sasa ni chadema historia ni mbaya sana, usishangae next five years chadema hii ikawa sio hii ya leo, kwa mawazo mgando mliyokuwa nayo wa kujiona superior

chama pekee chenye hostoria iliyoleta mabadiliko nchi hii na wengine wanapaswa kujifunza ni CUF-zanzibar, then those can be applaused!

ebu kua kidogo
 
Halima mdee=viti maalum wote wa CCM na CUF + kumi wa kuchaguliwa wa CCM+Ana makinda
Tundu Lisu=jk+sitta+pinda+EL+RA+ wengine sitini
Mnyika=wa kuchaguliwa wote wa CUF+NCCR+UDP+TLP +majimbo waliyoiba kura ya segerea, temeke,kinondoni,ilala na kigamboni

Zitto=jaza mwenyewe
Vicent Nyerere=endelea
Mbowe=acha kabisa

utakuwa ujinga kwa ccm kuwapa watu wanaotoka a small area as pemba kuunda serikali ya upinzani il hali wapo wanaotoka almost all corners of the country. mwaka 2015 hiyo move itatumika kuwaadhibu sana.

toa na mifano wamefanya nini katika jamii kwa kuwaringanisha hivyo? acha ushabiki wewe unafikiri mtu akiwa chadema ndiyo anakuwa malaika?
 
Kura za wabunge kwa wagombea wa nafasi ya Spika zimenifanya nihitimishe kuwa Kama bungeni kunatakiwa kuwa na kambi mbili basi CCM ina wabunge 265 na Upinzani una wabunge 53. Nimefikiri hivyo hasa pale ambapo CCm walikuwa wanaimba CCM! CCM! CCM! wakati Anna Makinda anakwenda kula kiapo. Kwa maoni yangu wapinzani waliopiga kura kwa CCM nao ni CCM tu.

kura hizo zinaweza kuonyesha pia ubovu wa mgombea wa chadema usiangalie upande mmoja tu. huenda wanngeweka mtu mzuri angepata na kura za CCM
 
mh kwa mbinu za sisem watahakikisha wanaisambalatisha chadema vibaya mno. sasa nijukumu ya wabunge wa chadema na wanachama kuwa na msimamo sana kutokudanganyika!

Walijaribu mbinu zote kukisambaratisha wameshindwa. Kilichobaki ni CHADEMA kuwa chama kikuu kwa sasa, na baadaye kuwa chama tawala!!!!!!!!!!!

Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeezzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Slaa ali shine bungeni kutokana na support aliyoipata kwa vyama vingine vya upinzani wakati ule. Sasa hivi wamepata viti kidogo wameshakuwa CHADEMA wapinzani peke yao hehehe
 
Baada ya CUF kuungana na CCM kuunda serikali ya mseto, ni vizuri watanzania wote waelemishwe kuwa chama pekee cha upinzania kilichobaki Tanzania ni Chadema. Kulikuwa na nafasi ya vyama vingine kama TLP, NCCR navyo kuwa vyama vya upinzani. Lakini baada ya TLP, NCCR na vyama vingine kuungana na CUF bungeni inamaanisha kuwa CUF, TLP, NCCR vyote vimeungana na CCM. Hivyo, kama ambavyo tumeendelea kutoa elimu ya uraia kwa watanzania, tuendelee kuwafahamisha na waelewe kuwa chama cha upinzani na ambacho kinatetea masilahi ya Watanzania nchini kwetu ni Chadema pekee. Ujumbe huu na uenee nchi nzima sasa.

Tulishalijua hili siku nyingi, ulikuwa wapi?
 
kura hizo zinaweza kuonyesha pia ubovu wa mgombea wa chadema usiangalie upande mmoja tu. huenda wanngeweka mtu mzuri angepata na kura za CCM

hivi wewe unazo za kukutosha kweli makinda hata robo ya qualification alizonazo marando hanazo think twice!
 
Back
Top Bottom