Bungeni: TLP, CUF, UDP na NCCR Mageuzi navyo vyaungana

CHADEMA kuungana na CUF ni sawa na kuuwa upinzani! Iko wazi CUF ni CCM B, kuna makubaliano ya siri kati yao. Time will tell

kikwete+lipumba+seif+1.jpg
 
sidhani kama cuf wanaweza kuunda upinzani na vyama vidogo sababu jumla ya wabunge wao wote ni 39(cuf 34) nccr 4, na tlp 1 wakati chadema wanawabunge 45!!
 
hao cuf wengi ni wawakirishi wa misikiti bungeni harafu ni lazima tufike mahali tutambue kuwa wameuza utu na
upizani wao kwa shekeli na uroho wa madaraka tu, wengi tumeshuhudia hawa watu wakifanya vikao vyao vya cri na
ccm ikiwa chini mwenyekiti maamuma wa uongozi dunia kikwete ili kuisimilisha nchi kwa manufaa ya cuf na nafsi zao
 
Ni kweli tunahitaji umoja wa upinzani bungeni lakini sio kuungana na mtu kama Mrema ambaye msimamo wake uko wazi.
 
Baada ya chadema, kutangaza kiongozi wao wa kambi ya upinzani bungeni, vyama vingine vinne vimeamua kuungana na kuwa na kiongozi wao huko bungeni vyama hivyo ni TLP, CUF , UDP NA NCCR MAGEUZI

source TBC1( MUKTASARI WA HABARI)

SIWASHANGAI KWANI HAO HAO NDO WALIOWAHI UWANJA WA TAIFA KUMPONGEZA JK KWA KUCHAKACHUA. sidhani kama hawa ni wapinzani na niseme hawa ndiyo wanaochelewesha kuundwa kwa katiba na kuletea kupata tume huru. Cuf huyu mgombea wake amejitokeza kwa mara ya nne huku akijia kuwa hapati hata 10% ya kura. huu ni usaliti na pengine wana maslahi yao na siyo ya wananchi ndiyo maana wanapingana na chadema ili kurudisha nyuma nguvu ya uma.
 
Oya wewe mkenya nini maana watanzania si unawajua ni mabingwa wa kusahau????????????? nakushangaa unalikumbuka hili nadhani ngoja waachiwe huo uwanja waweze kujitutumua vizuri........
WADAU, Tuwache UNAFIKI:

IWE ITAKAVYOKUWA, CUF INAIHITAJI CHADEMA NA CHADEMA INAIHITAJI CUF na wale wanzao.
 
hao cuf wengi ni wawakirishi wa misikiti bungeni harafu ni lazima tufike mahali tutambue kuwa wameuza utu na upizani wao kwa shekeli na uroho wa madaraka tu, wengi tumeshuhudia hawa watu wakifanya vikao vyao vya cri na
ccm ikiwa chini mwenyekiti maamuma wa uongozi dunia kikwete ili kuisimilisha nchi kwa manufaa ya cuf na nafsi zao
nakusikitikia sana hapo na kama ndio misimamo yenu katika upinzani ni hiyo basi, siku zote ccm itaitawala nchi hii:smile-big: fungua macho, piga hesabu, utapata jawabu. Wawindaji huwa hawawindi wasivyoweza kuvila @Obheli
 
Kuna ujanja kwa upande wa CUF kwani chaguzi saba (7) zilizobaki wanaweza kupata viti vinne na vilevile kupata viti viwili vya upendeleo hivyo watakuwa na jumla ya viti 40. Hivyo basi ukiongeza vile vinne vya NCCR, kimoja kimoja cha UDP na TLP basi wao watakuwa na wabunge wengi kuishinda Chadema na hivyo vyama hivyo kuwa na haki ya kuongoza upinzani bungeni. Hili litashindikana tu kama Chadema wataweza kushinda walau viti viwili vya Mpanda na kupata wabunge wengine wawili wa upendeleo. Inabidi Chadema wahakikishe kuwa wanashinda viti hivyo viwili Mpanda na ni lazima wahamasishe watu wao kupiga kura huko.
 
Ndugu zangu kitendo cha Lipumba kumkubali Kikwete wakati wa kutangaza mshindi wa urais inaonesha wazi upande anaoegemea. Hana jipya la kutueleza akae na CCM yake bado Chadema itapeta bila msaada wa CUF
 
Nafikiri jambo jingine ni kuwa kimsingi hili Bunge ni la Tanganyika na wengi wa wabunge wa CUF wameingia kwa muundo huu wa muungano ambao sisi tunaupinga. Wabunge wengi wa CUF wanatoka Pemba na huku bara kama sijakosea wana mbunge mmoja tu. Kwa hiyo utaona kuwa kinachowasumbua ni wivu kwa Chadema kuvuna wabunge wengi bara. Kama katika miaka hii mitano katiba itabadilishwa huenda tusiwe na wingi wa wabunge wa CUF na hapo ndipo kitakuwa kifo cha CUF bara.

CUF kueni wapole, kama kweli ni wapinzani shirikianeni na wenzenu wenye wabunge wengi, tusimame pamoja, tusukume pamoja, pasiwe na Kilimanjaro na Kichuguu. Prove wrong wale wanaosema nyie ni CCM B. TOGETHER WE STAND DIVIDED WE FALL.
 
nashukuru mkuu umeiona point, chadema wanajiona vichwa juu kwa wabunge 45 tu wakati cuf in 34. bunge lililopita chadema walikuwa na 11 na walipewa nafasi ya naibu kiongozi wa pinzani leo cuf in 34 hakupewa hata nafasi ya naibu, eti wamekapa ka-zito, sijui wanakaogopa katavuruga chama? kusema kweli kama chama kinaweza kuvurugwa na kavulana kama zito, basi hakuna chama hapo na nashukuru Mungu hakikushinda uchaguzi. hata kama kura zilichakachuliwa, zitabarikiwa na Mungu, hikichama walahi kingeichakachua nchi nzima kwa ubinafsi. kueni kwanza (watoto wote mnaoishabikia chadema) mtayaona!
HUO NDIO UBINAFSI WA CHADEMA!!:smile-big: wamesahau kuwa CUF, TLP na NCCR bila kuwaunga mkono katika mambo mengi hawana mwendo!:smile-big:

Ninarudia tena; BADO HATUJAWA NA WAPINZANI WA UKWELI TANZANIA.:A S angry:
 
WADAU, Tuwache UNAFIKI:

IWE ITAKAVYOKUWA, CUF INAIHITAJI CHADEMA NA CHADEMA INAIHITAJI CUF na wale wanzao.

hapo ndio unakosea kaka cuf haaihitaji chadema bali ccm! si kuna muafaka wa ccm na cuf?
cuf wangekua wanawahitaji chadema wasingekubali ule upuuzi waliofanya kule zanzibar
kilichofanyika zanzibar ni kuua demokrasia wakati chadema ni chama cha demokrasia
 
Wana JF nimepata habari kuwa CUF imesema haitashirikiana na CHADEMA kuunda serikali ya upinzni ramsi bungeni. Na wanasema wao watashirikiana na vyama vya NCCR Mageuzi na TLP kuunda kambi yao ya upinzani bungeni.

Source: Mlimani TV leo saa 1:30

Hiki nacho ni kituko gani wajamaa!!!! Huu ni wivu ama ni nini? Mimi nafikiri adui wa rafiki yako ni adui yako. Sasa bunge hili linaonekana kuwa kituko, kambi tatu zinazopingana?

Haya wana JF mnasemaje?

CUF wao si Zanzibar tu ndio wana wabunge wengi, mstakabali wa mapambano haya hautegemei kushirikiana na makafiri.
 
CCM poleni sana hamna bahati. CUF sioni wakiwa viongozi wa kambi ya upinzani. Mnategemea CUF wawe vibonde wa kupitisha mambo yenu poleni? You must face the wrath of CHADEMA men and women in the parliament.
 
hoja ya msingi ndugu zanguni ni kwamba cuf inawakilisha wazanzibar walio wachache katika bunge letu haswa ikizingatiwa wazanzibar walijitokeza kwa wingi kupiga kura na sidhani kama kuna mwakilishi aliyepata kura elfu kumi kutoka visiwani hivyo basi washukuru vigezo vya kifisadi vilivyotumika kupata wawakilishi walio wengi nafikiri ufikee wakati wakupata uwiano ulio sawa wa uwakilishi bungeni kwani zanzibar inatumika kupitishia mamluki kuelekea bungeni na kwa kuwa cuf na ccm wanalitambua hilo huitaji kwenda madarasa ya juu kuutambua upinzani halisi ni kutoka chama gani nothing more nothing less chadema ndio real opposition party in tanzania!
 
Naona sasa Chadema tunalewa umaarufu! na ipo hatari kubwa sana kwa chama tukiendekeza fikra kama hizi.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom