Bungeni: Ni kweli maswali ya papo kwa papo au usanii?

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Maswali ya papo kwa papo anayoulizwa waziri mkuu kweli ni papo kwa papo au usanii tu? Nauliza hivyo kwa sababu namuona waziri mkuu anasoma majibu kwenye karatasi hasa maswali anayoulizwa na wabunge wa CCM. Nimemuona akisoma kwenye karatasi majibu kwa maswali aliyoulizwa na Martha Mlata, Mangungu, Mtanda. Maswali kutoka kwa Mbowe(CHADEMA) na Mkosamali(NCCR) hakusoma lakini swali la Mnyaa(CUF) spika kazuia lisijibiwe eti liko very technical.

Je wabunge wa CCM hutakiwa kuwasilisha maswali yao kabla ndiyo maana PM anakuja na majibu? Kama ni hivyo iko wapi essence ya maswali/majibu ya papo kwa papo? Pia Spika kamzuia PM asijibu swali la pili la Mkosamali kuhusu DECI eti lilishajibiwa. Huu ni usanii mtupu!
 
Back
Top Bottom