Mzee Wa Rubisi
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 1,757
- 437
Uwezi kata taji la mti ulilokalia.CCM wanakata taji walilokalia
Yaani bado viongozi wanadhani Watanzania ni wajinga kiasi kwamba hawajui hata wanachokitaka? Inapofikia mpaka mwanafunzi anamtuzi mwalimu wake, then hapo kuna tatizo kubwa.
Wasira kichwa bana, anajua kujenga hoja na ni mzoefu wa mambo. ikumbukwe msuada wenyewe unaingiliwa na siasa sana mpaka wataalam wetu wakiwemo hao maprof. wanatumia utalaam wao kufurahisha kundi fulani la wanasiasa. kwa ufupi Wasira sio anafanya siasa ila anatoa taswira jinsi siasa inavyozidi utaalam na hata wataalam wetu wanatumia siasa kuwasilisha utalaam wao wasipofanya hivyo wanaonekana either waunga mkono serikali au wanafuata beat ya opposition. haya yanafanyika hapa Tanzania tu, vukeni mipaka muone. am out.
Kwa taarifa yako Jaji Werema na Wasira wamewekwa na rafiki yao JK lazima walinde maslahi ya mtu aliye waweka wala si vinginevyo!!!!!!!!!Hawaja fanyiwa vetting kama tunavyotaka katiba mpya iwekwe, kazi ya hawa watu nikulinda maslahi ya mwajiri wao kirafiki period!!!!!!!!!!!!Jaji Werema amewataka wanasheria nchini kuwa wakweli, wasiwapotoshe wananchi, kwanza muswada huo sio muswada wa katiba mpya kama wanasheria wanavyohubiri.
Muswada unaosomwa kwa mara ya pili, ni muswada wa kukusanya maoni jinsi ya kuunda tume ya kukusanya maoni na sio muswada wa katiba mpya.
Yaani bado viongozi wanadhani Watanzania ni wajinga kiasi kwamba hawajui hata wanachokitaka? Inapofikia mpaka mwanafunzi anamtuzi mwalimu wake, then hapo kuna tatizo kubwa.
Wanabodi wenye access na TBC, angalieni TBC Live kipindi cha Jambo Tanzania. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Warema na Waziri Stephen Wasira, wanahojiwa live kuhusu kuwasilishwa Muswada wa Sheria wa Kuundwa Tume ya Kukusanya Maoni ya Kubadilisha Katiba.
aji Werema amewataka wanasheria nchini kuwa wakweli, wasiwapotoshe wananchi, kwanza muswada huo sio muswada wa katiba mpya kama wanasheria wanavyohubiri. Muswada unaosomwa kwa mara ya pili, ni muswada wa kukusanya maoni jinsi ya kuunda tume ya kukusanya maoni na sio muswada wa katiba mpya.
Jaji Werema na Waziri Wasira, wamelishambulia Jukwaa la Katiba na wale wote waliotoa maoni hasi kuhusu kusomwa kwa mara ya pili kwa muswada wakiwataja kwa majina akiwemo Deus Kibamba, Prof. Issa Shivji, Prof. Josephat Kanywanyi na wengine wote wanaopinga muswada huo usiwasilishwe wakiwemo Chama cha Wabasheria Tanzania, TLS, wametajwa kuwa sio wakweli bali wanapinga kwa ushabiki tuu.
Kipindi hicho, kimeongozwa na mtangazaji Elisha Eliya , ambaye ni mmoja wa watangazaji mahiri kabisa wa TBC ambaye sio tuu anakipaji, bali ni kichwa mbaya. Elisha Eliya ameuliza maswali mengi ya msingi Jaji Werema na Waziri Wasira wakitoa majibu ya chenga ya mwili.
Kuhusu kwanini unaitwa Muswada wa Mapitio ya Katiba iliyopo wakati wananchi wanataka katiba mpya?.
Jaji Werema alijibu, katiba ni living document, ikishaundwa, inaishi milele, hivyo hatuwezi kuwa na katiba mpya wakati tayari tunayo katiba iliyopo, hivyo ni lazima kuifanyia mapitio katiba iliyopo na kuiunda upya na kusisitiza katiba itakayopatikana baada ya mapitio hayo, ndio itakuwa ni Katiba Mpya.
Hoja kuhusu mamlaka kubwa ya rais pia yapanguliwa. Jaji Werema amesema, muswada huo unasomwa kwa mara ya pili na maoni bado yanapokelewa hivyo kama wabunge watatoa maoni madaraka ya rais yapunguzwe, serikali itayazingatia maoni hayo ila hailazimishwi kuyakubali naoni yoyote.
Kuhusu kushirijisha maoni ya wadau kwenye huu muswada mpya, wamedai kuwa baada ya kusomwa kwa mara ya kwanza, wameyazingatia maoni ya wadau, hata maoni ya wanajukwaa la katiba pia wameyazingatia, ila hawawezi kutajumuisha kila maoni, hivyo wameyachambua na kuyajumuisha yale walioona yanafaa.
Muda umemalizika, kipindi kimekwisha.
My Take.
1. Kwa vile muswada huo ulipowasilishwa kusomwa kwa mara ya kwanza, ulikataliwa na serikali ika u withdraw, hii inamaanisha muswada husika haukusomwa kwa mara ya kwanza, hivyo kihalali ulitakiwa kusomwa kwa mara ya kwanza.
2. Kwa walisoma sheria UDSM, wanawafahamu walimu magwiji wa mambo ya Katiba. Prof. Shivji, Prof. Kanywanyi na Prof. Fimbo ni miongoni mwao. Kitendo cha Jaji Werema kuwaponda maprofesa hawa na kitampekekea kupata laana kwa 'karma' ya uadilifu wa walimu hawa kumshukia.
Serikali inamtumia Prof. Kabudi kila inapotaka maoni ya wasomi wa sheria. Ilimtumia wakati wa kuzima hoja ya mgombea binafsi, juzi ndio imemtumia kuendesha semina ya wabunge kuhusu mchakato huu.
Pasco.
Update.
Muswada huo, bado haujawasilishwa bungeni mpaka sasa,, serikali imekacha kuuwasilisha leo.
Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba, inayoongozwa na Mhe. Pindi Chana, wameitana kukutana saa hizi, kujadili nini cha kufanya, labda sasa utawasilishwa kesho asubuhi na sio leo.
Wao wanafikiria kuwa tunasema huu ni mswada wa katiba yenyewe mpya. Sijui ni kitu gani kinawafanya wafikirie hatuna uwezo wa kusoma madudu yao.
Wao wanafikiria kuwa tunasema huu ni mswada wa katiba yenyewe mpya. Sijui ni kitu gani kinawafanya wafikirie hatuna uwezo wa kusoma madudu yao.
Serikali na wabunge wa ccm wana madharau ya hali ya juu. Kila siku utawasikia wasima watu walio na mawazo tofauti kuwa 'wametumwa'. Walishaamua siku nyingi kuwa watanzania wengine (except wao) ni wajinga hawana uwezo wa kufikiri. Na hii ndio inawasumbua maana wanafikiri hizi kelele ni za wabunge wachache wa upinzani hivyo wanaona wapambane na hao watu wachache.