BUNGENI: Muswada wa mabadiliko ya katiba

WEREMA AMEFIKIA HATUA YA KUMTUKANA MWALIMU WAKE ILI AMTETEE JK NA MAFISADI WENZAKE ??KWELI MTU HUYU NI HATARI ANAWEZA KUFANYA JAMBO LOLOTE ILIMRADI UBINAFSI WAKE NA MARAFIKI ZAKE UFANIKIWE,HANA AIBU NA WALA STAHA HANA NI MTU HOVYO NA HUONGEA HOVYO KWA UDANGANYIFU WA HALI YA JUU,GEORGE NI JINGA KABISA HATA UKIANGALIA SURA YAKE NI ABNORMAL KWA HIYO SIWEZI MLAUMU SANA ILA WEREMA NI MUONGO NA HANA AIBU ANAWEZAJE KUMTUKANA MWALIMU WAKE KWELIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII MWALIMU ANADHALILISHWA KWA AJILI YA NJAAA ILHALI UKWELI UNAUJUA

ndugu yangu rudi nyuma na ukumbuke ulipokuwa unavaa malapa yaliyotoboka pale mlimani

NJAA MBAYA JAMANI USIMUONE JK KAKAA KIMYA ISSUE ZA CAMEROON ATAIBUKA TUU NA KULEGEZA MAMBO BAADAE

WEREMA KWA HILI UNASTAHILI KUMUOMBA MWALIMU WETU RADHI KWA KUPIGA MAGOTI bungeni
 
Kwakweli madaraka ni kitu cha ajabu sana, mtu asipojaliwa hekima na aliye muumba madaraka humbadirisha ghafla na kujiona anaweza kila kitu na anajua kila jambo, wakati mwingine huweza kumfanya hata akadharau wale walio mfikisha hapo alipo!

Poleni sana wote mlio kwazwa, lakini basi ndugu yangu Were.. tafadhali si kweli kwamba watanzania wooooote hawajui isipo kuwa wewe tu kwa vile tu wewe ni msheria mkuu!
 
jaman sasa wasira anapoelekea inaonekana ana interest binsfs, kwan huyu mzee anaelimu gan hasa mpaka kubishana na wataalum?
 
Nimekumbuka kauli ya gwijij mmoja mwanamapinduzi comrade Mao tse tung, aliwahi kusema namnuku; 'Vita na vurugu ni muendelezo wa Siasa, pale siasa inaposhindikana, basi vita na vurugu huibuka ili kutatua yale matatizo yaliyo shindikana kisiasa.' Mh JK unayo mamlaka ya kuzuia hilo lisitokee, achana na wapambe nuksi! Usikubaliane nao kwa njaa zao, huko wanakotusukuma sana tuelekee! Hao mkuu hata ukiwaangalia usoni kweli haimo ndani yao na wanakusaliti wewe na Watz tu! Basi nakuomba tafakari na uchukue hatua kwa kukataa pumba zao!
 
Kuhusu kwanini unaitwa Muswada wa Mapitio ya Katiba iliyopo wakati wananchi wanataka katiba mpya?.

Jaji Werema alijibu, katiba ni living document, ikishaundwa, inaishi milele, hivyo hatuwezi kuwa na katiba mpya wakati tayari tunayo katiba iliyopo, hivyo ni lazima kuifanyia mapitio katiba iliyopo na kuiunda upya na kusisitiza katiba itakayopatikana baada ya mapitio hayo, ndio itakuwa ni Katiba Mpya.
Wasira kichwa bana, anajua kujenga hoja na ni mzoefu wa mambo. ikumbukwe msuada wenyewe unaingiliwa na siasa sana mpaka wataalam wetu wakiwemo hao maprof. wanatumia utalaam wao kufurahisha kundi fulani la wanasiasa. kwa ufupi Wasira sio anafanya siasa ila anatoa taswira jinsi siasa inavyozidi utaalam na hata wataalam wetu wanatumia siasa kuwasilisha utalaam wao wasipofanya hivyo wanaonekana either waunga mkono serikali au wanafuata beat ya opposition. haya yanafanyika hapa Tanzania tu, vukeni mipaka muone. am out.
 
Kipindi hicho, kimeongozwa na mtangazaji Elisha Eliya , ambaye ni mmoja wa watangazaji mahiri kabisa wa TBC ambaye sio tuu anakipaji, bali ni kichwa mbaya. Elisha Eliya ameuliza maswali mengi ya msingi Jaji Werema na Waziri Wasira wakitoa majibu ya chenga ya mwili.
Kanjanja tu huyu hamna kichwa hapo. Kwanza huwezi kufanya majadaliano na watu wa upande mmoja ambao mtazamo wao unafanana..pili kama mwandishi wa habari unatakiwa uwe neutral na uelewe vizuri mada unayoiongoza. Mwisho unapopewa jibu ambalo halina mashiko unatakiwa uulize kupata ufafanuzi zaidi kwa faida ya watazamaji/wasikilizaji. Wananchi wanachopinga ni huo mswada ambao una mpango na utaratibu utakaotumika kwa ajili ya kukusanya maoni na hatimaye kuandika Katiba mpya. Na hapa ndio Elisha kama ni makini na kichwa alitakiwa awabane hawa wanasiasa (Kombani, Werema, na Wasira) watoe ufafanuzi. Lakini alikuwa akipewa majibu rejareja anenda kwenye swali lingine..hili ni tatizo ambalo liko kwa wanahabari wengi sana bongo, hawajui kuuliza maswali, kuongoza mijadala na kutoa taarifa zenya kukosoa serikali waziwazi. Mfano mzuri wa hivi karibuni ni juzi Mboe alivooengea bungeni kuhusu wabunge kudai posho na matumizi ya anasa kwa watumishi waandamizi serikalini. Hakuna kituo cha TV kilichoripoti au kujadili hoja hiyo, utasikia tu enzi hizo na miaka 50 bada ya uhuru, tumethubutu…..malizia. Wanahabari wetu wengi ni vilaza, njaa kali, si wazalendo na waoga.
 
inasikitisha sana mtu kuwa mwanasiasa anajifanya yeye ni kila kitu, mbona tunao wabunge waganga wa kienyeji, darasa la saba kama kile kibajaji na vikaragosi kama wasira. wanasiasa acheni ujinga wa kujifanya mnajua kila kitu. Kwa taarifa wassira hupaswi kujilinganisha na prof SHIVJI kwa jinsi jamii inavyomuheshimu. unatia kichefuchefu
Humji Wasira wewe! may be unamuona kwenye tv. that man is very vigilant and Aggressive. anza kumfuatilia sasa you might come with something. ushauri tu.
 
Kikwete akiendelea kusikiliza hawa watu wake Werema na wassira shauri yake, lazima asome kuwa kikulacho kinguoni mwako wengine wanataka kumharibia tu, kwani wakishalikoroga si wassira wala Werema atakayekuwepo mzigo wote utahamia kwa kikwete, inabidi awe mbayuwayu
 
Hata fedha ikipatikana watu hawatengenezi au hawaifanyi miradi inavyotakiwa sababu ya kutaka cha juu kila kona, matokeo yake ndo kurudia rudia kufanya vitu vile vile kwa kutumia watu wale wale. Hapo ndo nachoka na viongozi wetu, sijui huwa hawajionei wanapofanya safari za nje tena mara kwa mara. Wanadhani walifika hapo wenzao kwa porojo na kutegemea misaada bila mikakati ya maana.

Ni Jambo La Kusikitisha Kwenye Hii Nchi Kila Kitu Kinafanyika Bora Liende!! Hela Nyingi za Ujenzi wa Miundombinu Kupitia TAMISEMI ni kama zinapotea Kwani Hakuna Ubora na Udhibiti wa Kitu Chochote!! Hadi Machozi Yananitoka!!

Angalia barabara nyingi chini ya Halmashauri zinatia Hasira Kama sio Kinyaa Kwa gharama ileile!! Ya TZS 1,000,000,000 KWA Kilometer!! Kama barabara iliyojengwa Juzi Kutoka Kijitonyama kwenda Mwananyamala Hapa Kati!! Just Miezi Miwili Barabara full Mashimo!!

Wanajua sisi walipakodi Hatuna Uchungu na Kodi Zetu?
 
Yaani hizi ni zaidi ya sarakasi!!! Hawa akina Werema na wasira wanataka ku achiev kitu gani? Tutafika kweli kwa hali hii?
 
nina wasiwasi kama anawasikiliza, inaelekea kila mtu akiamka anaamua la kwake na ndio maana kila siku nasikia serikiari ikitoa taarifa zinazotofautiana kwenye kipindi kisichozidi masaa 24!
Kikwete akiendelea kusikiliza hawa watu wake Werema na wassira shauri yake, lazima asome kuwa kikulacho kinguoni mwako wengine wanataka kumharibia tu, kwani wakishalikoroga si wassira wala Werema atakayekuwepo mzigo wote utahamia kwa kikwete, inabidi awe mbayuwayu
 
Mimi nina wasiwasi mkubwa sana kama kweli Werema ni mwanasheria kwa sababu wakati anapoulizwa mambo yanayohusu sheria huwa anajibu hovyo hovyo tu. Eti mwanasheria mkuu wa serikali. Bogus
 
hao Tbc mbona wameita watu wa ccm tu? kwanini hawakumuita waziri kivuli wa sheria Mhe. Lissu? mi naona hicho kipindi kiliandaliwa mahsusi kwa ajili ya kujaribu kujisafisha na kuwadanganya wananchi wasio na uelewa wa kile kinachoendelea, naomba ule mkakati wa wanaharakati kuandaa maandamano nchi nzima uanze kufanyiwa kazi maana hawa vilaza watapitisha tu huu mswada, LAZIMA TUFANYE KITU TENA SASA, vinginevyo hii nchi itazama kama ile meli waliyoizamisha kwa uzembe ya Mv Spiceislander...
 
Tumeshaamua, wakijidai kuusoma kwa mara ya pili - maandamano nchi nzima.
Wanapaswa waelewe kuwa serikali ili-withdraw muswada, hivyo hakuna muswada uliosomwa mara ya kwanza.
 
MAPUNGUFU YA MUSWADA
Interpretation sect 3
-Constitutional organs means the president, the constituent assembly or the national assembly.
Lakini the president ni nani? – not defined
constituent assembly ni kitu gani – not defined
the national assembly.ni kitu gani – not defined
Bila kueleza vitu hivi mjanja yeyote anaweza kuchomeka chombo chochote, mfano bunge kuwa ndilo constituent assembly!

Ni muhimu pia kudefine president ni nani kwani tutaona huko mbele alivyopewa madaraka makubwa Kwa mfano isemwe tu kwamba the president means the president of the Tanzania
Part III
Hapa tunaona madaraka makubwa ya president juu ya hii commission
Sec 5 The presideny may,………….establish a commission to examine……
Hapa kuna tatizo moja kubwa kisheria; neno ‘may' halimlazimishi huyo president kufanya hivyo tofauti na kama ingetumika neno ‘shall'. Halafu ile comma imewekwa baada ya may ndiyo sababu ya kusema kuwa hiyo may inahusu ku-establish hiyo commission. Kama comma ingewekwa kabla ya may, basi ingehusu consultations with the president of Zanzibar.
Kwa hiyo president ndiye anaanzisha hii commission
Sec 6 (1) President ndiye atateua wajumbe wote wa hiyo commission
Sec 6 (2) ni vigezo vya kuchagua wajumbe, hapa vimetajwa vigezo (criteria), lakini kigezo (e) president amepewa madaraka ya kuamua vigezo vingine vyovyote atavyoona vinafaa – bila masharti yoyote wala kuulizwa na yeyote!
Sec 6(3) kinawaondoa baadhi ya watu kuwa wajumbe wa commission
Sec 6(3) (a)…a councilor or a leader of a political party. Yaani viongozi wa vyama vya siasa hawawezi kuchaguliwa kuwa wajumbe. Lakini huyu president (kama ndiye president of Tanzania) ni kiongozi wa chama cha siasa. Ina maana kiongozi wa chama kimoja cha siasa amepewa mamlaka makubwa ambayo viongozi wenzake wa vyama vingine vya siasa wamenyimwa! Kwa hiyo ataweka mbele maslahi ya chama chake (Labda hapa ndipo inakuja shida ya kuwa na president ambaye ni sehemu ya executive)

Sec 8 (1) The terms of reference shall be issued by the president….president huyo huyo ndiye ataipa hiyo commission hadidu za rejea yaani ataiambia nini cha kufanya! Na kwenye ya sec 8(3) hayo atakayowambia kufanya yanapewa nguvu ya kisheria. Maana yake president atatunga sheria yeye mwenyewe!
Ukisoma sec 9(1) (c) utaona kuwa hii commission ndiyo itaandika katiba ya awali. Je si ni wazi kuwa katiba hiyo itaandikwa kwa matakwa ya aliyewateua na kuwapa majukumu?
Kifungu cha 9 (2) kimeifunga mikono commission juu ya (a) muungano wa Tanganyika na Zanzibar na (c) urais. Je kama wananchi wanataka muungano wa kuwa nchi na serikali moja, maoni hayo yatashughulikiwa na nani? Je kama wanataka muungano uvunjike kila nchi ijitawale kivyake – maoni hayo yatachukuliwa na nani?
Kuhusu urais, watu wana mapendekezo ya kutaka rais asiwe sehemu ya serikali – wasemee wapi?

Sec 13 Commission itakuwa na secretariat ambayo katibu wake atateuliwa na president!
Sec 16 Commssion itapeleka ripoti yake kwa president ambaye atampatia nakala rais wa Zanzibar.
President atamuagiza waziri wa sheria na katiba kupeleka constitutional bill kwenye constituent assembly ambayo kama nilivyosema hapo awali haikuwa defined.
Sasa madaraka zaidi yanayokaribia labda ya kimungu yapo kwenye hiyo constituet assembly. Nimeona niscan hizo sections:


Kwa hiyo madaraka yote juu ya hiyo assembly yapo kwa president hadi kutangaza majina ya wajumbe aliowachagua kwenye gazeti; Hiyo ni sec 21.
Sec 22 (1) madaraka ya hiyo assembly hayajali kuwapo kwa madaraka kama hayo kwa bunge.
Yaani hapa president amepewa madaraka ya kuteua chombo na wajumbe wake chenye kutumia madaraka yake notwithstanding kwamba madaraka kama hayo yapo kwa bunge!
Madudu yasiyokubalika yako mengi. Labda nimalizie kwa keleza kuwa kifungu cha 26 kinaipatia tume ta uchaguzi kuendesha kura ya maoni. Ni tume hii hii inayolalamikiwa kuwa siyo huru. Na swali litakaloulizwa ni la kujibu ndiyo au hapana.
Kifungu cha 28(2) kinasema kuwa kampeni ya kura ya maoni itaendeshwa na commission, Ni hiyo hiyo iliyoteuliwa president, ni commission hiyo hiyo iliyodraft katiba, halafu ni hiyo hiyo peke yake inapiga kampeni! Vyama vya siasa havitaruhusiwa kuendesha kampeni, na mtu yeyoye atakayekampeni ambaye siyo mwana-commission atahukiwa kifungo bila faini.
NAFASI YA MWANANCHI AMBAYE NDIYE ANATAKIWA AAMUE NCHI YAKE ITAKAVYOENDESHWA, AMEACHWA NA KUTOA MAONI (SI MAAMUZI) NA MWISHO KUHUBIRIWA SEMA NDIYO! Ni vigumu kwa commssion kukampeni kuwa hiyo katiba iliyoandikwa na wao wenyewe ikataliwe!
Je hayo ndiyo tuliyolilia?
UKIFUATA BARABARA ISIYO SAWA HUWEZI KUFIKA KULE UNAKOKUSUDIA KUFIKA.
MUSWADA HUU NI BARABARA ISIYO SAWA!
 
hivi hawa watu wanafikiria hatujui tunachopinga ni nini? Tunachopinga ndicho hicho kinachowasilishwa. Tunapinga mpango na utaratibu ambao umewekwa kwa ajili ya kukusanya maoni na hatimaye kuandika Katiba mpya. Hakuna mtu mwenye akili timamu anayefikiria huu mswada ni mswada wa Katiba mpya. Tunaelewa kuwa ni mswada ambao una lengo la kuweka utaratibu wa hatimaye kufikia Katiba mpya, unaweka vyombo, taratibu na sheria ya kufikia Katiba Mpya. Na hicho ndicho tunachokipinga. Tunakipinga kwa sababu kubwa mbili.

a. Rais amechukua madaraka ya wananchi kuandika Katiba yao
b. Utaratibu mzima utasimamiwa na CCM na wajumbe wengi wa CCM na jhivyo kufanya Katiba mpya kuwa ni Katiba ya CCM.

Hili lina ugumu gani wa kulielewa?

Si kwamba hawajui wanachokifanya no wanajua ila wanjua pia hicho ndo kitanzi chao; wameteka madaraka yetu na hawako tayari kuyaona yanarudi mikononi mwetu. Wanaogopa kuishi maisha yatakayowafanya wawe wawajibikaji na kushindana kwa uwezo badala ya nepotism kwasababu wengi wao hawakuwahi ishi hayo maisha. Ni watu waliopewa majukumu makubwa tangu ujana wao na kwakuwa wakati huo wengi hawakuwa na uelewa mkubwa ilikuwa rahisi kuwapeleka wanavyotaka bila kuulizwa maswali hata kama wahusika walikuwa wanatendewa ndivyo sivyo. Sasa kwakuwa wanaona hatari ya wao kuto weza kushindana pamoja na kizazi chao kilichojaa deko basi inabidi wang'ang'anie madaraka kwa nguvu zao zote.

Kinachonishangaza ni hao wapambe wao ambao wanajua kabisa hili likitokea kizazi chao hakitakaa kipate fursa sawa za kulitumikia taifa lao; ni kipi kinawapa motisha wakutumiwa kama dodoki?
 
Tumeshaamua, wakijidai kuusoma kwa mara ya pili - maandamano nchi nzima.
Wanapaswa waelewe kuwa serikali ili-withdraw muswada, hivyo hakuna muswada uliosomwa mara ya kwanza.

Na mimi na yasubiri haya maandamano muhimu kwa maisha yangu na ya kizazi changu kwa hamu kubwa ...Grrrrrrrrrrrrrrrrrr how can this people play with us like we are kindergaten children?
 
Yaani hizi ni zaidi ya sarakasi!!! Hawa akina Werema na wasira wanataka ku achiev kitu gani? Tutafika kweli kwa hali hii?

Mwanawane hujui hao ndugu zetu wa mkoa huo kwa ubishi! wasiiiraa na wereeemaaa kwao bangi na mboga walikula utotoni!
 
Back
Top Bottom