Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,598
Hadi sasa huu muswada ni wa kurekebisha katiba na sio kwa kutunga katiba mpya. Kwa Werema kuutetea ni sawa kabisa maana tangu hapo awali alisema waziwazi kuwa katiba ya sasa haina shida kama kuna jambo la kurekebisha basi watu waseme na litarekebishwa. Maneno haya ya Werema pia yalisemwa na Celina Kombani.
Kwa hiyo Serikali ya ccm haina nia ya kuandika katiba mpya - that's very obvious. Kama walikuwa na nia ya kuandika katiba mpya kwa nini hawataki kusikiliza maoni ya wananchi? Ni kitu gani kinawafanya watake kusoma huu muswada kwa mara ya pili? Ni ni lini muswada wa KUTUNGA katiba mpya uliwahi kupelekwa bungeni? Ule mwingine ulipelekwa tena kwa lugha ya kiingereza ulikuwa wa KUREKEBISHA katiba.
Naye Steven Wasira na utaalam gani kwenye mambo ya katiba kiasi kwamba ccm wanamtumia kuhubiri huu muswada uliojaa matatizo? Kwa nini watu kama Wasira na Werema wanajiona wanajua mambo ya katiba kuliko Prof Shivji? Shida kubwa ninayoona ni kwamba kuna gap kubwa sana kati ya ccm na wananchi. Wakishapata Ubunge hawa ccm ni kama wanajigeuza baraza la mawaziri tena mawaziri wasiosikiliza wale wanaowaongoza. Huu muswada unaweza kuipeleka kuzima ccm mapema kuliko ilivyokuwa iwe.
Ningeomba kuuliza, Spika wa bunge ana uwezo/nguvu gani katika hali kama hii ambapo serikali inaonekana waziwazi kwenda kinyume na public interest?
Spika yupi unayemwongelea??? Sijui kama kuna mtu anayeitwa Spika sasa anayeweza walau kuhoji maelekezo ya serikali!!
Tusubiri tuone....!