BUNGENI: Muswada wa mabadiliko ya katiba

Jaji Werema na Waziri Wasira, wamelishambulia Jukwaa la Katiba na wale wote waliotoa maoni hasi kuhusu kusomwa kwa mara ya pili kwa muswada wakiwataja kwa majina akiwemo Deus Kibamba, Prof. Issa Shivji, Prof. Josephat Kanywanyi na wengine wote wanaopinga muswada huo usiwasilishwe wakiwemo Chama cha Wabasheria Tanzania, TLS, wametajwa kuwa sio wakweli bali wanapinga kwa ushabiki tuu.
Ushabiki kwa nani! Mtu akikosa cha kujitetea!
 
Hivi kweli Prof. Shivji na Kanywanyi hawajui muswada huu unahusu nini? au Werema na huyo Tayson wameamua kuwaponda hadharani wanataaluma hao?
 
Kuhusu kushirijisha maoni ya wadau kwenye huu muswada mpya, wamedai kuwa baada ya kusomwa kwa mara ya kwanza, wameyazingatia maoni ya wadau, hata maoni ya wanajukwaa la katiba pia wameyazingatia, ila hawawezi kutajumuisha kila maoni, hivyo wameyachambua na kuyajumuisha yale walioona yanafaa.
Muda umemalizika, kipindi kimekwisha.
Wao wana uwezo gani wa kuweza kuyakubali mengine eti ndiyo yanayofaa na maoni mengine wameyaacha eti wameona hayafai. Wao ni nani Vilaza wakubwa hawa!
 
My Take.
1. Kwa vile muswada huo ulipowasilishwa kusomwa kwa mara ya kwanza, ulikataliwa na serikali ika u withdraw, hii inamaanisha muswada husika haukusomwa kwa mara ya kwanza, hivyo kihalali ulitakiwa kusomwa kwa mara ya kwanza.
2. Kwa walisoma sheria UDSM, wanawafahamu walimu magwiji wa mambo ya Katiba. Prof. Shivji, Prof. Kanywanyi na Prof. Fimbo ni miongoni mwao. Kitendo cha Jaji Werema kuwaponda maprofesa hawa na kitampekekea kupata laana kwa 'karma' ya uadilifu wa walimu hawa kumshukia.

Serikali inamtumia Prof. Kabudi kila inapotaka maoni ya wasomi wa sheria. Ilimtumia wakati wa kuzima hoja ya mgombea binafsi, juzi ndio imemtumia kuendesha semina ya wabunge kuhusu mchakato huu.

Baada ya dakika chache kutoka sasa, muswada unatinga mezani kwa spika.
 
Hadi sasa huu muswada ni wa kurekebisha katiba na sio kwa kutunga katiba mpya. Kwa Werema kuutetea ni sawa kabisa maana tangu hapo awali alisema waziwazi kuwa katiba ya sasa haina shida kama kuna jambo la kurekebisha basi watu waseme na litarekebishwa. Maneno haya ya Werema pia yalisemwa na Celina Kombani.

Kwa hiyo Serikali ya ccm haina nia ya kuandika katiba mpya - that's very obvious. Kama walikuwa na nia ya kuandika katiba mpya kwa nini hawataki kusikiliza maoni ya wananchi? Ni kitu gani kinawafanya watake kusoma huu muswada kwa mara ya pili? Ni ni lini muswada wa KUTUNGA katiba mpya uliwahi kupelekwa bungeni? Ule mwingine ulipelekwa tena kwa lugha ya kiingereza ulikuwa wa KUREKEBISHA katiba.

Naye Steven Wasira na utaalam gani kwenye mambo ya katiba kiasi kwamba ccm wanamtumia kuhubiri huu muswada uliojaa matatizo? Kwa nini watu kama Wasira na Werema wanajiona wanajua mambo ya katiba kuliko Prof Shivji? Shida kubwa ninayoona ni kwamba kuna gap kubwa sana kati ya ccm na wananchi. Wakishapata Ubunge hawa ccm ni kama wanajigeuza baraza la mawaziri tena mawaziri wasiosikiliza wale wanaowaongoza. Huu muswada unaweza kuipeleka kuzima ccm mapema kuliko ilivyokuwa iwe.

Ningeomba kuuliza, Spika wa bunge ana uwezo/nguvu gani katika hali kama hii ambapo serikali inaonekana waziwazi kwenda kinyume na public interest?
 
Jaji Werema na Waziri Wasira, wamelishambulia Jukwaa la Katiba na wale wote waliotoa maoni hasi kuhusu kusomwa kwa mara ya pili kwa muswada wakiwataja kwa majina akiwemo Deus Kibamba, Prof. Issa Shivji, Prof. Josephat Kanywanyi na wengine wote wanaopinga muswada huo usiwasilishwe wakiwemo Chama cha Wabasheria Tanzania, TLS, wametajwa kuwa sio wakweli bali wanapinga kwa ushabiki tuu.
wadau nijuvyeni, kuteuliwa kuwa mwanasheria mkuu je, maana yake we unajua sheria kuliko watu wote kwenye nchi? haiwezekani ukawa masaburi tu na ukateuliwa kwa kuwa unatumia zaidi hayo masaburi kwenye kutafsiri sheria? wadau nifahamisheni,
 
Hivi kweli Prof. Shivji na Kanywanyi hawajui muswada huu unahusu nini? au Werema na huyo Tayson wameamua kuwaponda hadharani wanataaluma hao?

Sina shaka lolote kuwa watapewa jibu soon!

Ulevi wa madaraka ni hatari kuliko AK-47!!!
 
Back
Top Bottom