BUNGENI: Muswada wa mabadiliko ya katiba

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,551
Wanabodi wenye access na TBC, angalieni TBC Live kipindi cha Jambo Tanzania. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Warema na Waziri Stephen Wasira, wanahojiwa live kuhusu kuwasilishwa Muswada wa Sheria wa Kuundwa Tume ya Kukusanya Maoni ya Kubadilisha Katiba.
aji Werema amewataka wanasheria nchini kuwa wakweli, wasiwapotoshe wananchi, kwanza muswada huo sio muswada wa katiba mpya kama wanasheria wanavyohubiri. Muswada unaosomwa kwa mara ya pili, ni muswada wa kukusanya maoni jinsi ya kuunda tume ya kukusanya maoni na sio muswada wa katiba mpya.

Jaji Werema na Waziri Wasira, wamelishambulia Jukwaa la Katiba na wale wote waliotoa maoni hasi kuhusu kusomwa kwa mara ya pili kwa muswada wakiwataja kwa majina akiwemo Deus Kibamba, Prof. Issa Shivji, Prof. Josephat Kanywanyi na wengine wote wanaopinga muswada huo usiwasilishwe wakiwemo Chama cha Wabasheria Tanzania, TLS, wametajwa kuwa sio wakweli bali wanapinga kwa ushabiki tuu.

Kipindi hicho, kimeongozwa na mtangazaji Elisha Eliya , ambaye ni mmoja wa watangazaji mahiri kabisa wa TBC ambaye sio tuu anakipaji, bali ni kichwa mbaya. Elisha Eliya ameuliza maswali mengi ya msingi Jaji Werema na Waziri Wasira wakitoa majibu ya chenga ya mwili.

uhusu kwanini unaitwa Muswada wa Mapitio ya Katiba iliyopo wakati wananchi wanataka katiba mpya?.
Jaji Werema alijibu, katiba ni living document, ikishaundwa, inaishi milele, hivyo hatuwezi kuwa na katiba mpya wakati tayari tunayo katiba iliyopo, hivyo ni lazima kuifanyia mapitio katiba iliyopo na kuiunda upya na kusisitiza katiba itakayopatikana baada ya mapitio hayo, ndio itakuwa ni Katiba Mpya.

Hoja kuhusu mamlaka kubwa ya rais pia yapanguliwa. Jaji Werema amesema, muswada huo unasomwa kwa mara ya pili na maoni bado yanapokelewa hivyo kama wabunge watatoa maoni madaraka ya rais yapunguzwe, serikali itayazingatia maoni hayo ila hailazimishwi kuyakubali naoni yoyote.

Kuhusu kushirijisha maoni ya wadau kwenye huu muswada mpya, wamedai kuwa baada ya kusomwa kwa mara ya kwanza, wameyazingatia maoni ya wadau, hata maoni ya wanajukwaa la katiba pia wameyazingatia, ila hawawezi kutajumuisha kila maoni, hivyo wameyachambua na kuyajumuisha yale walioona yanafaa.
Muda umemalizika, kipindi kimekwisha.

My Take.
1. Kwa vile muswada huo ulipowasilishwa kusomwa kwa mara ya kwanza, ulikataliwa na serikali ika u withdraw, hii inamaanisha muswada husika haukusomwa kwa mara ya kwanza, hivyo kihalali ulitakiwa kusomwa kwa mara ya kwanza.
2. Kwa walisoma sheria UDSM, wanawafahamu walimu magwiji wa mambo ya Katiba. Prof. Shivji, Prof. Kanywanyi na Prof. Fimbo ni miongoni mwao. Kitendo cha Jaji Werema kuwaponda maprofesa hawa na kitampekekea kupata laana kwa 'karma' ya uadilifu wa walimu hawa kumshukia.

Serikali inamtumia Prof. Kabudi kila inapotaka maoni ya wasomi wa sheria. Ilimtumia wakati wa kuzima hoja ya mgombea binafsi, juzi ndio imemtumia kuendesha semina ya wabunge kuhusu mchakato huu.

Pasco.

Update.1

Muswada huo, bado haujawasilishwa bungeni mpaka sasa,, serikali imekacha kuuwasilisha leo.
Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba, inayoongozwa na Mhe. Pindi Chana, wameitana kukutana saa hizi, kujadili nini cha kufanya, labda sasa utawasilishwa kesho asubuhi na sio leo.

Update. 2
Muswada uliwasilishwa jana jioni na majadiliano yanaendelea.
 
Jaji Werema amewataka wanasheria nchini kuwa wakweli, wasiwapotoshe wananchi, kwanza muswada huo sio muswada wa katiba mpya kama wanasheria wanavyohubiri.

Muswada unaosomwa kwa mara ya pili, ni muswada wa kukusanya maoni jinsi ya kuunda tume ya kukusanya maoni na sio muswada wa katiba mpya.
 
Jaji Werema na Waziri Wasira, wamelishambulia Jukwaa la Katiba na wale wote waliotoa maoni hasi kuhusu kusomwa kwa mara ya pili kwa muswada wakiwataja kwa majina akiwemo Deus Kibamba, Prof. Issa Shivji, Prof. Josephat Kanywanyi na wengine wote wanaopinga muswada huo usiwasilishwe wakiwemo Chama cha Wabasheria Tanzania, TLS, wametajwa kuwa sio wakweli bali wanapinga kwa ushabiki tuu.
 
Kipindi hicho, kimeongozwa na mtangazaji Elisha Eliya , ambaye ni mmoja wa watangazaji mahiri kabisa wa TBC ambaye sio tuu anakipaji, bali ni kichwa mbaya.

Elisha Eliya ameuliza maswali mengi ya msingi Jaji Werema na Waziri Wasira wakitoa majibu ya chenga ya mwili.
 
Jaji Werema na Waziri Wasira, wamelishambulia Jukwaa la Katiba na wale wote waliotoa maoni hasi kuhusu kusomwa kwa mara ya pili kwa muswada wakiwataja kwa majina akiwemo Deus Kibamba, Prof. Issa Shivji, Prof. Josephat Kanywanyi na wengine wote wanaopinga muswada huo usiwasilishwe wakiwemo Chama cha Wabasheria Tanzania, TLS, wametajwa kuwa sio wakweli bali wanapinga kwa ushabiki tuu.

wote twajua kuwa ule sio muswada wa katiba bali ni utaratibu kuusu tume ya kukusanya maoni na uundwaji wake. tatizo ni mamlaka kubwa aliyopewa raisi kuhusu huu muswada. watz tunataka urudishwe kwetu wananchi tuujadili. mjadala ni mpya usomwe mara ya kwanza. period.
 
Jaji Werema na Waziri Wasira, wamelishambulia Jukwaa la Katiba na wale wote waliotoa maoni hasi kuhusu kusomwa kwa mara ya pili kwa muswada wakiwataja kwa majina akiwemo Deus Kibamba, Prof. Issa Shivji, Prof. Josephat Kanywanyi na wengine wote wanaopinga muswada huo usiwasilishwe wakiwemo Chama cha Wabasheria Tanzania, TLS, wametajwa kuwa sio wakweli bali wanapinga kwa ushabiki tuu.

Tatizo wasira kujiona mwanasiasa anaona anajua kila kitu kuliko wataalamu kumbe hajui kitu, UNAJUA KILA MTU ANAWEZA KUWA MWANASIASA ILA SI KILA MTU ANAWEZA KUWA MTAALAMU KWA ELIMU, hapa wasira anajiona kuwa anauwezo wa kuwapinga wataalamu kwa jinsi anavyojua kwa kujua yeye ni mwanasiasa.
 
Kuhusu kwanini unaitwa Muswada wa Mapitio ya Katiba iliyopo wakati wananchi wanataka katiba mpya?.

Jaji Werema alijibu, katiba ni living document, ikishaundwa, inaishi milele, hivyo hatuwezi kuwa na katiba mpya wakati tayari tunayo katiba iliyopo, hivyo ni lazima kuifanyia mapitio katiba iliyopo na kuiunda upya na kusisitiza katiba itakayopatikana baada ya mapitio hayo, ndio itakuwa ni Katiba Mpya.
 
Hoja kuhusu mamlaka kubwa ya rais pia yapanguliwa. Jaji Werema amesema, muswada huo unasomwa kwa mara ya pili na maoni bado yanapokelewa hivyo kama wabunge watatoa maoni madaraka ya rais yapunguzwe, serikali itayazingatia maoni hayo ila hailazimishwi kuyakubali naoni yoyote.
 
Jaji Werema na Waziri Wasira, wamelishambulia Jukwaa la Katiba na wale wote waliotoa maoni hasi kuhusu kusomwa kwa mara ya pili kwa muswada wakiwataja kwa majina akiwemo Deus Kibamba, Prof. Issa Shivji, Prof. Josephat Kanywanyi na wengine wote wanaopinga muswada huo usiwasilishwe wakiwemo Chama cha Wabasheria Tanzania, TLS, wametajwa kuwa sio wakweli bali wanapinga kwa ushabiki tuu.
Werema asipotoshe akili zake na ubushani usio na maana. Kama alimsikiliza ProfKanywani, haya yote yanatokea si kwa kuwa watanzania wana kiu kubwa sana ya katiba, bali wanataka mabadiliko katika maisha yao. Hii katiba, ndiyo ni muhimu sana lakini kwa wengi ni kama fursa ya kutoa hisia zao. Watu wamepigika. Kwa miaka 50, wakati wengine wakiwa hawana uhakika wa maisha yao, kuna watu, humuhumu nchini, wanaogelea katika utajiri wa kutisha.
Hivyo, Werema afumbue macho na aangalie zaidi ya katiba.

hata huo muswada, uwe wa katiba au wa kukusanya maoni, kinachotakiwa ni kuwashirikisha wananchi kwenye uandaaji wake. Ni kwa nini wananchi wasishirikiswe kwa maopana eti kwa sababu si muswada wa katiba?
 
bora wache ya zamani kuliko kusema wamerekebisha katiba huku mchakato wake umeendeshwa kihuni huni tu.
 
hivi hawa watu wanafikiria hatujui tunachopinga ni nini? Tunachopinga ndicho hicho kinachowasilishwa. Tunapinga mpango na utaratibu ambao umewekwa kwa ajili ya kukusanya maoni na hatimaye kuandika Katiba mpya. Hakuna mtu mwenye akili timamu anayefikiria huu mswada ni mswada wa Katiba mpya. Tunaelewa kuwa ni mswada ambao una lengo la kuweka utaratibu wa hatimaye kufikia Katiba mpya, unaweka vyombo, taratibu na sheria ya kufikia Katiba Mpya. Na hicho ndicho tunachokipinga. Tunakipinga kwa sababu kubwa mbili.

a. Rais amechukua madaraka ya wananchi kuandika Katiba yao
b. Utaratibu mzima utasimamiwa na CCM na wajumbe wengi wa CCM na jhivyo kufanya Katiba mpya kuwa ni Katiba ya CCM.

Hili lina ugumu gani wa kulielewa?
 
Kuhusu kushirijisha maoni ya wadau kwenye huu muswada mpya, wamedai kuwa baada ya kusomwa kwa mara ya kwanza, wameyazingatia maoni ya wadau, hata maoni ya wanajukwaa la katiba pia wameyazingatia, ila hawawezi kutajumuisha kila maoni, hivyo wameyachambua na kuyajumuisha yale walioona yanafaa.
Muda umemalizika, kipindi kimekwisha.
 
Tatizo wasira kujiona mwanasiasa anaona anajua kila kitu kuliko wataalamu kumbe hajui kitu, UNAJUA KILA MTU ANAWEZA KUWA MWANASIASA ILA SI KILA MTU ANAWEZA KUWA MTAALAMU KWA ELIMU, hapa wasira anajiona kuwa anauwezo wa kuwapinga wataalamu kwa jinsi anavyojua kwa kujua yeye ni mwanasiasa.
kaka hapo penye blue mbona umetushusha hadhi sana sisi wanasiasa?
 
Kuhusu kwanini unaitwa Muswada wa Mapitio ya Katiba iliyopo wakati wananchi wanataka katiba mpya?.

Jaji Werema alijibu, katiba ni living document, ikishaundwa, inaishi milele, hivyo hatuwezi kuwa na katiba mpya wakati tayari tunayo katiba iliyopo, hivyo ni lazima kuifanyia mapitio katiba iliyopo na kuiunda upya na kusisitiza katiba itakayopatikana baada ya mapitio hayo, ndio itakuwa ni Katiba Mpya.
ccm haina nia ya kuunda katiba mpya, na dio maana kwenye ilani yao ya uchaguzi hakukuwa hata na mstari mmoja unaotamka katiba mpya. kwa hiyo msishanage haya ya werema.
 
Back
Top Bottom