Bungeni: Muswada wa Katiba Unajadiliwa!

Kombo, unajichosha kumjibu huyo jamaa, huwa anaushabiki wa kimagamba.
Wewe ndiyo unaeleta ushabiki. Ungetoa tofauti kati ya meneja wa breweries na DED.
Hawa watu hawana uhusiano wowote na mambo ya siasa. Msiingize watu wenye vyeo ambavyo ni non-union kwenye mchakato wa katiba ya jamhuri ya muungano. Wewe ndiye unayeleta ushabiki.
 
@ Kibona. Nakubaliana nawe kwamba CCM sasa haina wanasiasa ambao wanaweza kujadili hoja kwa mtazamo mpana. Ukiangalia ubishi wa ama wawe maDC ama maDED utagundua unafiki wa kijinga wa wabunge wa CCM. Wanaona wanamkomoa Kikwete na CDM wakati wanawakomoa Watanzania kwa kuendeleza mijala isiyo na tija kwa walipa kodi zinazowahudumia.
Kweli mkuu wameshikilia sana wakuu wa wilaya kwa sababu kuu mbili: kwanza hawa ndio alama ya nguvu za rais hivyo ni rahisi kwao kuchakachua mchakato, pili wanajaribu kuficha aibu ili wasionekane hawajui kitu chochote ndani ya muswada wakati kimsingi hawajui kweli. Kuthibitisha kuwa hawajui angalia michango yao, ishu ya DCs ilisemwa na mchangiaji wa ccm wa kwanza sasa wachangiaji wote wa ccm wameacha kuendelea kupinga vipengele vingine ili waulinde mswada walioupitisha awali wao wameufanya mjadala uwe ni maDC na maDED. Kwa mtu aliyewahi kushiriki midahalo anajua kuwa silaha kubwa ya mtu aliye shallow ni kung'ang'ania point moja mpaka mdahalo uishe.
 
Kweli mkuu wameshikilia sana wakuu wa wilaya kwa sababu kuu mbili: kwanza hawa ndio alama ya nguvu za rais hivyo ni rahisi kwao kuchakachua mchakato, pili wanajaribu kuficha aibu ili wasionekane hawajui kitu chochote ndani ya muswada wakati kimsingi hawajui kweli. Kuthibitisha kuwa hawajui angalia michango yao, ishu ya DCs ilisemwa na mchangiaji wa ccm wa kwanza sasa wachangiaji wote wa ccm wameacha kuendelea kupinga vipengele vingine ili waulinde mswada walioupitisha awali wao wameufanya mjadala uwe ni maDC na maDED. Kwa mtu aliyewahi kushiriki midahalo anajua kuwa silaha kubwa ya mtu aliye shallow ni kung'ang'ania point moja mpaka mdahalo uishe.
Vipi kuhusu Zanzibar?
 
Kweli mkuu wameshikilia sana wakuu wa wilaya kwa sababu kuu mbili: kwanza hawa ndio alama ya nguvu za rais hivyo ni rahisi kwao kuchakachua mchakato, pili wanajaribu kuficha aibu ili wasionekane hawajui kitu chochote ndani ya muswada wakati kimsingi hawajui kweli. Kuthibitisha kuwa hawajui angalia michango yao, ishu ya DCs ilisemwa na mchangiaji wa ccm wa kwanza sasa wachangiaji wote wa ccm wameacha kuendelea kupinga vipengele vingine ili waulinde mswada walioupitisha awali wao wameufanya mjadala uwe ni maDC na maDED. Kwa mtu aliyewahi kushiriki midahalo anajua kuwa silaha kubwa ya mtu aliye shallow ni kung'ang'ania point moja mpaka mdahalo uishe.
u're right mkuu.
 
Mwaka 1984 Jaji Mkuu, Francis Nyalali alifikia kikomo cha uvumilivu kwa jinsi nchi inaendeshwa huku sheria na haki zikipuuzwa. Kwa mfano wakati huo askari na mahakama ambazo hazitambuliwi na katiba na sheria au katiba zilishika hatamu wakiitwa kwa jina “Sungusungu”.

Nyalali alivyoona hivyo hakutaka kubishana na Nyerere. Alimfuata Msasani akamuambia kwamba anataka ku-resign kwa sababu mambo yanaendeshwa bila kufuata sheria hivyo yeye kama Jaji Mkuu, mhimili wake hauna kazi ya kufanya.

Nyerere akaongea naye kwa kirefu na siku hiyo kulikuwa kumebaki siku kadhaa Halmashauri ya CCM (NEC) ilikuwa inafanyika. Nyerere akamuambia atamkaribisha ili aeleze hali hiyo kwenye NEC. Siku ya NEC ikafika. Nyalali akajieleza ile mbele ya NEC ila hakusema alitaka kujiuzuru maana hiyo ikawa ni siri yake na Nyerere.

Nyalali alipomaliza maelezo, alipomaliza akawaacha NEC na Nyerere waendelee na ajenda zingine yeye akarudi kwenye kazi zake za Ujaji Mkuu.

Sijui kilijadiliwa nini huko nyuma baada ya kuondoka Nyalali, lakini inaelekea kulikuwa na ulazima wa kumutia tena Nyalali katika kikao kingine kinachofuata cha NEC. Kwenye masimulizi yake mwenyewe Nyalali yaliyochapishwa kwenye RAI mwishoni mwa 1990s na kurudiwa baada ya kifo chake, Nyalali anasema kwamba aliamua hii mara ya pili asiende peke yake, bali akaita majaji wengine wawili wakamsaidie kutoa ufafanuzi wa jinsi gani kila mtu anavyotakiwa kuishi kwa kuongozwa na sheria na si vinginevyo. Maana alihisi kwenye kikao cha kwanza zilijitokeza dalili za wajumbe kutokumuelewa.

Siku ikafika, Nyalali akatinga na majaji wenzake kwenye NEC. Nyerere akafungua kikao na kina Nyalali wakaaza kufafanua kwamba kila mtu hapa nchini anatakiwa kuishi kwa kufuata ssheria yaani hakuna aliye juu ya sheria. Walipomaliza ikaja zamu ya wajumbe wa NEC kutoa maoni yao.

Kabla sijasema walisema nini tujikumbushe kwamba wakati huo na hata sasa NEC ilikuwa na watu kadhaa ambao professional lawyers. NEC ilikuwa ngazi ya kupatia vyeo kama uwaziri kama ilivyo sasa. Hivyo, NEC ilikuwa imesheheni wanasheria na wanahistoria ambao kwenye proeffesssion zao wanajua wazi kwamba kila mtu hata Rais lazima aishi kwa kufuata sheria.

Sasa, tuone wajumbe wa NEC wakiwemo hwa wanasheria wali-react vipi kulingana na maelezo ya Nyalali na wenzake. Wajumbe wengi waliwashambulia vibaya sana Nyalali na wenzake. Walioongoza mashambulizi si watu mbumbumbu, bali ni wasomi wazuri wa sheria. Mmoja alidiriki kusema hivi “Sasa mnakuja hapa kutuambia kuwa kila mtu anatakiwa kuwa chini ya sheria, je, kwa maana hiyo hata Rais Nyerere mnataka atawaliwe na sheria??!!”

Wakati ule kulikuwa bado kuna Preventive Detention Act yaani rais alikuwa amepewa uwezo wa kumtia mtu kizuizini. Hivyo, palepale wajumbe kadhaa wakaleta hoja wakimuomba Nyerere kwamba huyu Nyalali na wenzake wawekwe kizuizini.

Nyerere aliacha uwanja mpana na akahakikisha wote wametoa dukuduku lao. Kikubwa ni kwamba Asilimia kubwa ya NEC hawakukubaliana na anachosema Nyalali na wenzake. Lakini wajumbe hawakujua kuwa Nyerere ndiye aliyemzuia Nyalali kujiuzuru na ukumbuke hiyo ni miaka mitano baada ya Edwin Mtei kujiuzuru kwa kutofautiana na Nyerere kwa mambo mengine. Si sheria bali uchumi.

Je, baada ya wote kusema , unadhani hadi hapa Nyerere alikuja na jibu gani? Nyerere alifunga mjadala kwa njia ambayo wajumbe hawakuamni na wakaaibika.
Alifunga mjadala kwa jibu fupi sana kwa kusema “Ndugu wajumbe, kuanzia sasa kila binadamu nchini Tanzana hatakuwa juu ya sheria, kila mtua atakuwa chini ya sheria na tunalazimika kuongozwa na sheria”

Nyalali anasema alifarijika na ndilo jibu lililomfanya afute wazo la kujiuzuru na aendelee kuwa Jaji Mkuu hadi alipostaafu. Ila anasema, hakuamini macho na masikio ndani ya NEC kuona wajumbe waliochachamaa ni wale ambao ni wasomi wazuri wa sheria lakini wanahoji kwa nini wanasiasa, mawaziri na rais wawe chini ya sheria.

Nyalali anasema, wasomi hao walikuwa wanasaliti taaluma yao kwa kujipendekeza kwa Nyerere bila aibu lakini wakaumbuliwa na jibu la Nyerere.

Sasa, tuje kwenye Muswada huu wa Katiba. Tuliona CHADEMA wakitoka nje kwa sababu ya ubovu wake. Lakini wabunge wa CCM wakaushangilia na kuuona safi. BInafsi nilimshuhudia Mh. Angelah Kairuki akijadili kana kwamba si mwanasheria wakati hadi sasa yuko Sabatic Leave kama State Attorney.

CHADEMA wakaona waende kumuona Rais Kikwete kama Nyalali alvyoenda kumuona Rais Nyerere. Nyerere akaona kweli hali ya Chama kushika hatamu na viongozi kuwa juu ya sheria ni upuuzi mtupu. Tumeona Nyerere alivyoitisha NEC kujadili hoja ya Nyalali. Wajumbe wa NEC badala ya kujadili hoja wakaanza kumjadili na kumkebehi Nyalali mbele ye Nyerere wakidhani kwa kufanya hivyo wanamfutahisa Nyerere.

Haina tofauti na wabunge wa CCM ambao waliutetea Muswada mbovu wakidhani wanamfurahisha Kikwete, sasa Kikwete kaamua kuleta marekebsho. Kuletwa kwa marekebisho maana yake wabunge wa CCM wameumbuka kama walivyoumbuka wale wajumbe wa NEC,

Hadi hapa nimemaliza maelezo yanakuja maoni yangu. Aoni yangu ni kwamba mazoea ya kuishi kwa kujipendekeza kwa bosi yoyote kujikubali kwamba wewe mwenyewe ni dhaifu.
Siamini kama wabunge wa CCM waliosoma Sheria kama wangepelekewa Muswada ule kwenye University Exam wangekuja na majibu ovyo kama waliyokuwa wanayatoa bungeni siku wanaupitisha. Hili ndilo lilikuwa kosa lao kama lilivyokuwa NEC members against Nyalali.

Walichofanya CHADEMA kwenda Ikulu wala hakikuwa kigumu kwa msomi yoyote. Hata Ridhiwani Kikwete ambaye ni mwanasheria kwa taaluma yake angejibu sawa na CHADEMA walivyotaka maana CHADEMA walisimama kwenye profession base na hapo hakuna Rais yoyote wa dunia hii angewakatalia hoja yao, achilia mbali.

Sasa, kuna mawazo kwamba wabunge wa CCM wanaona aibu kwamba wenzao CHADEMA ni vipanga. Ukweli ni kwamba haya wameyataka wenyewe kwani ni ukweli kwamba wamo baadhi yao ni lecturers wa profession mbalimbali ikiwemo sheria na sidhani kama hili walishindwa kuliona.

Hivyo, zama za kufanya siasa za kuukwepa ukweli zimepitwa. CCM au chama chochote wakiukwepw ukweli basi CHADEMA watautumia ukweli huo na jamii itawaheshimu kuwa ni wasomi na wataumbuka.

Jadili

Thanks! Nikupataje?
 
Chadema wamefunga goli kwa kupiga kanzu bugeni na kupiga tobo kwa JK.Aibu yao au aibu yetu?????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????
 
Mkuu Nikupateje,maelezo yako hapo juu nimerudia zaidi ya mara nne kuyasoma,wewe kweli ni Great Thinker. Hata mimi naamini sasa Kikwete anajua ni akina nani wanamwambia ukweli na nani wanajipendekeza.
 
Wakuu wa WIlaya wenyewe ni kama akina NAPE NYAUYE-DC MASASI....KAda wa CCM na Mkuu wa wilaya, je kutakuwa na usawa kweli hapo?
 
Back
Top Bottom