Bungeni: Muswada wa katiba mpya wasomwa

Maswi

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
932
211
MSWADA unasomwa kwa mara ya 2, angalia TBC1, spika anatetea mswada kusomwa kwa mara ya 2.

Kazi ipo
Wanabodi, hatimaye Muswada wa Kukusanya Maoni kuhusu Mabadiliko ya Katiba watinga rasmi bungeni na kusomwa kwa mara ya pili!.

Muswada huo umewasilishwa kikao hiki cha jioni. Spika wa Bunge, Mhe. Anna Makinda alianza kwa kuitetea serikali kwa nguvu zake zote japo sauti yake ilikuwa ikitetemeka.

Sasa Waziri wa Sheria, Mhe. Celina Kombani ndio anausoma na kutetea uwasilishaji wa muswada huo kwa mara ya pili.

Nadhani ninavyomsikiliza Mama Kombani, kwa maoni yangu binafsi kama Pasco wa jf, nadhani anajikanyaga kanyaga tuu, kwani ulipowasilishwa kwa mara ya kwanza, si ulikataliwa?!.

Hebu na tusubiri jinsi wanasheria, watakavyomchana Mama Kombani!.
 
...Spika Anne Makinda ameanza kufanya kazi za serikali pale alipoanza kutoa maelezo ya awali kabla ya mswada wa kubadilisha katiba unaosomwa mara ya pili leo...akatoa vitisho ili wabungw wasiukatae amesema wakiugomea ina maana hakuna katiba mpya na hii itazuia kuendelea kwa michalato mingine ya katiba.Amesema wale wanaowaambia watanzania waandamane wanaleta majungu yasiyo na maana.Na amesema huu mswada ni safi na hauna tatizo.

My take:
Huyu mama anafanya kazi za magamba na mafisadi waziwazi angalieni TBC1 muda huu...huyu Anne vp wakuu?
 
Spika Anna makinda amelinanga jukwa la katiba kwa madai kuwa limewapotosha wananchi jana katika mjadala wao wa katiba. sasa waziri wa sheria na katiba Celine Kombani anasoma muswaada kwa mara ya pili na kisha kujadiliwa.
 
asema ulikuwa kwenye stage ya kusomwa kwa mala ya kwanza sasa hivi inasomwa kwa mala ya pili.kamuita mtoa hoja asome mswada wake.anayesoma ni wazili wa sheri mh.selina kombani.Mia
 
Wanabodi, hatimaye Muswada wa Kukusanya Maoni kuhusu Mabadiliko ya Katiba watinga rasmi bungeni na kusomwa kwa mara ya pili!.

Muswada huo umewasilishwa kikao hiki cha jioni. Spika wa Bunge, Mhe. Anna Makinda alianza kwa kuitetea serikali kwa nguvu zake zote japo sauti yake ilikuwa ikitetemeka.

Sasa Waziri wa Sheria, Mhe. Celina Kombani ndio anausoma na kutetea uwasilishaji wa muswada huo kwa mara ya pili.

Nadhani ninavyomsikiliza Mama Kombani, kwa maoni yangu binafsi kama Pasco wa jf, nadhani anajikanyaga kanyaga tuu, kwani ulipowasilishwa kwa mara ya kwanza, si ulikataliwa?!.

Hebu na tusubiri jinsi wanasheria, watakavyomchana Mama Kombani!.
 
Adai ulishasomwa kwa mara ya kwanza mwezi April hivyo sasa unapaswa kusomwa kwa mara ya pili na kuendelea na hatua nyingine. asema ni muswada wa kuunda tume tu sio muswaada wa kukusanya maoni ya katiba mpya
 
Kombani anawataka wenye katiba na kanuni za bunge wazitumie kufuatilia maelezo yake, anatolea ufafanuzi namna miswada inavyowasilishwa bungeni, hapa anaonekana kuwajibu wanajukwaa la katiba juu ya kusomwa kwa mara ya kwanza au ya pili
 
Wakuu,mswada wa katiba umesomwa mara pili,hivi serikali ya magamba ni kiziwi au? mbona aifanyii kazi maoni ya wananchi! nawakilisha
 
Nimemwona Bi Kiroboto (Spika) akiutetea kwa nguvu ila bila hoja. Hoja kubwa ni kuwa mswada huu unamfanya Rais kuwa alpha na Omega wa mchakato wote.
Waziri mhusika anasoma hotuba huku anatetemeka utafikiri amelazimishwa. Wangojee nguvu ya umma
 
Ama kweli nimejua serikali ya CCM ina dharau na kiburi! Hajali watanzania wanachotaka wanachojali ni maslahi yao. Je kuwanyima watanzania kutoa maoni yao ni kwa maslahi ya nani? woga huu waserikali hii unamaana gani?
 
ilitakiwa wabunge kwenda jimboni kutafuta maoni kwa wananchi, wakati mswada wenyewe ulikuwa kwa lugha ya MR cammeroon.
 
Kama kawaida yake nyuma ya magamba. tusubili wachangiaji watasema nini kuhusu hilo
 
Mpo tayari kwa maandamano wakameroon wameonyesha dalili zoote za kuupitisha
 
Back
Top Bottom