Bungeni Live: Naibu spika akataa hoja ya Lissu kuzungumzia kuzama kwa meli

Kwakweli inasikitisha sana jinsi mwanasheria mkuu wa serikali na waziri Lukuvi na viongozi dhaifu wa bunge wanavyoshirikiana kuzima hoja pale bungeni. Leo hii tena Lukuvi na mwanasheria mkuu wametumia uzaifu wa naibu spika kuzima hoja ya mh. Lisu aliyoitoa ili kujadili swala la ajali ya meli.Wabunge wengi hasa wa upinzani walijitahidi kumshauri naibu spika ili hoja hiyo ijadiliwe lakini naibu spika kwa makusudi na kwa kupindisha kanuni alikataa hoja hiyo ya mh.Lisu.Ni kama spika alivyokataa hoja ya mh.Hamad Rashidi juzi.Hii ni hatari kwa taifa kwani hili bunge sasa liko kuilinda serikali na si kutete wananchi. Hata hivyo wabunge wengi wa upinzani walitoka nje ya bunge. Binafsi inaniuma sana na najiuliza huyu Lukuvi na mwanasheria mkuu wa serikali kama kweli ni watanzania na wana uchungu na watu wa chii hii. Mungu atalipa kwa dhuluma hii.Inauma sana hasa kama unafuatilia mambo haya bungeni. Viongozi wa leo ni janga kwa taifa.
Ni kweli inauma sana tena sana ila jambo moja ni wazi hakuna marefu yasiyokuwa na ncha na zaidi ya hilo What goes around comes around.
 
Kazi ya AG ni kutoa ufafanuzi au mwongozo wa kisheria na au wa kanuni za bunge pale ambapo panahitajika. Bwana Werema(namwita bwana kwa kuwa hana hadhi ya kuwa Jaji- he aint impartial) imekuwa kawaida yake kupiga vijembe,kutoa mafumbo na ngonjera. Mbaya zaidi vijembe hivyo vinaelekezwa kwa wapinzani. Kwani yeye ni AG wa CCM? Mfano Kazi ya kichwa ni kufuga nywele....... hii inatoa mwongozo gani au ufanunuzi gani wa kisheria au kanuni za bunge? This is an example of Judge gone rogue

Mi kaniudhi sana pale alipotusi afu ndugai nalo eti akakazia "huo ndo ukweli"
 
Unafiki tu wa Tundu Kissu sasa anataka wajadili nini kama sio kuweka siasa tu! Tatizo la Tundu anatumia kichwa kufugia nywere!
 
lissu anatisha nyie chunguzeni anaposimama kutoa hoja,kuomba taarifa au mwongozo,UTAMUONA LUKUVI,MKURYA WA KUPANIC,NDUGAI NA WABUNGE WENGI WANAKUWA STANDBY,PAMOJA NA KUUMA MENO,WAKISUBIRI KUSIKIA KWA MAKINI,TUACHE USHABIKI WA KISIASA HUYU JAMAA ANATISHA,NDO MAANA HATA MR DHAIFU ALIVYOKWENDA KWENYE KAMPENI IRAMBA MASHARIKI ALISEMA NI BORA WAMNYIME YEYE KURA LAKINI WASIMPE TUNDU LISSU.HAMJIULIZI WHY?TUNGEKUWA NA VICHWA 6 VYA NAMNA HII NCHI INGESONGA MBELE JAMAA ANATISHA,MI NAFIKIRI ANAWEZA KUWA MBADALA WA DK SLAA 2020.
 
Back
Top Bottom