Bungeni Live: June 28, 2012

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Habari toka jikoni zinasema kuwa Waziri wa afya bwana Hussein Mwinyi kutoa kauli ambayo ina ujumbe huu.

Wote watakao Goma kufukuzwa kazi kuanzia leo na wataweka daftari la kujiandikisha na kusaini.

Viongozi wote wa migomo kusimamishwa kazi na ikiwezekana kufutwa kazi na ikiwezekana kunyang'wanywa leseni.

Kutofanya shughuri yoyote katika maeneo ya hospitali.

Watakao kubali kufanya kazi kulindwa na askari.

UPDATES

Dodoma Interns 11 watimuliwa katika mafunzo ya vitendo kwa sababu ya mgomo
Katika kipinda cha maswali kwa waziri mkuu. Pinda amesema kuwa hawatarajii kutoa tamko leo. Anasema bado wanaruhusu majadiliano na madaktari lakini kwa hatua za dharura wanafikiria mpango wa kuwarudisha madaktari wastaafu kazini na kuwachukua wote ambao wapo wizara ya Afya.
Leo katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni Mh Lissu amemtaka Waziri mkuu ajipime na aone kama kweli anastahili kuendelea na nafasi yake ya uwaziri mkuu ama lah.

Hii imekuja baada ya Lissu kumwuliza mbona ahadi zake alizotoa juu ya sakata la madaktari kushindwa kuzitimiza?
Waziri mkuu akajibu kwamba ameshafanya the best kupambana na na swala hilo.

Mhe Lissu akamwambia kama ndiyo umeshafanya the best na bado Madaktari wameanza mgomo huoni ni wakati muafaka wa wewe kujiudhuru.

Mwishowe Waziri mkuu akatetewa na Madam Speaker.
Mh.Shymar Kweygir amwaga machozi Bungeni kuwalilia walemavu wenzie wa ngozi kwa kuuliwa na watuhumiwa kutokamatwa ili hali tembo aliyeuwawa porini watuhumiwa wamepatikana.
 
huwezi lazimisha ng'ombe kunywa maji ilhali umempeleka mtoni.
 
Mmmmmmmmmm
Hivi chanzo cha kugoma ni nini???
Mtoto kagoma kwenda shule wewe unapgaaaaa''mmmmmmmmhhhhhh

T.I.T (This Is Tanzania)
 
kabla wabunge hawajaongelea kugoma wamepandishiwa mishahara kwa ajili ya kununua kura 2015 hadi m.10,yani madaktari kutaka walipwe milioni 3 imekuwa nongwa hadi mnataka kuwaua kwa kipigo..mtajificha wapi siku ukombozi ukiwadia?
 
Iko wapi utawala wa kidemokrasia unaojali haki na utu wa mwananchi?
Wanajeshi wetu mnayaona haya?
 
Kunyang'anywa leseni ya kufanya kazi hawana jeuri hiyo. Mwenye uwezo wa kumnyang'anya leseni ya kufanya kazi ni chama chao cha Medical Association of Tanganyika. Hata hiyo MAT ni mpaka uende kinyume na maadili ya udaktari ndio wanaweza kukunyang'anya leseni. Serikali inaweza tuu kumfukuza kazi ila bado leseni yake anayo na anaweza kuendelea kupractice popote.
 
Ni dakika chache zimebaki kwa Pinda kutekeleza maamzi dhaifu juu mgomo wa madaktari, ni siku itakayogubikwa majonzi na simanzi kwa watanzania na kauli ya serikali itageuza mjadala wa wabunge kuijadili bajeti ya ofisi ya waziri mkuu ilowasilishwa Jtatu kwa kuanza kujadili maamzi ya serikali, wabunge wengi watapandwa na jazba kwani miongozo itatawala leo huku wapinzani wakionekana ni wachochezi. Nawasilisha.
 
Kunyang'anywa leseni ya kufanya kazi hawana jeuri hiyo. Mwenye uwezo wa kumnyang'anya leseni ya kufanya kazi ni chama chao cha Medical Association of Tanganyika. Hata hiyo MAT ni mpaka uende kinyume na maadili ya udaktari ndio wanaweza kukunyang'anya leseni. Serikali inaweza tuu kumfukuza kazi ila bado leseni yake anayo na anaweza kuendelea kupractice popote.

tatizo wanafikiria kutumia njia ya mkato kumaliza tatizo wakati walitakiwa kukaa na kujadili yapi yanatekelezeka na yapi yanaweza kusubiri ,... dr's nao ni binadamu wataelewa tu
 
Bungeni sasa, baada ya kuulizwa na KUB hakuna kauli ya serikali leo, wamesoma upepo mbaya!
 
kutoka bungeni pinda ametoa salam na tamko la serikali kwa dk,ulimboka na mgomo wa madaktari, na amesema serikali haina tamko la zaidi!
 
Back
Top Bottom