Wana JF nimekuwa nasikiliza taarifa ya habari ya CLOUDS FM saa 12 jioni nikasikia kwamba Spika Anna Makinda ameteua kamati ya wabunge watakaofanya uchunguzi wa tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge. Moja ya jina nililolisikia kwenye kamati hiyo ni Gozibert Blandes Mbunge wa Karagwe, Nilijiuliza kama bunge limekosa watu wasio na doa kuwapo kwenye kamati ya uchunguzi.
Huyu bwana kwanza si mbunge harali, alitangazwa mshindi mbele ya mtutu wa bunduki, askari walitumwa toka Bukoba mjini kwenda karagwe kuwatisha wananchi waliokuwa wanasubiri matokeo ya uchaguzi. Alisindikizwa na askari mpaka airport Bukoba na sasa hivi hawezi kukanyaga huko wananchi wana hasira naye. Sasa mtu kama huyu anatoa wapi moral authority ya kwenda kuwahoji watuhumiwa wakati yeye ni mtuhumiwa wa vote rigging?
Nawakilisha.