wewe utakuwa mfanyakazi wa tanesco au ulitumia yale mambo ya undugunaizesheniKwa hili la Tanesco sikubaliani na kiwia kuwa hawana walilofanya. Tanesco ya miaka iliyopita siyo hii ya leo nafikiri bado baadhi ya watu wamebaki na historia, Tanesco ya sasa inafanya kazi zake kwa mpangilio unaoeleweka, sikutarajia hata siku moja kuwa nitakuja kuwasha umeme wa Tanesco ila nataka nikuhakikishie kuwa nilipofanya mchakato wa ufuatiliaji nilishangaa jinsi Tanesco walivyokuwa wanafanya shughuli zao kwa uhakika kiasi cha mtu kama mimi kupata huduma hiyo bila kutoa chochote ndani ya week tatu toka nilipe kiasi cha pesa kilichohitajika, awali nilikuwa natumia jenereta, kwa siku tatu petrol ya sh.10,000/= sasa hivi hiyo elfu kumi napata uniti kama sikosei zaidi ya hamsini ambapo nazitumia kwa zaidi ya week tatu au mwezi kabisa, sasa jamani ni kweli hawajafikia hicho kiwango kinachotakiwa ila kwa sasa wanajitahidi tuwatie moyo matatizo mengine yako nje kabisa ya uwezo wa Tanesco.