Bungeni: CHADEMA yawavuruga wabunge, jazba zatawala na muswada wa katiba mpya haujadiliki

MAGEUZI KWELI

JF-Expert Member
Jul 16, 2011
1,947
253
Naona anaongea tuuuu na kumfanya Nyerere kama Mungu aliyekuwa Tanzania na ambaye hakuwa na neno au baya lolote kwa Taifa hili.

Anatumia kigezo gani kumsafisha Nyerere milelle kwamba hakuwa na baya lolote ndani ya utawala wake kwa taifa la Tanzania???

Nahisi kukereka na hili Gamba Pevu kwa porojo zisizo na mwelekeo.

Nawakilisha
 
nimemsikiliza ole sendeka, ndugulile na hamad, kwa kweli muda wote wanaponda tu hoja za upinzani na hakuna cha maana wanachochangia.

Kwa kweli mjadala wa namna hii ni kupoteza muda.
 
Namsikia rage mwizi wa FAT anabwabwaja tu, yaani badala ya kujadili mswaada wao ni chadema,bungeni leo ni wanaijadili chadema,hii ni ajabu na kweli,badala ya kujadili vifungu vilivyomo kwenye mswaada wao wamekomaa na chadema, chadema.kila anayesimama ni anaunga mkono.ni upuuzi tu.
 
natamani hata hilo bunge lihairishwe sasa hivi tu kupunguza gharama za uendeshaji na kodi za watanzania , badala ya kujadili vifufungu wao wanaweka upupu wao.
 
Bunge la leo ni ovyo, hawajadili kitu zaidi kujibu hoja za Lissu!
 
Namsikia rage mwizi wa FAT anabwabwaja tu, yaani badala ya kujadili mswaada wao ni chadema,bungeni leo ni wanaijadili chadema,hii ni ajabu na kweli,badala ya kujadili vifungu vilivyomo kwenye mswaada wao wamekomaa na chadema, chadema.kila anayesimama ni anaunga mkono.ni upuuzi tu.

Hivi huyu Rage ana CV gani vile?? maana mimi namkumbuka tu kwenye mambo ya mpira kama katibu wa Simba, FAT Ilala then Taifa then Lupango (Jela)!!!

kuna ki mbunge kinaongea ss hivi kinabwabwaja tuuu! aisee tunaongozwa na VILAZA mnooooo! waache wajiliwaza mjengoni wakitoka duniani watatukuta barabarani!
 
Mh Ole Sendaka adai ni mara ya kwanza kwake kumuona m2 eti anaejiita mwana sheria akipotosha watz.
Mh Sendeka amemtaka Tundu lisu aache kumdhihaki muasisi wa taifa hili Mw Nyerere,
Mh Sendeka amemnukuu Mh lisu akidai kwamba''Uhifadhi wa haki za binadamu ulikataliwa na serikali ya Mw Nyerere miaka yote ya utawala wake''.
Mh Sendeka Alimtaka Lisu arudi katika katiba akasome tena Ibara zifuatazo-12 hadi 24.
 
Masaburi, Ole Sendeka alipata zero form four, we know
 
At the end amesema nini,maana 1 and 2 ni personal observation, 3 is a fact, bill of rights zimekuja mwaka 1985 if not wrong na tukapewa muda kuweka nyumba sawa na 4 ni maombi yake kwa lisu vifungu ambavyo sina shaka Lissu anavijua.

Yeye ( sendeka) anasema nini?????
 
Ole Sendeka ndio anatakiwa aache kudhihaki watanzania. Watanzania wana akili timamu na utashi wa kujua jema na zuri. Kitendo cha kusema Lissu anapotosha watanzania ni madharau ya hali ya juu kwa watanzania.
 
Nani amemtuma Sendeka kwamba Lissu ananipotosha mimi mwananchi? Sendeka, mimi nina akili, nina macho, nina masikio, nina nusa nin mdomo kama wewe. usinisemee kama sijakutuma. Nilitaka unihusishe katika kuandaa mchakato wa jinsi ya kuandika Katiba mpya lakini hujanishirikisha. Anapotokea mtu kutoa tahadhari kuwa sikushirikshwa wewe unamwambia ananipotosha! Kulikoni! Tundu Lissu, nipo pamoja nawe, waambie mswaada huo usipite bila kuhakikisha kuwa ninashirikishwa.
 
Safi sana. Kwani kwa namna hiyo wanakiongezea umaarufu CHADEMA. Sasa kila mtu hadi vijijini watakua interested kujua zaidi juu ya CHADEMA.
Hakika CHADEMA kimecheza kama Pele.
 
Sendeka anadhani akitumia jina la Nyerere tutamwona mkweli

Uwongo ni uwongo na ukweli ni ukweli

Big up Tundu!
 
Back
Top Bottom