Nikupateje
JF-Expert Member
- Dec 22, 2009
- 1,334
- 988
Dakika tano zilizopita Mh. John Mnyika aliinuka kutoa hoja aungwe mkono na bunge zima. Hoja yenyewe ilikuwa ni kuhusu jambo linalohusu mamlaka ya bunge kwamba liweke ukomo kupewa taarifa ile ya David Jairo.
Mh. Mnyika aliuliza kwanza kutokana na swali lake Alhamis iliyopita kwa Waziri Mkuu aliyejibu kwamba taarifa ya suala lile ni kweli imechelewa kufika lakini itakuja bungeni wakati wowote kuanzia sasa.
Lakini Mnyika akiwa ameshika gazeti la JAMBO LEO la jana amelisoma likisema REPORT YA JAIRO IKO KWA SPIKA NA IMEOZEA PALE. BUNGE LACHAMBULIWA KAMA KARANGA.
Hivyo, Mnyika akataka kujua ukweli ni upi. Je, Pinda alikuwa muongo aliposemakuwa ripoti haijafika bungeni. Je, kama JAMBO LEO wako sahihi je, kwa nini uongozi wa bunge usichukuliwe hatua na bunge kwa si kwa kuitoa tu, bali kuiacha hadi iozee ofisini kwa spika? J,e huko kuozea kwa Spika ni kwa sababu bunge limechambuliwa kama karanga?
Hivyo, kutokana na mkanganyiko huo, Mnyika alitaka kuungwa mkono hoja ili bunge liweke deadline kuwa tipoti hiyo ifike siku fulani itakayotajwa kuliko kuwa na ambiguity kama inayojitokeza.
Anne Makinda aliinuka na kusema kwamba hoja hiyo haikubali kwa sababu Bunge halifanyi kazi na magazeti ambayo mara nyingi huandika habari za uongo.
MY TAKE:
Jibu hili la Spika, limenipa nguvu ya kuandika headline kwamba CCM yaliumbua JAMBO LEO. Ingekuwa umbuko hilo limetolewa na upinzani JAMBO LEO lisingejali sana, lakini kwa sababu limetolewa na kuumbuliwa na mwana-CCM yaani Anne Makinda na wengine weng mle walioko upande wa kulia wakashangilia basi alhamdulilah.