Bunge: Tunaendelea kupitia utetezi wa Zitto

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,781
5,205
[h=2][/h]




Zittospeak%282%29.jpg

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe




Ofisi ya Bunge imesema bado inaendelea kulifanyia kazi utetezi uliowasilishwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, (Chadema), la kudai Baraza la Mawaziri lilirubuniwa ili kuliua Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC).
Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel, alisema jana kuwa ofisi hiyo inaendelea kulifanyia kazi ushahidi uliowasilishwa na Zitto baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Katika sakata hilo, Juni 23 wakati Bunge lilipokuwa likijadili Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2011, ambapo Zitto alipinga kauli ya Serikali iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo aliyesema Serikali imeamua kuhamisha kazi zilizokuwa zikifanywa na CHC zifanywe na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Zitto alisema kipengele cha kuhamisha kazi za CHC kilikuwa kimekataliwa na Kamati ya Fedha na Uchumi kwa kuwa kuhamishia kazi za CHC katika Ofisi ya Msajili wa Hazina kililenga kuyaua mashirika ya umma nchini.
Alisema msajili huyo hajui hisa za baadhi ya mashirika ya umma yanayoendeshwa na Serikali kwa ubia na kwamba kitendo cha Serikali kuwasilisha kipengele hicho katika muswada uliowasilishwa bungeni siku hiyo, kilifanywa makusudi na Baraza la Mawaziri baada ya kulubuniwa na watu wasiokuwa na nia njema na mashirika ya umma.
Baada ya kutoa shutuma hizo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi na Waziri wa Tamisemi , George Mkuchika, walihamaki na kumtaka Zitto athibitishe kauli yake kwa kuwa wao walikuwa hawakulubiniwa na mtu ingawa ni mawaziri.
Hata hivyo, Mbunge wa Mwibara, Alphaxard Lugola (CCM) ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, aliungana na Zitto kupinga shughuri za CHC kuhamishiwa katika Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Alisema kuwa, msajili huyo hana uwezo wa kusimamia mashirika ya umma kwa kuwa ndiye chanzo cha kufa kwa Kampuni ya General Tyre ya jijini Arusha.
Kutokana na mjadala huo, Spika Anne Makinda alimtaka Zitto awasilishe usahidi wa shutuma dhidi ya Baraza la Mawaziri Juni 29 lakini ilipofika siku hiyo, ushahidi huo haukuwapo jambo ambalo lilimfanya amwongezee muda muda Jumatatu wiki hii.
Wakati Spika akiongeza muda huo, alisema Zitto alikuwa amemwomba amsaidie kupata nyaraka za Baraza la Mawaziri zilizojadili suala hilo pamoja na nyaraka za Kamati ya Fedha na Uchumi zinazohusu suala hilo.
Spika alisema hawezi kumsaidia mbunge huyo kupata nyaraka za baraza hilo kwa kuwa ni siri za baraza na kwamba msimamo huo uliwahi kutolewa na aliyekuwa Spika wa Bunge lililopita, Samwel Sitta.



CHANZO: NIPASHE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom