Bunge ni shaghalabagala kwasasa...

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Tangu nianze kufatilia siasa za Tanzania ni mara ya kwanza kwa bunge kuongozwa bila ratiba....jana kikao kimeanza spika akahairisha bunge baada ya maswali na majibu ili kutoa nafasi ya kupanga ratiba..

Leo kikao kinaendelea na kuna dalili ya ratiba kutojulikana kinaendelea nini baada ya maswali na majibu. Bila kuficha hii ni dalili mbaya kwa bunge na nchi kwa sasa.

Nchi inakwenda shaghalabagala na hakuna anayestuka, na viongozi wetu wanaona mambo ni sawa tu...na wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanadai ni dalili mbaya kwa bunge kukosa ratiba maalumu.
 
Lazima kuna pressing issue na itakuwa ni issue ya pesa. Nahisi ofisi ya bunge haina fungu la kuendesha kikao kwa wiki mbili hivyo bado wanavutana na serikali waingize nini kwenye ratiba na nini waache.

Maadam membe wetu humu jf mkuu Said Yakub aliyekuwa BBC London sasa ni ofisa habari wa Bunge letu, hopeful atatujuza kinachoendelea bila kuathiri ahadi za usiri kwa watumishi wa umma, hivyo tutajua nini kimejiri.

Naomba niwaandae kabisa kisaikolojia, msije kushangaa mkisikia kikao ni mpaka Ijumaa tuu!.
 
Si wamepitisha bajeti juzijuzi tu (5 months ago).

Kuna thread humu watu wanabishana kuwa serikali haijaishiwa. Sasa kama hawana pesa za kuendesha vikao muhimu vya bunge hii ni dalili mbaya sana. Haijapata tokea.
 
Ratiba iko na wakubwa na usishangae kikao kikaisha bila ya hoja za msingi. Najiuliza walikuwa wapi kama kazi yao ni bunge? Au issue ya jairo na mstaafu wa siku nyingi secretary luhnjo ina moto kwa hiyo inaandaaliwa namna?
 
yetu macho na miguu tu! wkishindwa kujadili mambo ya msingi naamini cdm kitawashtaki kwa wananchi
 
Si wamepitisha bajeti juzijuzi tu (5 months ago).

Kuna thread humu watu wanabishana kuwa serikali haijaishiwa. Sasa kama hawana pesa za kuendesha vikao muhimu vya bunge hii ni dalili mbaya sana. Haijapata tokea.

Bajeti iliyopitishwa ni kwenye makataratasi tu; serikali haina pesa kabisa; Zitto aliongea wakasema kwamba anaropoka lkn kumbe alikuwa sahii.
 
Mwana mama Makinda yuko kaziini kweli kweli.....no plan no job done....wait for the worst
 
Waliitisha bunge la nini wakati hawana ratiba? Makinda angalia hili jina lisiwe lina reflect watoto wa ndege walioko bado kwenye kiota na hawajawa na uwezo wakuruka na kujitegemea. Hii ndo ninayoiona umekuwa chini ya Mh Sitta kwa miaka yote hiyo umejifunza kwake na sasa unashangaza unaendesha bunge kama kiota cha ndege?
 
Kwani walikurupushwa kuja bungeni. Yaani sasa usanii nao umehamia rasmi bungeni. Kwa nini walimweka huyo 'mwanamke' kwenye hicho kiti ili hali kazi haiwezi? Iko siku atakataza maswali yasiulizwe kabisa mle ndani
 
Bajeti iliyopitishwa ni kwenye makataratasi tu; serikali haina pesa kabisa; Zitto aliongea wakasema kwamba anaropoka lkn kumbe alikuwa sahii.

mara zote CDM huwa wana advance information. Na hicho ndo kinachowatesa sana magamba maana wanajua wananchi wameshawaamini kwa kila wanaloongea kwani mwishowe hujidhihirisha hivyo
 
kuna kila dalili ya hizo ripoti kutosomwa hadharani kama walivyofanya kwa ile ya Lowassa
 
Mkuu nahisi hapa kuna ishu zinawatesa...
  1. Mswada wa katiba
  2. Ishu ya Jairo na Luhanjo
Inawezekana haya mambo yatawaumbua sana na kuonyesha umafia wao,na huyu mama atapata shida sana maana huku presha ya kisiasa ni kubwa na yeye anatamani kulinda maslahi ya chama na mafisadi...
 
Tumekwishaaaaaaaaaa sasa sijui viongozi bado awaoni tu au ubishi tu!
 
Kama Hawana Hela Wakakope tu kama kawaida yao.

Huyo Kiazi Mkullo si ndivyo anavyowashauri......endeleeni kukopa 2 nasema endeleeni kukopa 2
 
Mbona walijiandaa mapema kwa nini ratiba iwe bado haijaandaliwa?? Kuna kitu kweli nyuma ya pazia.
 
Back
Top Bottom