Bunge ni mhimili?

johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
713
692
Najiuliza sana kama Bunge letu kweli linaweza kuwa chombo kinachojitegema. waliotengeneza taratibu au kanuni za kuendesha bunge wanaweza kuthibitisha kuwa labda walikosea au walifanya makusudi kuondoa uhuru wa bunge hilo

kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza ni kwa nini bunge letu pamoja na wingi wa wana CCM limekuwa likiedeshwa puta na serikali? pamoja na mambo mengine nimebaini kuwa chanzo kinatoka kwenye dua ya kila siku ambayo hufungua bunge

utamsikia kiongozi w abunge siku hiyo pamoja na mambo mengine akiomba kuw Eee Mungu ... umsaidie rais wetu...! Ebo! kwa mujibu wa katiba rais ni sehemu ya bunge, kwanini kumtukuza yeye?. kwanini isiwe umsaidia Jaji mkuu? N.k

kama unaanza kwa kumuaomba mungu amsaidie fulani na kumwacha fulani basi hapo kwa hakika siku yako utaifanya kuwa ya kumtukuza mtu huyo am,baye ulimwombea kwa Mungu.

nafikiri watunga kanuni za bunge waliangalie suala hili
 
Sijajua kama mswada umepitishwa au la,maana haujajadiliwa walikuwa wanajadili kwanza cdm na tundu lisu.Hapo ndipo utakapojua kuwa majimbo yote yenye mbunge wa ccm yamefulia.Namuomba sita ampindue spika aliepo.
 
Kimsingi bunge ni muhimili unaojitegema kama ilivyo mahakama na serikali. Mihimili hii yote ni lazima iwe na uhuru wake na kutoingiliwa na muhimili au mihimili mingine.

Kwa kujua, kudhamilia na kwa makusudi serikali uwa inaingilia mihimili mingine (mahakama na bunge) katika maamuzi wao. Kwa mfano kwanini mwanasheria mkuu wa serikali, mawaziri, baadhi ya wakuu wa mikoa ambao kimsingi ni watendaji wa serikali waingie bungeni kutoa maamuzi. Kwa nini Mh. Spika awe ni mjumbe wa halmashauri ya chama tawala .... atatenda haki???? Kama haitoshi kwa nini Mh. rais ateue jaji mkuu na majaji wengine wakati ni muhimili mwingine tofauti????. Nadhani katiba mpya (ikiendeshwa vizuri) itakuwa ni jibu tosha kwa maswali haya na mengine ya wengine.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom