Bunge maalum la katiba kuondoa kipengele cha elimu ya mbunge kwa maslahi ya nani?

ligera

JF-Expert Member
May 17, 2014
2,646
1,167
Kila kamati inaposoma maelezo yao inataka kuondolewa kipengere cha elimu ya mbunge isiwe kidato cha nne, baadala yake kipengele hicho kisomeke awe anajua kusoma na kuandika kiswahili na kiingereza.

Chaguzi zetu nyingi tunazifahamu,kiasi kikubwa ni pesa tu .
Ukiwa na fedha ya kuhonga takukuru wasikufuatilie na fedha ya kuhonga wapiga kura,kununua vikanga,na vitishirt

Katika karne hii tuliyopo tunahitaji viongozi wa karba hiyo kweli ?, hata kama mnaona warioba alikosea basi japo mngeweka awe hata kidato cha pili.

Huku uraiani wapo vichaa wengi tu wanao andika na kuongea kiswahili na kingereza , tutegemee kuna siku watagombea na kupita (kwani kichaa si lazima aokote makopo),sasa hilo litakuwa bunge au kituko
Kwa jinsi shule za kata zilivyo nyingi kwa nini mbunge asijiendeleze , mnamtetea nani ?

Warioba hayakuwa maoni yake alipopendekeza elimu ya mbunge iwe kidato cha nne, yalikuwa maoni yetu wananchi.

ANG ALISHO: Zingatieni vitu vya msingi vinginevyo naona kila dalili ya katiba kukataliwa
 
Ha ha ha h h haha ha mm na Lema sugu na maji marefu tulishaa kosa sifa asante Sana wajumbe Wa bunge LA katiba
 
Ha ha ha h h haha ha mm na Lema sugu na maji marefu tulishaa kosa sifa asante Sana wajumbe Wa bunge LA katiba

hapo labda maji marefu, lakini sugu na lema sina uhakika na ulichokiandika, ngoja waje wanaojua.
 
Eti hawataki ubaguzi,kila raia awe na uwezo wa kugombea. Wanasahau kuwa kigezo cha umri wa miaka 21 nao pia ni ubaguzi na kigezo cha kujua kuongea na kuandika kiingereza na kiswahili ni ubaguzi kwani kuna wengi tu wanaotaka kugombea ubunge lkn wamekosa sifa hizo. Tuna safari ndefu sana kupata katiba bora kwa maslahi ya wananchi wote na si maslahi ya watawala. Karne bado wanataka wabunge wa ngumbaru!!!!Ama kweli huku ni kutapatapa kwa mfa maji.!!
 
Hofu kuu ya CCM ni kuondoka madarakani na/ au kupoteza majimbo mengi ya uchaguzi. Iweje wabunge waendelee kuwa darasa la saba? Nchi hii tutaendelea kweli? Kwa upuuzi huu,suala la wabunge kuwa angalau na elimu ya kidato cha 4 ccm hawataki. Wananchi kuwawajibisha wabunge,ccm hawataki,Serikali 3 ccm hawataki.
Ccm ninyi mnataka nini?
 
sometime huwa nahisi akina mbowe ni vibaraka wakuu wa ccm coz kila mara inapofikia kuna issue muhimu inajadiliwa kwa mustakabali wa nchi ambayo inaonekana itwaumiza ccm basi wao hususa na kuacha hao wapuuzi watengeneze watakacho!!yaani huu ni ujinga uliopitiliza ambao sijawahi kudhani kuwa kuna binadamu mwenye akili zake timamu kwenye karne hii anaweza kufikiria.watanzania wenzangu tuendelee kusubiri hiko kituko kinsachoitwa katiba kiletwe na kwa sababu sisi ni mazuzu tutakuja kudanganywa na juisi na kanga tutapitisha tu lakini kiukweli kabisa itakuwa ni katiba mbovu kuliko hii iliyopo na pengine itakuwa ni miongoni mwa katiba mbovu kabisa duniani.anyway,no wonder na sisi ni mazuzu so itakuwa KATIBA YA MAZUZU WA TANZANIA!
 
Nimepata hasira sana maana itakuwa ni muendelezo wa wajinga kuwatawala wasomi.

Nashauri kikwete aache maslahi binafsi na chama chake waliache hili swala la katiba maana limemshinda.

Tuache suala la katiba lowe la wananchi na sio wabunge. Lipi gumu hapa?
 
Mimi nawashangaa sana yaani hata vitu vya msingi navyo wanaviwekea question mark??? Kwahiyo ndio kusema nchi hii hadi wakati huu inashida ya waliokwenda shule kwahiyo hao wabunge waliomaliza kidato cha nne watakosekana?? This is constitutional amendment and not constitutional change.
 
Hofu kuu ya CCM ni kuondoka madarakani na/ au kupoteza majimbo mengi ya uchaguzi. Iweje wabunge waendelee kuwa darasa la saba? Nchi hii tutaendelea kweli? Kwa upuuzi huu,suala la wabunge kuwa angalau na elimu ya kidato cha 4 ccm hawataki. Wananchi kuwawajibisha wabunge,ccm hawataki,Serikali 3 ccm hawataki.
Ccm ninyi mnataka nini?

wanachokitaka watakipata mwakani , wewe waache tu.Wasione wananchi wapo kimya wakadhani ni mazuzu, wana yao waliyo yahifadhi moyoni.
 
Kibaya zaidi ibara zote zinazowabana ccm wamezipiga chini ila zilizonafaida kwao wameziacha kama zilivyo na kuziboresha zaidi.....

Tume ya jaji warioba nitaendelea kuirespect maisha yangu yote kwani ilitaka sisi wananch tuwe na meno zaidi kuliko watawala ila leo watawala ndiyo wamenoa makali ya meno yao ili watule vzr kbs
 
Kibaya zaidi ibara zote zinazowabana ccm wamezipiga chini ila zilizonafaida kwako wameziacha kama zilivyo na kuziboresha zaidi.....

Simple arithmetic ilikuwa ni kwa wapinzani kuandaa wasomi baaaas!!!!!
Wanadeka sana hawa watu, they gotta learn in a bit diff way!!!!

Ila na.upinzani nako sasa????!!!!!
 
Wanataka wafadhili wao, matajiri wasio na kisomo wasikose sifa za kugombea as with pesa wakiingia kwenye harakai za kisiasa wanashinda hata pasipo sifa ya elimu.
 
Kuondoa sifa ya F4 kuwa kiwango cha chini cha elimu, Ccm watawakosa wale Wabunge wanaoingia kusaidia Kamati ya Ufundi ya Wabunge wa Ccm.
 
Back
Top Bottom