Bunge livunjwe kwa sababu limejaa wahuni - Ole Sendeka

anamaanisha wapinzani ..anadai kuwa bunge limejaa wahuni wengi ndio maana anapendekeza livunje... Aliyasema haya wakati akihojiwa na mwananchi kwenye viwanja vya bunge.

Ni wabunge wa Chama gani waliojaza viti vya Bunge? Upinzani wana 80, CCM zaidi ya 230. Sasa anaposema limejaa wahuni si anamaanisha CCM ndo wahuni walojaa bungeni. Au ndo yaleyale ukishavaa yale magamba ya kijani, akili nayo inajaa kutu.

Athubutu kulivunja kama hatarejea na robo ya wabunge alionao sasa.

Sometimes hawa Magamba wanaongea pumba tu kila wakati. Uhuni, nani mhuni kat ya Mbunge anaehoji kukosekana kwa Umeme na yule anayeshangilia na kuunga mkono 100 kwa 100 hoja hata isiyo na masilahi kwa taifa.
 
Mbunge mhuni ni yule anayetetea maslahi yake binafsi na chama chake na si yule anayetetea maslahi ya Taifa na wananchi ambao wengi wetu ni hoi bin taabani na kila kukicha ni afadhali ya jana. Hapa kuna haja ya Mh. Ole afafanue anachokiamanisha.
 
Namkumbuka yule mama yetu "Mpole" Sofia Simba alishawahi kutuambia kwamba, kama Nchi hii ingekuwa inafuata utawala wa Sheria, Sendeka angekuwa ananyea debe kwa kumtia mimba mwanafunzi wa Shule ya Msingi. Sijui hii iliishia wapi? Lakini Mtu mzima kama Ole Sendeka kumpa Mimba mwanafunzi wa shule ya msingi wewe utamweka kwenye kundi la watu wenye busara au Wahuni!
 
Ole Sendeka amemuomba rais Jakaya Kikwete avunje bunge kwa sababu limejaa wahuni.
Source: mwananchi.

Hivi Sendeka anajua ni nini anakiomba! Coz nijuavyo mimi na niko tayari kukosolewa...Ni kwamba rais anapovunja Bunge ina maana anaitisha uchaguzi mwingine na kwa kuwa anajua hakushinda unafikiri ataruhusu nchi kuingia katika uchaguzi mwingine yet anajua kabisa kwa kufanya hivyo ni kikiondoa Chama Cha Magamba kuiongoza govt! Nway, kwetu sisi mbona ndo itakuwa nafasi nyingine ya kuwahenyesha magamba coz most of them have done nothing ni wizi tu ndo uliowaingiza huko....
 
anamaanisha wapinzani ..anadai kuwa bunge limejaa wahuni wengi ndio maana anapendekeza livunje... Aliyasema haya wakati akihojiwa na mwananchi kwenye viwanja vya bunge.
Sidhani kama alimaanisha wapinzani. Hawa hawajajaa humo. Waliojaa Jengo la Posho ni CCM.
 
Raisi hana mamlaka ya kuvunja bunge....... ila kuna wakati niliisha sema Mbunge 1 CDM = 5 CCM thinking capacity. sijawahi ona Mbnge wa CDM akisinzia bungeni.
 
Ole Sendeka amemuomba rais Jakaya Kikwete avunje bunge kwa sababu limejaa wahuni.
Source: mwananchi.

Yeye Ole ndiye muhuni kwa vile haelewi mambo yanayojadiliwa kwa maslahi ya taifa. Anataka tuendelee kufumbwa kama wakati wa chama kimoja
 
Raisi hana mamlaka ya kuvunja bunge....... ila kuna wakati niliisha sema Mbunge 1 CDM = 5 CCM thinking capacity. sijawahi ona Mbnge wa CDM akisinzia bungeni.

Hata Wasira hajawahi kusinzia bungeni ila alikuwa amekunywa dawa ambayo inasababisha usingizi ndio maana akasinzia, lakini kila kilichokuwa kinajadiliwa alikuwa pamoja nao. Na ushahidi wa hilo kaangalie kitabu cha kupokea Posho (ambayo ndiyo kipengele muhimu kwetu CCM) kama hakusaini!
 
kweli mzaz wabunge wa ccm weng wahun 2 hawana hoja wanashabikia uchama tuu mda wote badala ya kuwasilisha maon na matatzo ya mwananch!wahun wachakachulwe 2mechoshwa na hawa vilaza wa ccm
 
Samaki mkunje angali mbichi. Hili bunge limeharibiwa na watu wawili tu: Spika Anne Makinda na Mizengo Pinda.

Kupitia semina elekezi, Mizengo Pinda ameweza kuwaja hofu na nidhamu ya woga wabunge wa ccm kwa kile anaochoona ni 'kuleta umoja kwa chama'. Matokeo yake bungeni kumekuwa na 'sisi dhidi ya wao'. CCM kupitia kwa huyu Waziri Mkuu wameweka matatizo ya wananchi pembeni kwani kazi yao ni kuzomea.


Spika Makinda, haelewi na wala hataki kuelewa kuwa yeye ni Spika wa bunge la vyama vingi. And from day one alionesha kuwa yeye sio Spika ila mwenyekiti wa kikao cha wabunge wa CCM hivyo wabunge wengine wote ni watoto wa kambo na wategemee kula 'left-overs' Ukishaonesha waziwazi kuwa unambagua mtoto basi usishangae kuona Rebellious behaviour. Kwa mara ya kwanza watanzania tumeona wabunge 'hasa ccm-wanawake' wakipaza sauti, misemo ya kiswahili (mipasho) kana kwamba wako kwenye kitchen party. Kama Spika angekemea tabia hii siku ya kwanza tusingeona tunayoona leo, lakini kwa mshangao Spika naye alianza kutoa mipasho na hivyo kuwapa nguvu wana-mipasho wenzake. Matokeo yake samaki amekauka huwezi kumkunja tena!

Sasa hivi Bungeni imekuwa ni 'survival of the fittest'. Ni aibu ilioje kwa Tanzania, na mbaya zaidi Makinda ameharibu sifa ya wanamama katika safu ya uongozi kwa kiwango kikubwa sana.
 
Ni kweli ana haki ya kusema hivyo kwa sababu huu sio ule wakati wa kupitisha kila kitu kwa urahisi, lazima utokee mzozo
 
Olesendaka hajui akiwa katikati ya wahuni yeye ni nani? Uhuni hauna rika wala kiwango cha eliminate, uhuni mwingi 100% unafanywa na magamba ya ccm bila kujali umri wala jinsia mfano kuzomea kuunga mkono hoja mbovu na kuzipinga kwa nguvu haja za upinzani zenye tija kwa jamii.
 
Bunge likivunjwa na CCM imekwisha maana hakuna hata mmoja atarudi mjengoni hebu waache masihara kujifanya wao ndio wanajua sana kuliko wengine.
 
Olesendaka hajui akiwa katikati ya wahuni yeye ni nani? Uhuni hauna rika wala kiwango cha elimu, uhuni mwingi 100% unafanywa na magamba ya ccm bila kujali umri wala jinsia mfano kuzomea kuunga mkono hoja mbovu na kuzipinga kwa nguvu haja za upinzani zenye tija kwa jamii.
 
Wabunge wahuni ni wale wa kile chama ambacho kimeweza kufumbia ufisadi mkubwa wa fedha na raslimali za tz..................wahuni ni wale ambao wana uroho wa hali ya juu na ambao kamwe hawataki poso zao ziguswe kwa vyovyote vile..............kwa hakika wabunge wahuni ni wabunge wa ccm ambao wametufikisha hapa tulipo
 
Statement kama hiyo kwanza inawadhalilisha wapiga kura ambako "wahuni" hao na ni matusi kwa tafsiri nyingine. Huyo aliyetoa wazo hilo anatakiwa atuombe radhi sisi wananchi na afute usemi wake. Alichosema kinaleta maana tofauti. Vilevile nakubaliana na wale waliosema wabunge wengi ni CCM hivyo inawezekana wanahitaji si kutoa magamba tu bali hata sumu itolewe ili kuwe na amani Bungeni.
 
kweli bunge limejaa wahuni sitta lukuvi werema pinda ngeleja olesendeka sofia simba simba chawene anna makinda
 
Back
Top Bottom