Bunge Lisionyeshwe LIVE - Wabunge!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,723
Spika wa Bunge amesema kuwa baadhi ya wabunge wanaandaa hoja ya kuzuia vipindi vya Bunge kuonyeshwa LIVE kwa wananchi!
Ninavyochukulia: Huku ni kulewa Madaraka!...Wanataka wachape usingizi bila kuhojiwa na wapiga kura hawa!

CHANZO: Gazeti la Mtanzania leo 13/08/2012
 
Wamechoka kuigiza huku tukiwashuhudia live eeh? Na kuongezeana posho za kusinzia na kuzurura kila uchao? Wanatia aibu!
Utu uzima dawa. Moto hauzimwi kwa kuufunika na khanga. Jirekebisheni mambo huenda yakabadilika, no promises manake wananchi wamechoka.
 
Na ni lazima Wasira + Komba ndiyo wanaunda hicho kitu!

Wapuuzi kweli kweli!
Hakika kabisa, hao uliotaja wanahusika moja kwa moja, na amini usiamini lazima ni wa CCM wote!
Hakika hoja hiyo ikifanyiwa kazi wananchi tunapaswa kuonyesha live kuwa hatukubali upopompo huo!...
 
Wao wanafikiria tupo ile karne ya chama chao kimoja!

Watajuuuuuta kuukubali mfumo wa vyama vyama vingi!
 
Spika wa Bunge amesema kuwa baadhi ya wabunge wanaandaa hoja ya kuzuia vipindi vya Bunge kuonyeshwa LIVE kwa wananchi!
Ninavyochukulia: Huku ni kulewa Madaraka!...Wanataka wachape usingizi bila kuhojiwa na wapiga kura hawa!

CHANZO: Gazeti la Mtanzania leo 13/08/2012

Sijawahi kuandamana miaka ya hivi karibuni lakini yakiitishwa maandamano ya kupinga hii hoja mimi Kimbunga nitashika bango na kuwa mstari wa mbele. Hawa wabunge wetu wamepatwa na nini? Karne hii ya utandawazi, uwazi na uhuru wa kupata habari wao wanataka kutunyima kujua wanatuwakilishaje? Hivi wamesahau kwamba sisi ndio tumewatuma na tunatakiwa tujue wanatuwakulisha vipi? Wanataka kufanya siri?

Ama kweli madaraka kitu kibaya sana. Mtu akiitwa mheshimiwa basi anadhani anaweza kufanya analotaka? Mimi binafsi nataka tuendelee kupata habari za kibunge LIVE bila Chenga. Kama hawatimizi wajibu ipasavyo tuwaone wasitake kujificha.
 
Hakika kabisa, hao uliotaja wanahusika moja kwa moja, na amini usiamini lazima ni wa CCM wote!
Hakika hoja hiyo ikifanyiwa kazi wananchi tunapaswa kuonyesha live kuwa hatukubali upopompo huo!...

Mkuu PakaJimmy yeyote atakayefanya ama anayefikiria hilo ni wa kulaani awe wa CCM ama CDM au NCCR ama CUF. Mbona Mrema naye aliwahi kuonyeshwa akipata tano bora!
 
Last edited by a moderator:
Hoja ya hawa MPs wetu haina mashiko kabisa! Wanataka wapitishe mambo yao kule mjengoni sie bila kujua. Nonsense!
 
Sijawahi kuandamana miaka ya hivi karibuni lakini yakiitishwa maandamano ya kupinga hii hoja mimi Kimbunga nitashika bango na kuwa mstari wa mbele. Hawa wabunge wetu wamepatwa na nini? Karne hii ya utandawazi, uwazi na uhuru wa kupata habari wao wanataka kutunyima kujua wanatuwakilishaje? Hivi wamesahau kwamba sisi ndio tumewatuma na tunatakiwa tujue wanatuwakulisha vipi? Wanataka kufanya siri?

Ama kweli madaraka kitu kibaya sana. Mtu akiitwa mheshimiwa basi anadhani anaweza kufanya analotaka? Mimi binafsi nataka tuendelee kupata habari za kibunge LIVE bila Chenga. Kama hawatimizi wajibu ipasavyo tuwaone wasitake kujificha.

Mimi nitaenda kulala kabisa kwenye lango la kuingilia Bungeni kuwazuia wasiingie!.. Shame!
 
Mkuu PakaJimmy yeyote atakayefanya ama anayefikiria hilo ni wa kulaani awe wa CCM ama CDM au NCCR ama CUF. Mbona Mrema naye aliwahi kuonyeshwa akipata tano bora!

Hoja ya hawa MPs wetu haina mashiko kabisa! Wanataka wapitishe mambo yao kule mjengoni sie bila kujua. Nonsense!
Mimi nadhani ndio lile dai la Naibu spika kuwa WABUNGE WENGI WANAINGIA BUNGENI WAKIWA WAMELEWA POMBE NA SIGARA KALI KALI.
This is too abnormal!
 
Wabunge wengi wa CCM ambao kazi yao ni kuunga mkono hoja za kipuuzi ili kuilinda serikali, hata kama hoja hizo zinamuumiza mwananchi wamegundua kwamba wapiga kura wao wanaona mchezo wote na kwamba mwaka 2015 patachimbika huko majimboni kwao. Nadhani hii ndio sababu ya msingi ya hao wabunge kuja na hoja hizi kwani hata mimi katika pita pita zangu, nimeshuhudia hata wanachama wa CCM katika majimbo mbalimbali wenye nia ya kugombea ubunge kupitia CCM 2015 wanakwenda kwenye majimbo ya wabunge wa "NDIYOOOO" na kuwaonyesha mara nyingine video clips jinsi gani wabunge waliowachagua wasivyokuwa in touch na maisha ya wapiga kura; Sitashangaa kama hoja hii itapitishwa kwa vigezo kwamba bunge limekuwa la kihuni na lililokosa maadili kwahiyo wabunge wajirekebishe kwanza n.k;
 
Sijawahi kuandamana miaka ya hivi karibuni lakini yakiitishwa maandamano ya kupinga hii hoja mimi Kimbunga nitashika bango na kuwa mstari wa mbele. Hawa wabunge wetu wamepatwa na nini? Karne hii ya utandawazi, uwazi na uhuru wa kupata habari wao wanataka kutunyima kujua wanatuwakilishaje? Hivi wamesahau kwamba sisi ndio tumewatuma na tunatakiwa tujue wanatuwakulisha vipi? Wanataka kufanya siri?

Ama kweli madaraka kitu kibaya sana. Mtu akiitwa mheshimiwa basi anadhani anaweza kufanya analotaka? Mimi binafsi nataka tuendelee kupata habari za kibunge LIVE bila Chenga. Kama hawatimizi wajibu ipasavyo tuwaone wasitake kujificha.
Kimbunga mimi sitaandamana kwanza, nitakwenda Mbeya wanipe mbinu za kupopoa viongozi, ushanfahamu!

Halafu nifanye sahihisho katika bandiko lako, hatukuwatuma bali sisi ndio tumewaajiri. Tukisema tumewatuma watasema wakirudi watatupa habari. Tumewaajiri na kama waajiri tunatatka kujua wanafanya kazi tuliowatuma?
 
Mi naomba jina la aliyetoa wazo hilo, kama wanadhani sisi hatuwezi kuwapeleka kwenye ule MSITU wao, wathubutu, tutawapeleka tena mchana kweupe!
 
Kwa kuwa wanajua kabisa hakuna kitu wanachokifanya huko mjengoni,
wanaona aibu wapiga kura wao kuwatazama,
ni sawa na kusema wameshindwa kabisa kufanya kazi tuliyowatuma.
 
Siwezi kuwashangaa, nilisikiliza mawazo yao wakati wanaharakati wanapinga mfuko wa jimbo na sikuamini. Ni kipindi kile nilipong'amua kuwa hawa wabunge ni miongoni mwa watanzania wanaodhani wapo juu ya sheria.

Utasikia michango yao bungeni wakiwa wanawashambulia watumishi wa serikali kwa kula rushwa na huku wakiwataja majina kwa mbwembwe lakini ilipofika wao kula rushwa hawataki kabisa majina yao kutajwa!

Baada ya hapo wataamuru vyombo vya habari kutoandika habari ambazo ni "negative" dhidi zao! Huu ni ulevi usio na mfano na kama jamii itachelewa basi taifa litazidi kuongeza idadi ya "untouchables"!

Spika anathubutu kupokea hoja za hovyo kama hii? Wakati huwa anakataa zile zenye kujali maslahi ya Taifa. Hii ni aibu kwa watawala lakini pia litakuwa ni pigo kwa ccm.
 
Back
Top Bottom