Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge Linaweza Kumwondoa Madarakani Rais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Aug 13, 2008.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,604
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  “46A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshitaki rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.
  (2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba rais-
  (a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
  (b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba au
  (c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano”.
  ------------------------------------------
  Hicho kifungu C kinaweza kutumika kumuondoa Raisi madarakani.
  1) Akiwa nchini Ufaransa kwamba hajui umaskini wa Watanzania unatokana na nini.
  Akiwa na waandishi wa nje aliamua kuwa wazi na kuwaambia kwamba hata yeye hajui umaskini wa nchi yetu unasababishwa na nini.
  Tafsiri yake ni kwamba wakati anagombea urais ‘aliwadanganya’ Watanzania alipowaambia ataleta neema na maisha bora kwa kila Mtanzania.

  2 ) Aliporejea nchini na kutimiza miaka miwili Ikulu, aliwaambia waandishi wa nchini kwamba ahadi zote atazitimiza (ikiwamo ya maisha bora kwa kila Mtanzania, ambayo hajui sababu ya kwa nini Watanzania hawana hayo maisha bora na hivyo kuwa maskini). Huku ndiko ‘kudhalilisha’ kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kunakokataliwa na katiba.
  3 ) Rais akilihutubia Bunge Desemba 30 mwaka 2005 alisema: “Serikali ya Awamu ya Nne itaendeleza vita dhidi ya umaskini, ujinga na maradhi, tena kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya”. - Ataendeleza vipi vita wakati haelewi adui umasikini anakujakujaje.

  Nimeshangaa kuona kwamba hata pesa ya Rwanda na Burundi, nchi zilizokuwa na vita miaka mingi, ina thamani kuliko shilingi ya Tanzania. Amani tunayodai kuilinda kwa kila hali ni ya nini? Inatusaidia nini?
  Kama nchi zinazopigana vita ya wenywe kwa wenyewe baada ya vita watawala wanakuwa na adabu na kuwatumikia wananchi sawa sawa, basi na sisi tupigane.
  Baadhi yetu tufe kama kafara ili tuokoe maisha ya vizazi vijavyo, vinginevyo kwa ari hii, nguvu hii na kasi hii, Tanzania ijayo itakuwa maskini sawa na jalala na Watanzania wa kizazi kijacho watakuwa maskini sawa na vichaa na chokoraa wanaokula majalalani.
  3 ) Mimi sitembei na fuko la pesa -Kiti Cha Uraisi kimedhalilishwa
  4 ) Anasema serikali hii yenye kitivo cha sheria cha kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki, haina wataalamu wa kujua hilo! Hii ni aibu na kwa kweli kwa mkuu wa nchi kuwatangazia mataifa ya nje kwamba nchi yake haina wanasheria wa kujua mambo madogo kama hayo ni kukidhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano.
  Na wanasheria wa nchi hii sijui kwa nini hawajajitokeza kupinga kauli hii ya rais iliyowadhalilisha sana!

  Kama nchi zinazopigana vita ya wenywe kwa wenyewe baada ya vita watawala wanakuwa na adabu na kuwatumikia wananchi sawa sawa, basi na sisi tupigane.
  Source : Kalamu ya MWIGAMBA
   
 2. W

  WembeMkali JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2008
  Joined: Jun 16, 2007
  Messages: 282
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna taarifa kuwa siku chache zijazo ataanza safari ya kwenda Marekani.Zile trip za Iringa na Muheza zilikuwa ni cover tu kwa ajili ya safari ndefu ya Marekani.
  Na tatizo lake ni kuwa ziara hizi nyingi ni za kimatanuzi! na gharama zote hulipwa na fedha za walipa kodi!
  Na haelekei kuelewa kuwa kuna watu wanaishi kwa mlo mmoja na kukosa huduma muhimu za kijamii kama afya,maji,chakula n.k.
  Nafikiri kuna umuhimu wa kuanza kuprotest kila mahala atakapokuwa anatembelea ili japo kumpa signal kuwa makubwa yanaweza kutokea kama serikali yake itaendelea kupuuzia matatizo ya wananchi.

  Wembe.
   
 3. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 704
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwanini nyie watanzania mnaoishi huko nchi za ughaibuni msitusaidie haya mambo
  Kwa kuwa nyie mmeonyesha sana kuchoshwa na porojo za huyu Commedian, na kila akija mnataka kukutana naye eti kuzungumza naye, kwa nini pakiandaliwa vikao kama hivyo mvisusie kabisa na akienda pale ajikute yuko na balozi wake tu

  Labda ingeonyesha kuwa watanzania hawataki safari hizo zinazotugharimu mapesa kibao wakati watu wanakufa kila kukicha kwa kukosa huduma muhimu
   
 4. Dr.W.Slaa

  Dr.W.Slaa Verified User

  #4
  Aug 13, 2008
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 674
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kumwondoa Rais wakati Bunge lina zaidi ya Asilimia 80 ya Wabunge wa Chama Chake, na katika Bunge ambalo kila jambo linaloletwa na Serikali linaweza kuchanwa chanwa na hatimaye kuptishwa kwa asilimia 100 mmh! mmh! may be years to come? Jambo jema kuwa na hasira ya namna hiyo tunapuguswa hata hivyo.....
   
 5. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 16,047
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Kwani huku anakuja kukutana na watanzania ama wafadhili?
  Maana hata huu ubalozi huku si ni kwa ajili ya wawekezaji?
   
 6. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,742
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Mara ya mwisho nilienda kuangalia comedy hii 2005 mwishoni Mkapa alipokuja na Kikwete, sijaenda tena.

  Kinachotakiwa zaidi ya kususia ni ku organize protests, watu waende na mabango kumuonesha disapproval ya Watanzania.
   
 7. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,919
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  ..kwahiyo rais anatakiwa kuondolewa madarakani?
   
 8. M

  MiratKad JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2008
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 294
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...Bila shaka. Akafanye maigizo sehemu nyingine sio kwenye Urais.
   
 9. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,919
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  ..lets be real, this is wishful thinking!
   
 10. M

  MiratKad JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2008
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 294
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  One day your wish will be granted. Especially if we decide that we have had enough, and take actions. They might be temporarily painful but the result will be lasting. Hakuna atakae dhubutu kuchezea fedha na Haki za umma kiasi hiki tena.
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Aug 14, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 50,023
  Likes Received: 9,672
  Trophy Points: 280
  Siku hizi hakutani tena na Watanzania wote bali huchaguliwa kundi la watu mataahira ambao hawajali chochote kile kinachoendelea ndani ya nchi yetu na wala huwa hawaulizi swali hata moja.

  Nia yao kubwa ni kupiga picha na msanii ili wakawatambie wenzao na kumpa sifa kem kem kwa 'kazi nzuri anayoifanya kuongoza nchi' :(

  Kwa mtaji huu tutaendelea kuona picha za msanii 'akizungumza na Watanzania alipokuwa Marekani' ukweli ni kwamba wanaochaguliwa wote ni mataahira, nadhani ubalozi utakuwa unahusika katika kuwachagua watu hao ili 'wasimpe muungwana wakati mgumu na kumuumbua'
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,604
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  Hilo sio tatizo ,kwani ikiwa mtaweza kufikia hatua ya kudai jambo hilo ,basi Watanzania nao watasikia na kuona ,kupima na kufikiri,watazidi kuelewa umuhimu wa kura yao.

  Na kiasi itakuwa somo na kuona ,kumbe jambo hili linaweza kufanyika.Vile vile yanayotetewa ni maslahi ya wananchi au taifa kwa ujumla hivyo ,hata humo ndani ya CCM kuna mwamko fulani ambao umejitokeza siku hizi,japo hatujaona ukweli wa makeke yao ,au kuungana katika hoja zinazolitetea taifa (Pengine wamewahi ila sina kumbukumbu) na wabunge watokeao vyama vingine.

  Tuseme CCM hawawezi kujitokeza kudai kuwa Raisi aliyepo madarakani amekidharaulisha kiti cha Uraisi wa Tanzania , lakini Je hawa ambao ni vyama pinzani ambavyo vinatakiwa viwe vinapigilia msumari kila pale ambapo sheria inawaruhusu ,hivyo huoni kama hili amelitenda ni wakati muafaka kwa vyama au upinzani kusimama kwenye Katiba na kutumia kifungu hicho,hapa ni Tanzania hali ya wabunge kutoka Chama cha CCM inajulikana tofauti na nchi za Ulaya ambapo wabunge wanawathamini zaidi wananchi waliowapigia kura kuliko Raisi hata kama wanatoka Chama kimoja ,Mbunge ni raisi katika jimbo analotoka ,maana hata mtu akiumwa,akishitakiwa basi mbunge anapashwa habari kuwa fulani ameshitakiwa na tunaona hatatendewa haki,ikiwa mwananchi huyo yupo au amepata matatizo hayo,mbunge wao itambidi aijulishe serikali na serikali ni lazima ifuatilie kwa kutumia Mabalozi wao wa nchi za nje husika,na kama hakufuatilia na serikali nayo haikufuatilia basi inakuwa balaa kubwa sana na huonekana ni jambo la aibu kwa serikali nzima na wananchi wote hukaribia kuungana au huungana ndio ,ukaona raia wa nchi za nje wanaringa na hawana wasiwasi wanapofika nchi za kwetu si kwa sababu Marekani ni nchi yenye nguvu au nchi nyengine yeyote kwa kuwa tu ni ya kizungu lakini ule msimamo wa mshikamano baina ya wabunge na raia zake ndio unaowafanya waheshimike.

  Hivyo upinzani usingojee kupata idadi kubwa ya wabunge kwani msimamo wanaochukua ndio utakaowageuza wananchi kuchagua chama kingine badala ya CCM,kama ulivyosema labda Years to come ! ni sawa lakini miaka hiyo huanza na hatua moja ,vitendo vya ujasiri ndivyo vitakavyowaongezea wabunge na sio malumbano ya ukali na makeke ndani ya bunge,vitendo ambavyo wananchi wataviona vina ukweli ,kama hili ambalo kwa nchi za Ulaya tayari Raisi asingekuwepo ,huko wanategemea wananchi hivyo wabunge wote wasingeweza kukwepa kwa sababu tu Raisi anatoka Chama Chao na naamini na hapa ulingano huu wa kusimamia vifungu vya Katiba mkivianza na wananchi kuvielewa na nyie mkivitumia hivyo hivyo mlivyo basi itakuwa rahisi kwa years to come utekelezwaji kuwa ni jambo la kawaida na heshima ya kiti hicho itabakia milele na milele.
   
 13. Augustoons

  Augustoons JF-Expert Member

  #13
  Aug 14, 2008
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 397
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  unajua kwa jinsi katiba yetu ilivyo na hasa ukiangalia wording ya hiyo ibara ya 46A na mamlaka mengine aliyonayo Rais,wabunge hata kabla hawajafikia hitimisho la kmuondoa Rais madarakani ayari Rais anaweza kuwa ameshalivunja bunge kwa mamlaka aliyonayo na likelihood ya Rais kurudi madarakani ni kubwa kuliko wabunge aliowaondoa kwa kutokuwa na imani naye.Kama unavyosema Dr.Kutumika kwa ibara hiyo kunawezekana tu iwapo kuna majority oppositions na pia mamlaka mengine ya Rais kikatiba yakawa yamerekebishwa.Utaratibu wa kumuondoa umewekwa kuwa mgumu hivyo ili ishindikana kumtoa madarakani kiurahisi,kwani wakati ibara hiyo inawapa nguvu wabunge kumuondoa madarakani,kuna ibara inamruhusu Rais kulivunja bunge,kulihutubia akitaka, kutangaza hali ya hatari na vilevile kuna ibara inayosema atashika madaraka hadi kipindi chake kiishe,hivyo si mahakama wala mtu yeyote mwenye mamlaka ya kumuondoa madarakani.Hebu rudini nyuma kumbukeni kesi ya MWL.PAUL JOHN MUHOZYA V.AG ambapo alijaribu kumshitaki mwinyi kwa kuvunja katiba baada ya ZANZIBAR kujiunga OIC na hivyo kutaka mahakama itamke kuwa amevunja katiba na hivyo anapaswa kuondoka madarakani
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,604
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  Uwezo wa kumwondoa upo au haupo ? Sababu zipo au Hazipo ? Nia ipo au haipo ?
  Naamini kabisa ikiwa Wabunge watasimama kidete kuanzisha libeneke hili basi tutauona Uungwana wa Muungwana .
  Ikiwa amejitapa kuwa yeye ana uwezo mkubwa hivi nani asietambua kuwa raisi wa Tanzania ana mamlaka zaidi ya kiasi anachotakiwa awe nacho.
  Naona pengine mafisadi wana siri za ndani za Kikwete na hizo ndizo pengine wanazoringia nazo ,siri ambazo kama zipo ,na mafisadi watuhumiwa wakiamua kuzianika basi Kikwete itambidi ajiuzulu kikamilifu kuliko Lowasa maana pengine hata kwenye Chama atakuwa hafai ,kuna nini baina ya Kikwete na mafisadi ? hata Muungwana ikawa mgumu kuwachukulia hatua za nguvu anazotamba nazo kwenye Bunge letu ,maana kuwachekesha watu kwa kumtumbulia macho mtu na kumwambi ninaweza kuamrisha ukamatwe ,huku ni kujitangazia madaraka ya kiubabe, kuna msemo usemao na nataka nanyi muujue kwani ni wa maana sana na una elimu iliyojificha ,msemo wenyewe unasema kila kwenye masihara basi kuna ukweli fulani.
  Hivyo Raisi amesema kimasihara lakini kiundani kuna kajiukweli fulani.
  Wabunge ni lazima sasa wawe na meno au waonyeshe meno yao ili kukilinda kiti cha Uraisi kisiwe kinafanyiwa biashala na kutishana ,wabunge wanadhamana kwa wananchi hawakuchaguliwa kwenda bungeni kuonyesha meno.
   
 15. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,594
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kweli mumechanganyikiwa, Lakini mengine ni hivyo kwa kuwa taifa linapita kwenye transition, kutoka demokrasia iliyobanwa kwenda kwenye true democratic state.

  Taifa lina Mh. Rais ambaye anataka kuwezesha mifumo ifanye kazi as opposed na Rais wa kukurupuka, kuropoka na kukunya sura kama akidhani huo ndio urais.. huo ni Urais wa Miaka ya Arobaini.

  Wakati ameongelea Rushwa utagundua ndicho anachotaka kuwe na mifumo... sio mtu mmoja ndiye ategemewe kwa kila kitu....

  Mfano kwenye rushwa amesema yafuatayo:-
  -Kurekebisha tume ya maadili, sheria kanuni
  -Kuboresha sheria ya TAKUKURU
  -Kutunga sheria ya mchakato wa Uchaguzi - ndani na nje ya vyama.
  Baada ya hapo vyombo husika vitafanyia kazi...

  Kuna mambo mengi hamjaelewa mtaelewa baadaye ni ngumu kuelewa especially kwa kuwa mnatoka kwenye tawala zilizokuwa semi-dictactorship.

  Siku zote mabadiliko hayapokewi vizuri... hata Mkapa alichukiwa sana miaka yake ya Mwanzo wa Utawala wake... lakini eventually alivyoondoka alitoka kidedea.... mumesahau... the so called 'UKAPA"

  Marais madikteta wa kutoa siku saba Mungu atuepushe nao!
   
 16. BUSARA6

  BUSARA6 JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2008
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 304
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35

  Porojo nyiiingi hebu jaribu ku summarise hizo pumba zako!!
   
 17. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,604
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  watu kama nyinyi ndio mnaokaa kungojea mazungumzo baada ya habari .Na kufurahia kisa cha mazungumzo wakati ndani yake mna ujumbe lakini ninyi si wenye kufahamu kina cha mazungumzo baada ya habari.
   
Loading...