Bunge limekua kijiwe !

AK-47

JF-Expert Member
Nov 12, 2009
1,373
199
Nilikua naangalia bunge letu Live wakati wa mjadala wa mswada wa sheria ya madini cha kushangaza wakati wengine wakijadili kwa kina mswada huo muhimu baadhi ya wabunge walikuwa wakipiga soga kiasi cha kugeuza kabisa viti ili waangaliane vyema na kugonga mikono kunogesha maongezi yao kanakwamba wao hawahusiani kabisa na kinachoendelea. Najiuliza hivi bunge letu limekua kijiwe cha kupiga soga ?.
 
MIMI NAOMBA NIKUUNGE MKONO HICHO KITU NIMEKIONA HATA MIMI YAANI SI LIMEKUWA BALI NI KIJIWE HASWA! Nakumbuka kunasiku Mheshimiwa Zito Aliuliza swali wakati naibu spika ndio anakaimu kiti cha spika. Sasa baada ya kushindwa huku Naibu spika akitaka zito Anyamaze na akae. Naye Zito akishikilia Msimamo wake Mwisho NAIBU wa spika akamuambia Zito kwa ukali. '' Mh Zitto Kaa chini he e he ! HABARI ndo hiyo! '' na baadhi ya wabunge kucheka huku wakigongeana mikono. Hakika nilishangaa sana! Je si kijiwe hicho????
 
Basi kwa hali hiyo napenda kujumuisha maudhui yangu kuwa wabunge huwa wanaenda kujadiri kitu au ajenda ambazo zimeisha jadiliwa ni kupitisha mambo machache na kujifanya wana rumbana kwenye runinga na kuwapotezea wananchi sasa kama ni kweli bunge liko serious iweje wabunge wanakaa kupiga story za ushosti kwa matter nzito kama hii ya madini huku ikiendelea?? hivi mwisha wahi tizama bunge la Uingereza lilivyo na mabishano ya hapo kwa hapo na kelele nyingi na kumzomea hata G Brown au mtoa hoja?
 
MIMI NAOMBA NIKUUNGE MKONO HICHO KITU NIMEKIONA HATA MIMI YAANI SI LIMEKUWA BALI NI KIJIWE HASWA! Nakumbuka kunasiku Mheshimiwa Zito Aliuliza swali wakati naibu spika ndio anakaimu kiti cha spika. Sasa baada ya kushindwa huku Naibu spika akitaka zito Anyamaze na akae. Naye Zito akishikilia Msimamo wake Mwisho NAIBU wa spika akamuambia Zito kwa ukali. '' Mh Zitto Kaa chini he e he ! HABARI ndo hiyo! '' na baadhi ya wabunge kucheka huku wakigongeana mikono. Hakika nilishangaa sana! Je si kijiwe hicho????

Oh! my God, kama imefikia hatua hiyo basi hatuna bunge.
tatizo kuna wabunge wanachukulia ubunge ni kama ufalme kwani wana uhakika kila msimu ni lazma warudi mjengoni ndo maana wanafanya wanavyotaka bila hofu yeyote.
 
Bunge la Tanzania kwa miaka sasa limekuwa ni Bunge rubber stamp. Hakuna muswada wowote unaoletwa Bungeni ambao umeweza kuitingisha Serikali zaidi ya ule wa Richmond na huu wa Sheria ya Uchaguzi ambao imebidi urudishwe tena Bungeni baada ya kupitishwa kwa kuwa Mbunge mmoja makini alichachamaa.

Bunge hili pamoja na kwamba ni la vyama vingi kwenye suala la uwajibikaji na kutetea kwa nguvu zote hoja wanazozitoa linashindwa na Bunge la Chama Kimoja ambalo lilikuwa linawachemsha viongozi hadi wanachanganyikiwa! Rejea Kitabu cha Mwalimu Nyerere cha Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania. Wabunge wale pamoja na hoja zao potofu za kutaka kuvunja nchi walikuwa na msimamo na kuikomalia Serikali hadi kufanya Mwalimu aingie ulingoni kwa nguvu ya hoja.
 
Mimi sikubaliani na maoni kwamba tuna bunge la vyama vingi, Tanzania ina bunge lenye chama kimoja kwa sababu 90% of the MPs are from the same party how can we say ni bunge la vyama vingi??
 
Mimi pia nimeliona hilo...
Kisha la ajabu kubwa ni kwamba maswali mengi bungeni hujibiwa na mawaziri kwa kusoma yale waliyo nukuu toka karatasi zao na sii jambo ambalo waziri anatakiwa kufahamu majibu toka kichwani mwake kwa sababu mambo yote yanayoulizwa yapo ktk hatua ya Utekelezaji..Waziri anatakiwa kufahamu kafanya nini na kitu gani kina kwamisha.. Hiindio kazi yake na waziri anatakiwa kufahamu kila hatua ya sera ambazo tayari zipo ktk hatua hii na sii kunukuu vitu kama vile huyu waziri ni mtu alotumwa kujibu kwa niaba ya...

Pili, Majibu ya viongozi wetu wengi hayaridhishi hata kidogo na ajabu ni kwamba sijaona upande wa Upinzani kutoridhika na majibu ya mkato yanayotolewa na mawaziri..Tena ajabu ni kwamba Waziri anaweza kuja na kusema - NILIKUWA SIJUI, hivyo nitaliwakilisha kwa wahusika. Hapa inanichanganya zaidi kwani kama waziri alikuwa hafahamu na bado akapata muda wa kuandika majibu ya hoja iweje asiwe na muda wa kutafuta ukweli wa madai ya mbunge kabla hajaandika majibu yake, hivyo anapopanda jukwaani anakuwa na majibu yanayokwenda na wakati..

Hakika nimeona miujiza mingi tu bungeni na inasikitisha sana kuona wananchi tuna endelea kuwachagua viongozi kama hawa wasioheshimu kabisa Bunge na Spika wake...Jamani hawa watu (wabunge) wanapiga wameligeuza kabisa bunge kuwa kijiwe chao, na sidhani kama utovu huu unafanyika pia ktk mahakamani zetu..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom