VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Kila aliyenyooosha kiingereza kwenye uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki jana alichaguliwa.Wabunge wakiongozwa na Spika walihama kwenye hoja na kuhamia kwenye kiingereza.Imedhihirika jana.Waliojikwaa kwenye lugha hii,wamejikwaa pia kwenye kura. Wamedhalilishwa.Ni kweli kigezo pekee ni kujua kiingereza? Wangapi walikuwa Bunge hilo wakijua kiingereza lakini hawakufanya chochote?
Ni muda wa kubadilika.Ni muda wa kusema hata Kiswahili chapaswa kutumiwa. Tukisimamie Kiswahili chetu popote.Tutaeleweka na kutetea maslahi yetu vyema.Kiingereza si lugha yetu jamani..
Mzee Tupatupa
Ni muda wa kubadilika.Ni muda wa kusema hata Kiswahili chapaswa kutumiwa. Tukisimamie Kiswahili chetu popote.Tutaeleweka na kutetea maslahi yetu vyema.Kiingereza si lugha yetu jamani..
Mzee Tupatupa