Bunge limeahirishwa kutoka na ajali ya Mv Skagit

Habari zilizotangangwazwa hivi punde na itv ni kuwa meli ya zanzibar ijulikanayo kwa jina la skageti imezama na ilikuwa imebeba abiria 200..imezama katika kisiwa cha chumbe.
 
tunavuna tulichopanda kuwa na serikali ya kutoa ahadi tu lakini usimamizi na utendaji kazi ni zero.Mwaka jana walisema haitatokea tena kuzama kwa meli tanzania
 
Ooh! My God,save your innocent people from this! Kwani haya mambo yanatokea mara nyingi hivi? Serikali nayo vipi,haioni haya yanayotokea na kuchukua hatua?
 
Taarifa ni kuwa kuna boat imetoka dar kwenda kuokoa,lakini bado haijajulikana nini kinaendelea.
 
Inawezekana ni kweli meli inaitwa Skagit inadawa kuzama eneo la Chumbe ikiwa na abiria wapatao 200, meli ya Azam ya Kilimanjaro pamoja na meli zingine zinaelekea eneo la tukio kwa ajili ya uokoaji.
 
Fariour karimu anarepoti kuwa boat hiyo imepinduka kutokana na upepo mkali,meli inayofanya uokoaji ni kilimanjaro ikisaidia na baadhi ya boat nyingine,baadhi ya abiria wameokolewa na wako wanaelea na life jakets,meli ilikuwa ikitokea dar kwenda zenj.abiria wengine wanaendelea kuogelea kujiokoa..eneo hilo lina kina kirefu sana na mawimbi ni makali sana.
 
Boat ya Seagull inahofiwa kuzama na abiria zaidi ya mia nne maeneo ya chumbe!Boti mbalimabali za kasi zinaonekana maeneo hayo zikiwa katika za uokozi.
Nitawapa udate zaidi baadaye.
source. Niko maeneo ya Zanzibar serena inn nikishuhudia pita penya zikiendelea'
 
serikali dhaifu itakuja na maneno haya (TUMEJIPANGA AJALI ISITOKEE TENA) huku juzi boat imezimikia nungwi leo ajali
 
Duh!Mwenyezi mungu tuepushe na mabalaa haya yarabi! Kuna taarifa zozote za vifo?
 
Nimesikia kutoka Times FM radio (Breaking News) kwamba kuna boti iliyotoka leo Dar saa sita mchana iliyotegemewa kuwasili Zenji saa tisa na nusu ikizama maeneo ya Malindi. Tuwaombee walio katika dhoruba hilo ambalo limesababishwa na kuzimika kwa engine. Ni Boti yenye jina la "Seabus".
 
ITV wameprove ni Skagett, ilikuwa inatoka Dar, eneo lina upepo sana hivyo imepinduka ikazama. Rescue forces are on the way and Azam have dispatched one boat to support the rescuing process. Ee Mungu waokoe na kifo!
 
Back
Top Bottom