Bunge letu:zamani viwango;sasa vijembe

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Kimsingi,nimelimiss sana Bunge la Tisa lililoongozwa na Samwel Sitta kwakuwa lilikuwa Bunge la viwango(mijadala motomoto kwa mustakbali wa Taifa letu).Hili la sasa limejaa vijembe na miongozo ya Spika.Wana JF,tatizo la Bunge letu la sasa la Kumi liko wapi?
 
Choosen na bado utalimisss sana! nakumbuka bunge la kishsbiki wakati wa speaker Msekwa lilipitisha TAKRIMA waliokuwa wanapinga walionekana wapinzani leo hii iko wapi?ushabiki bungeni ni hatari kwa mustakabali wa taifa.
 
Sasa ndio wakati mzuri kabisa wa bunge letu kukua, maana kila mmoja anafahamu nafasi yake! Wakishatwangana ndio bunge linakomaa na busara zinaanza kutumika. Hakuna tena kuheshimiana kwa umri kwani kila mmoja ni mwakilishi ila hii ina faida na hasara. Nitapita baadaye kufafanua
 
Kila mbunge anatambua kuwa anawakilisha watu hivyo ana nguvu sawa. Huu si wakati wa kuwasikiliza akina Malecela ama akina Mzindakaya. Tena hata hao sisiemu wana makundi ambayo wao kwa wao wakitoa hoja za hovyo lazima wapeane shua na ikiwezekana baina yao kushabikia hoja za upinzani. Kama itaendelea hivi na kisha wakatwishana manundu jambo ambalo najua litaanzia nje ya kumbi za bunge basi ndio safari njema inaanza
 
Zaidi ni kuwa uhasama huu ambao unaanzia kwenye hoja na pia baada ya kutambua kuwa wapo wanaonufaika na wasio nufaika1 Wasionufaika ni dhahiri watazungumzia mambo ya wananchi ili kutaka kushinda uchaguzi ujao na nadharia nzima ya kuvua gamba. Ngumi ni muhimu kwa mfano Membe anaanznisha kambi yake binafasi pale UDOM wakati wanaotaka kuwania urais 2015 wengine kutoka CCM nao wanazo zao. Juzi tumemuona Lema naye akianzisha kambi huko na zamani kulikuwa na ile ya Zitto. Inakuhitaji muda kutafakari hizi mbinu za kisayansi za kisiasa zinazolenga kukutanisha wanasiasa na makundi yao lakini wa vyama tofauti, mwisho I can tell watatwishana makonde nje ya bunge na hasira zao zitaingia bungeni kwenye hoja na humo watapeana makonde kwa kuwa spika hana uwezo wa kuwakutanisha nje ya bunge. Nitarejea tena
 
Back
Top Bottom