Bunge letu na mustakabali wa taifa letu! Nini mchango wetu kama wazalendo?

Mboja

Senior Member
Sep 29, 2010
157
23
Juzi niliweza kufuatilia majadiliano Bungeni. Nilifurahishwa na umakini, ujasiri na uzalendo wa Lissu, Zitto na Mnyika. Kwangu mimi niliona hawa ndio aina ya Wabunge ambao tunawahitaji. Kwanzakabisa, nina hakika wanasoma miswada kwa umakini mkubwa, wanafanya consultation na wanapitia taarifa mbalimbali ili kuweza kujenga hoja zao vizuri. Kwa maneno machache wanafanya home work zao. Ndio maana wanaweza kuhoji, kukosoa na kupendekeza mabadiliko. Kama wangekuwa hawasomi wangeweza vipi kufanya hivyo??

Aidha wanahudhuria vikao vya bunge bila utoro na wanasikiliza kwa makini. Wanatumia muda wao kusoma machapisho mbalimbali. Hawapotezi muda katika mabaa na wala hawaendi kufanya biashara zao binafsi kama wafanyavyo walio wengi. Wengine tunawaona hapa Dar wakati Bunge linaendelea Dodoma.

Mwenendo wa wabunge hawa ni tofauti kabisa na wabunge wengine, ambao nina hakika hawasomi hata hizo budget na miswada mbalimbali. Ndio maana hawana cha kuchangia wala cha kuhoji. Wao wanasubiri waseme ndiooooooooooo!. Utaratibu wa Siofaa kabisa wa kufanya maamuzi.

Baada ya kufuatilia na kuyaona haya nimejiuliza maswali kadhaa:

1. Kwa nini wabunge wa CCM wana behave namna hii? kwa nini hawahoji critically? Kwa nini hawaisimamii serikali?

  • Sina majibu ya kuridhisha sana lakini yafuatayo yanawezekana. Inaonyesha kuwa wamepewa maelekezo kutoka ngazi za juu kuwa wasiihoji serikali, na atakayefanya hivyo anaweza hata kufukuzwa ndani ya chama na hivyo kukosa Ubunge. Hakuna uhuru wa kutoa mawazo ndani ya Chama.
  • Yawezekana kuwa kila Mbunge anajiona kuwa yeye ni Waziri au Naibu Waziri au Mkuu wa Mkoa mtarajiwa. Namna ya kufika hapo si kuchapa kazi na kuwa makini katika utendaji wako bali ni kwa kuwa kada na mtetezi mkubwa wa sera za serikali hata kama hazina maana yoyote.Hivyo kila Mbunge wa CCM anajipendekeza kwa tabaka tawala kuwalinda ili nao watawala wamkumbuke katika ufalme wao. Jipendekeze zaidi ili upate ulaji, huo ndio mkakati.
  • Sababu nyingine, yawezekana kuwa hata hawajali kuwa kwa namna wanavyo behave ndani ya Bunge wanaweza kupoteza kura. Hawajali kwa sababu zifuatazo:
  • Wanafahamu kuwa ni wananchi wa mijini tu ndio wanafuatilia vikao vya Bunge. Wananchi wanaoishi vijijini, ambako kuna wapiga kura wengi, kutokana na matatizo yao lukuki sina hakika kama wanafuatilia mijadala ya bungeni. Kwanza, hawana muda kutokana kazi zao za shurba, maisha yasiyokuwa na uhakika, umaskini, wanaishi katika giza bila umeme, hawapati taarifa kwa njia yoyote ile. Magazeti hayafiki, machapisho mbalimbali yanaishia mijini, wanahangaika na kupata maji safi, na mambo mengine. Hivyo hawana muda na hawana uwezo wa kufuatilia mijadala hii. Hali hii ni neema kwa Chama cha Mapinduzi. Ndio wanalotegemea. Ndio maana hawachukui hatua za dhati kuwaondoa wananchi hawa katika hali ya umaskini au ufukara (abject poverty).
  • CCM wanafurahi kuongoza taifa la watu wajinga ambao wamekata tamaa. Wanachofikiria ni namna ya kupata mlo mmoja tu kwa siku hawa hawana habari na sheria ya Fedha 211. Kwa kutambua hilo, CCM hawajali na ndio maana wana behave namna wanavyo behave. 80% ya watanzania wanaishi vijijini na maskini wanategemea jembe la mkono.
  • Unapotaka kuwanyonya watu create umaskini wa kutupa, ukifanya hivyo utaweza kuwanyonya kwa kadri unavyotaka. Ndivyo ambavyo CCM wamefanikiwa kufanya. Watu maskini sana wanakuwa waoga, wanaacha kufikiri, wanadanganyika hata kwa kilo moja ya chumvi. Hata mtu akitokea akawatetea wao wanaweza kumuona huyo ndio adui na wakampiga mawe ilhali anawatetea wao na yule anayewanyonya wakamtukuza na kumsifia. Ndipo hapo tulipo. Wapo watu wengi tu wanawatete wakusanya posho. Wako buisy kukusanya posho.
  • Personally, ninao mfano mzuri sana. Niliwahi kushiriki katika kuandaa workshop ya Wabunge miaka ya zamani. Nilichoona nilistajabu sana. Workshop ilifanyika Bagamoyo. Asubuhi ukumbi ulikuwa umejaa, tulipolipa posho na kwenda katika chai saa nne. Baada ya kurudi kutaka katika chai ukumbi ulikuwa mtupu kabisa. Tulipofuatilia tukaambiwa kuwa wamewasha mashingingi na kukimbilia Dar ili kuwahi posho katika kikao kingine kilichokuwa kinaendelea Dar. Tamaa ya fisi anayetaka karamu zote mbili.
2. Ztto, Lissu na Mnyika wataendelea kupambana na kundi kubwa linalowapinga na kuwakejeli mpaka lini?
  • Wapambanaji hawa wanafanya kazi nzuri ya kijasiri, lakini tujiulize watafanya hivi mpaka lini? kwani nao ni binadamu. Kuna wakati naogopa sana, nasema kuwa watafika mahali nao watachoka au watakata tamaa. Naomba Mungu mawazo yangu na fikra zangu zisiwe sahihi. Naomba Mungu awatie nguvu waendelee na ninawaambia kuwa wanaingia katika historia, vizazi vitawakumbuka kuwa, walifanya jitihada kupinga ufisadi wa kimfumo, ufisadi unaolindwa na sheria na kanuni gandamizi. Mafisadi ili wale vizuri wanatunga sheria za kulinda ufisadi. Wanajipa mamlaka kisheria ya kusamehe kodi ili wale, ili waweze kuchota mabilioni toka serikalini kufadhili uchaguzi, ili wakae madarakani milele na ili waendelee ku create umaskini na woga ili wananchi waendelee kuwa vipofu na kushindwa kuona ufisadi wa kimfumo.
  • Nawaomba msikate tamaa. Great people waliweza kutengeneza history. Leo historia katika sehemu mbalimbali duniani zimebadilika kwa sababu ya ujasiri na ushupavu wa watu. Mzee Mandela ametengeneza historia, watu kama kina Nkurumah, Chee, Castro, Carbral, Mwalimu Nyerere, Martin Luther King, Malcom X, Lincon, Lumumba n.k. These are few great people ambao wametengeneza historia. Leo tunazungumza tunayozungumza kwa sababu yao. Na nyinyi msikate tamaa, huenda mkaingia katika historia kuwa mlibadalisha Taifa hili kutoka katika umaskini kwenda kuwa Taifa lenye maendeleo, toka Taifa ombaomba kwenda taifa lenye heshima ya kujitegemea. Ndio kuomba ni aibu.
3. Ili kuwatia moyo tunafanya nini?
  • Hili linahusiana sana na suala nililoeleza hapo juu. Kama wananchi wazalendo ni lazimatutambue mchango huu adhimu wa Wabunge hawa. Ni muhimu tuwa - reward kwa kutambua tu kwani wanafanya kazi nzuri. Hatuwezi tukaa kimya na kuwaachia watu wa nje ndio watambue mchango wa Wabunge hawa. Nafikiri tuna kila sababu ya kutambua mchango wao. Hili litawatia moyo na pia linaweza kuwafanya Wabunge wengine nao waige mfano huu.Hivyo basi, ninalileta kwenu ili tuchangie tunafanya nini kutambua mchango huu adhimu wa taifa letu. A small event, will be an ideal. Mnasemaje?


Thanks
 
Back
Top Bottom